Fahari ya Serengeti

Thursday, February 8, 2018

MATUMIZI YA MAJI YASIYOSAFI NA SALAMA CHANZO CHA MAGONJWA

 Wanafunzi wa shule ya Msingi Gantamome kata ya Busawe wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa na mmoja wa wakazi wa kijiji hicho wakiangalia kisima cha maji ambayo wanatumia kunywa ingawa si safi na salama na inadaiwa ni chanzo cha ongezeko la magonjwa yanayosababishwa na maji,hata hivyo Mradi wa RAIN unaotekelezwa na Amref Health Africa kwa ufadhili wa Coca cola Foundation.

 Wanachota maji
 Murojo Malembo afisa toka Halmashauri ya wilaya ya Serengeti akisisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji.
 Wanachora mipaka ya kijiji
 Wanafunzi wa Nyabihore sec wakiangalia ramani

 Elimu inatolewa



TUJIKUMBUSHE MATUKIO SIKU BIASHARA UNITED INAPANDA LIGI KUU

 Miongoni mwa mambo yaliyokuwa kivutio ni huyo ndugu aliyevaa sura iliyowaacha wengi na maswali mengi
 Dc Musoma akiwa na baadhi ya watu waliokuwa wakizunguka uwanja kama watu wa tamaduni,kamati ya ufundi,ingawa inadaiwa ilikuwa ni mbinu za ushindi.
 Anashangilia
 Mshike mshike uwanjani ,mashabiki wakishangilia baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa

 Kila mmoja kivyake lakini anashangilia
 Kazi imekwisha sasa ligi kuuuuu
Biashara United Ligi KUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

Saturday, February 3, 2018

MRADI WA RAIN WAWAJENGEA UWEZO WANANCHI UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI

 Wakazi wa kijiji cha Nyansururawilaya ya Serengeti wakiwa katika kikao cha kujadili namna ya kutunza vyanzo vya maji,na kuchimba vyoo bora kupitia Mradi wa RAIN unaotekelezwa na amref health tanzania kwa ufadhili wa Cocacola Foundation .

 Mijadala ya Utunzaji wa vyanzo vya maji unaendelea.


 Wanafunzi wa shule ya msingi Nyansurura wakiwa wakishiriki mjadala pamoja na jamii

 Wanachora ramani ya kijiji


MIAKA 41 CCM VIONGOZI WAKEMEA WAAHIDI KUWASAKA WALIOHUJUMU MRADI WA MAJI RUNG'ABURE

 Dc Serengeti Nurdin Babu ameahidi kuchukua hatua kwa  wakazi wa kijiji cha Rung'abure watakaobainika walihusika kuhujumu mradi wa Maji kwa kukata mabomba na kusababisha wananchi zaidi ya 3200 kuendelea kuteseka kwa kununua  ndoo ya maji kwa sh 500 .

Katika maadhimisho ya miaka 41 ya CCM kiwilaya yaliyofanyika kijijini hapo,Babu amesema Mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Dunia ulilenga kutatua matatizo ya wakazi wa kijiji hicho,lakini baadhi ya watu kwa itikadi za kisiasa na wengine kujinufaisha kwa biashara ya kuuza maji walihujumu mradi huo huku serikali ya kijiji ikigoma kuupokea kwa madai kuwa haijakamilika.
 Baadhi ya wanachama wa CCM wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali.

 Wanafuatilia
 Makundi mbalimbali ya wanachama yalikuwepo
 Nasisitiza
 Mimi ni kada wa CCM lazima jimbo lirudi mwaka 2020,amesema
 Katibu wa CCM wilaya Solomoni amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wanachama wasaliti watadhibitiwa  ili kuhakikishawanakomboa jimbo na halmashauri.

Friday, February 2, 2018

ROBANDA WAANZA KUONJA MATUNDA YA MKURABITA

 Dc Serengeti Nurdin Babu akifungua semina ya Mkurabita kwa wakazi wa kijiji cha Robanda ili waweze kunufaika na raslimali ardhi kiuchumi
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa Dc


KINA MAMA NA MAENDELEO

 Mkazi wa kijiji cha Murito wilaya ya Tarime akinywesha mifugo Mto Mara,kazi ya kuchunga mifugo kwa asilimia kubwa  inafanywa na wanawake na watoto katika jamii ya eneo hilo,

 Anashuka taratibu na mifugo yake

WANANCHI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA WANAPOTAFUTA HAKI

 Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Ismael Ngaile amewataka wananchi kufuata taratibu za kisheria wanapokuwa wanatafuta haki ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua stahiki.

Amesema anashangazwa na wananchi kuwasilisha matatizo yao ya kisheria kwa njia ya mabango wanapofika viongozi badala ya kwenda kwenye mamlaka husika husika,hata hivyo amewataka watendaji wa mahakama kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.
 Dc Serengeti Nurdin Babu ameitaka mahakama kuendelea kutoa adhabu kali kwa watu wanaokamatwa kwa makosa ya ujangili,majambazi na wanaojichukulia sheria mikononi .

 Wanawahi


Thursday, February 1, 2018

WANANCHI 1300 WANUFAIKA NA MKURABITA ROBANDA NA MAKUNDUSI

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Nurdin Babu akizindua semina ya Mkurabita katika kijiji cha Robanda wilaya ya Serengeti ambapo wananchi 1300 watanufaika na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara ya wanyonge.
Meneja Urasimishaji Rasilimali ardhi (Mkurabita)Anthony Temu amesema lengo kuu ni kuwawezesha wanaomiliki raslimali ardhi na Biashara katika sekta isiyo kidhi matakwa ya Sheria (mfumo usio rasmi)kuingia sekta rasmi ili kushiriki kikamilifu katika mfumo wa kisasa,