Fahari ya Serengeti

Friday, June 9, 2017

GARI LA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI LAGONGANA NA PIKIPIKI YA POLISI.

 Gari la halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara likiwa mtaroni baada ya kugongana na pikipikiya Polisi iliyokuwa inaendeshwa na mkuu wa usalama barabarani wilaya,Inspekta Benson Omar ambaye amevunjika mguu,
 Ajali ajali.
 Watua wakiangalia gari la halmashauri lililopata ajali.

 Pikipiki ya Polisi iliyopata
 Gari la halmashauri lililopata ajali



UCHIMBAJI DHAHABU MERENGA SERENGETI WENYE LESENI WAKATALIWA NA WANANCHI

 Wakazi wa kijiji cha Merenga wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo hilo Marwa Ryoba na Mwanasheria wa Halmashauri wamesema hawatawaruhusu watu waliopewa leseni ya kuchimba dhahabu kijijini hapo kwa kuwa wenye mashamba wameishashirikishwa,wamekubaliana kuwa serikali ya kijiji ikate leseni na wananchi wachimbe kupitia kwenye vikundi vyao.
Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba wa pili kulia akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Merenga ambapo alikwenda kwa ajili ya kusikiliza matatizo yao kufuatia mvutano kati ya wenye mashamba,wananchi na waliopewa leseni ya uchimbaji dhahabu kijijini hapo.

Hata hivyo imebainika kuwa wenye leseni hawakuwashirikisha wenye maeneo,na hawana muafaka ,hivyo wameazimia kuwa leseni yao ifutwe ili serikali ya kijiji ikate leseni na wananchi kupitia vikundi vyao wachimbe,wa kwanza kulia ni Mwanasheria wa Halmashauri Veronica Luvanda,wa kwanza kushoto ni afisa mtendaji wa kijiji, na Kaimu Mwenyekiti wa kijiji,Picha zote Serengeti Media Centre.

Thursday, June 8, 2017

MKANGANYIKO WA SHERIA CHANZO CHA KUSHAMIRI UKEKETAJI

 Wasiriki wa mafunzo ya Kampeini kuondoa ukeketaji Tanzania kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mara wakiendelea kupata dozi,hata hivyo wamesema migongano ya sheria ya Mtoto,Makosa ya Jinai,Ndoa na mikataba mbalimbali ya kimataifa hailengi kuwanusuru watoto wa kike dhidi ya ukatili huo.
 Mwezeshaji akipitia mada kabla ya kuwasilisha.mambo ya elektroniki
 Wanafuatilia mada


 Wanafuatilia kwa makini
Wakili Hamisi Mkindi akimwaga sera .

KAMPEINI KUONDOA UKEKETAJI TANZANIA YATUA KWA MAHAKIMU,POLISI NA WATENDAJI WA HALMASHAURI MARA

 Wakili Hamisi Mkindi wa LHRC akitoa mada wakati wa mafunzo ya Kampeini Kuondoa Ukeketaji Tanzania kwa mahakimu,maafisa wa Polisi na Watendaji wa Halmashauri Mkoa wa Mara ukumbi wa Giraffe Mugumu Serengeti.
 Wanafuatilia mada
 Mada zinaendelea kutolewa.
 Ana mwaga sera

 Washiriki toka wilaya za Musoma ,Tarime na Serengeti wakifuatilia mada

 Wawaweshaji kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)
 Picha ya Pamoja ilipigwa


Monday, June 5, 2017

UJENZI WA HOSPITALI,MBUNGE/MWENYEKITI WACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI

 Mbunge wa jimbo la Serengeti kulia Marwa Ryoba akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti ambayo inaendelea kujengwa kwa michango ya wadau mbalimbali.

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini kulia akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo inajengwa kwa michango ya wadau na serikali.
 Kazi ya kupiga lipu inaendelea


 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiangalia kazi ya ujenzi wa Chujio katika bwawa la Manchira.
 Anaangalia kazi zinavyoendelea


 Maandalizi ya jiwe la Misngi hospitali ya wilaya ya Serengeti ambayo uzinduzi wake utafanywa na makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu.



WALIOJERUHIWA NA NYATI NYAMISINGISI SERENGETI WAFIKISHWA HOSPITALI YA WILAYA

 Mtoto aliyejeruhiwa na Nyati katika kijiji cha Nyamisingisi wilayani Serengeti Mkoa wa Mara akiwapokelewa katika hospitali Teule ya Nyerere kwa ajili ya matibabu,nyati huyo amejeruhi watu saba na kati yao wanne hali zao si nzuri.
 Makeruhi wakiendelea kupokelewa hospitali kwa ajili ya matibabu.
 Miongoni mwa majeruhi.






 Wanapelekwa kwa daktari kwa ajili ya matibabu.