Fahari ya Serengeti

Wednesday, August 30, 2017

MRADI WA TOKOMEZA UKEKETAJI SERENGETI WAMWAGA KOMPUTA KWA WADAU

 Meneja wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na Wadau wengine wilayani humo kwa ufadhili wa UN WOMEN Godfrey Matumu kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu kulia  Komputa 50 zenye thamani ya Tsh 54 mil kwa ajili ya  wadau mbalimbali ili kuwawezesha kutunza kumbukumbu na kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia vizuri.
Komputa hizo za mezani na Mpakato zimetolewa kwa taasisi za umma kama Polisi,Mahakama,Elimu Sekondari na shule za msingi ,Utawala ,za dini,mashirika yasiyo ya kiserikali.
 Dc Nurdin Babu kushoto amemkabidhi Ded Juma Hamisni kwa niaba ya wilaya

Wadau wa Mradi wa Tokomeza ukeketaji wakiwa katika picha ya pamoja

Sunday, August 27, 2017

595 WAPATA KIPAIMARA PAROKIA YA MUGUMU SERENGETI

 Askofu wa jimbo katoliki Musoma Michael Msonganzila akiwa katika picha ya pamoja na Alice Anthony kushoto na Sweetbertha Anthony kulia mara baada ya kutoa kipaimara kwa waumini 595 katika Parokia ya Mugumu,amesisitiza watu kumjua Mungu ,kuishi maisha matakatifu ambayo yanampendeza Mungu.
 Baadhi ya wanafunzi wa Little Flowers wakiwa nje ya kanisa wakisikiliza mahubiri wakati wa misa takatifu ya Kipaimara kanisa Katoliki Mugumu Serengeti.
 Alice Anthony akivishwa taji na Irene muda mfupi baada ya kupata Kipaimara
 Hongereni



Saturday, August 26, 2017

BABA ASKOFU AWASIFU WANAJUMUIYA YA MT.MARIA MAMA WA MUNGU





Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma Michael Msonganzila wa tatu toka kushoto amewasifu wanajumuiya ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu  Parokia ya Mugumu Serengeti kwa mshikamano wao walionao katika kusali na shughuli nyingine zinazowahusu,amewahimiza kudumisha umoja huo,huku akikemea wakristo wanaojihusisha na matendo mabaya ambayo yanaharibu sifa yao.wa pili kushoto Paroko Alois Magabe,wa kwanza kulia ni Vedastus Makaranga na masisita

Baba Askofu anamwombea Josephina Bakhita mama mzazi wa Anthony Mayunga ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa sukari na moyo kwa zaidi ya miaka miwili,Mungu aliyefufua watu atamponya na maradhi hayo
Picha ya Pamoja imepigwa
Nyimbo zimeimbwa na kwaya ya Mt.Fransisko wa Asizi


Ibada inaendelea


Anawalisha neno waumini


Wakati wa mageuzo
Pokea mwili wa kristo






ASKOFU MSONGANZILA AHIMIZA WANAJUMUIYA KUISHI MAISHA YA KIKRISTO

 Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma akiongea na Josephina Bakhita wa Jumuiya ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Parokia ya Mugumu wilaya ya Serengeti baada ya kusali misa katikaJumuiya hiyo na kumwombea na kumpa baraka mama huyo ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya sukari na Moyo,katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na waumini wa jumuiya mbalimbali wakiongozwa na Kwaya ya Mt,Fransisco wa Asizi Parokia ya Mugumu,amehimiza wanajumiya kuyaishi maisha ya somo wao Bikra Maria ya upole,unyenyekevu na imani huku wakiwaombea na wengine.

Baba askofu Msonganzila yuko katika ziara ya siku nne ya kichungaji katika Parokia hiyo ambapo mbali na shughuli nyingine atatoa Kipaimara kwa watu zaidi ya 400.
 Baba Askofu Michael Msonganzila akitoa maombi na baraka kwa Josephina Bakhita.

Baba Askofu Michael Msonganzila akiongoza sala ya baraka kumwombea Josephina Bahkita,kushoto ni Paroko wa Kanisa katoliki Mugumu Alois Magabe na Sista Rozina Massawe.

Thursday, August 24, 2017

WAZEE WA MILA KOO YA INCHUGU YATOA TAMKO

Baadhi ya wazee wa koo ya Inchugu kata ya Machochwe wilaya ya Serengeti wakiweka sahihi ya makubaliano ya  kuachana na ukeketaji katika koo hiyo ,uamzi huo umefikiwa na kutangazwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamakendo.
Wasanii wa Nuru Sanaa wakitoa elimu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike katika kijiji cha Nyamakendo muda mfupi kabla wazee wa mila hawajatoa tamko.
Wazee wa mila wakijadiliana mambo baada ya kutoa tamko la kukomesha vitendo vya ukeketaji katika koo ya Inchugu wilaya ya Serengeti na kuahidi kufanya Jando bila ukeketaji
Wasanii wakiendelea kutoa elimu ya madhara ya ukeketaji

Meneja Mradi wa Tokomezza Ukeketaji Serengeti Godfrey Matumu akiweka saini baada ya wazee wa  mila kukamilisha zoezi la kusaini makubaliano ya kukataa ukeketaji na kuanza mikakati ya jando bila ukeketaji.


William Mtwazi(Mwanasheria)kutoka LHRC ambaye ni afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti akitoa ufafanuzi kwa wazee wa mila wa koo ya Inchugu namna ya kusimamia maamzi yao ya kupiga marufuku ukeketaji na kuanza jando bila ukeketaji

Wazee wa mila na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja
Mjadala unaendelea wao kwa wao na hatimaye wakatoka na tamko la kupiga marufuku ukeketaji
Anasaini makubaliano yao ya kupiga marufuku
Wanaendelea kusaini
Watoto wameshuhudia makubaliano ya wazee wa mila kisha kutoa tamko ambalo linawaweka huru watoto wa kike ambao wengi wakati wa msimu wa ukeketaji hukimbia na kutafuta hifadhi maeneo mengine.
Biashara inaendelea lakini wakisikiliza msimamo wa wazee wa mila
Wanafuatilia mkutano wa wazee wa mila huku biashara ikiendelea
Hawa wote wameshuhudia tamko la wazee wa mila,huku wanawake wakidai kuwa kama hawatabadilika familia nyingi zitaishi kwa amani kwa kuwa kumekuwa na migogoro mingi wakati wa ukeketaji ukifika ambapo wanawake wanaowatetea watoto wao wamekuwa wakifukuzwa nyumbani
Kisha biashara zikaendelea kama kawaida

Wednesday, August 23, 2017

WAZIRI APOKEA MRADI WA NYUMBA ZA SH 1.4 BILIONI

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe  kushoto,Balozi wa Ujermani nchini Tanzania  Dk Detlef Wachter katikati na Afisa Ujilani Mwema shirika la Frankfurt Zoological Society Masengeri Tumbuyo kulia wakikata utepe kama ishara ya kuzindua nyumba nne za watumishi na ofisi tatu za watumishi wa Idara ya Ujilani Mwema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilizojengwa kwa Ufadhili wa Serikali ya Ujermani  kupitia Benki ya Maendeleo ya nchi hiyo KFW kwa thamani ya sh 1.4 bil,lengo likuwa ni kuhakikisha watumishi wengi wanahamia Fort Ikoma ambako ni nje ya  ili kulinda na kuhifadhi Mfumo wa Ikolojia ndani ya Hifadhi hiyo.



 Meneja Mahusiano wa Tanapa (mc)wa shughuli hiyo Paskael Shelutete akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la Msingi mara baada ya Waziri na Balozi kukabidhiana nyumba hizo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akipokea funguo za nyumba nne na ofisi tatu toka kwa Balozi wa Ujermani hapa nchini Dk Detlef Watchter zilizjengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujermani kwa thamani ya sh 1.4 bilioni kwa ajili ya wafanyakazi wa Idara ya Ujilani Mwema hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

 Waziri akiangalia mashine aina ya Hydroform ambayo wanaitumia kufyatua matofali ya gharama nafuu na ambayo hayachomwi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira,mashine hiyo ina uwezo wa kufyatua matofali 3000 kwa siku,inatumia mafuta ya dezeli lita 10 kwa siku.


 Wnashiriki zoezi la kufyatua matofali
 Wakiangalia matofali yaliyokwisha fyatuliwa
 Waziri Maghembe akimakbidhi funguo za nyumba nne na ofisi tatu Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Ujermani hapa Nchini.
 Burudani kutoka kikundi cha COCOBA Bonchugu ilikonga nyoyo za watu
 Waziri akikagua nyumba na ofisi kabla ya kuzindua

 Balozi wa Ujermani hapa nchini Dk Detlef Wachter akiwa na tofali alilofyatua kwa mashine ya Hydraform

 Moja ya nyumba ya watumishi iliyokabidhiwa

 Wasomee jiwe limeandikwaje?
 Mc Shelutete akifanya yake
 Wanafuatilia taarifa kutoka kwa viongozi mbalimbali

 Asante sana kwa msaada wa nyumba tunaomba mkamilishe mpango wa maji kutoka Borogonja na kituo cha Taarifa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti anasikika akisema Waziri
 Picha mbalimbali za pamoja zilipigwa

Walizungukia maeneo