Fahari ya Serengeti

Tuesday, December 12, 2017

ROBANDA WAITIKIA MKAKATI WA JENGA HOSPITALI KWA SH 1000

 Dc Serengeti Nurdin Babu akifafanua jinsi wananchi wa wilaya hiyo wanavyotakiwa kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo inatarajiwa kuanza kutoa huduma mwaka kesho januari,ili kukamilisha kazi hiyo kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa kujenga hospitali kwa kuchangia sh 1000,hata hivyo wakazi wa kijiji cha Robanda wameahidi kuvunja rekodi ya kuchangia ili kufanikisha kupata fedha zaidi ya sh 1 bil kwa ajili ya kazi hiyo.
 Mrobanda Japan mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Robanda amesema,wananchi wako tayari kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo kwa kuchangia ,mifugo,fedha na vitu vingine.
 Wananchi wanafuatilia mkutano huo
wanafuatilia



BWENI LA WAVULANA ROBANDA KUTUMIKA MWAKANI

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akishiriki kazi ya ujenzi wa bweni la wavulana sekondari ya Robanda ambalo linatakiwa kuanza kutumika mwaka kesho.
 Kazi zinaendelea kwa kasi
 Wakipata maelezo
 Dc akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Robanda na diwani wa kata hiyo Michael Kunani kushoto


Monday, December 11, 2017

UCHAFU WATISHIA AFYA ZA WAKAZI WA MTAA WA NHC



Taka ambazo zimerudikwa katikati ya Mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti zinatishia afya za watoto na wakazi wa mtaa huo baada ya wakala aliyepewa zabuni na Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mugumu kushindwa kuhamisha taka hizo kwa siku mbili,hata hivyo wananchi wanadai huo ni uzembe wa Mamlaka licha ya kununua Trekta lakini halitumiki badala yake wanatumia wazabuni 




 Hatari



DC ATAKA JAMII INAYOHESHIMU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.

 Dc Nurdin Babu amewataka wadau wote wanaojihusisha na vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia wilayani humo kushirikiana ili kuhakikisha wanakomesha vitendo hivyo ili kujenga wilaya yenye kuheshimu Haki za Binadamu na Utawala bora,na itasaidia kuharakisha maendeleo ya wilaya.
 Wanaandamana kupaza sauti za kupinga ukatili wa kijinsia

Ujumbe kwa njia ya Igizo kutoka Nuru Sanaa Group umetolewa

WAPAZA SAUTI KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

 Maandamano ya wadau mbalimbali wakati wa kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wilaya ya Serengeti wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
 Maandamano yakiongozwa na watoto wa kike walioko katika Kituo cha Nyumba Salama yakiendelea
 Wanawasilisha ujumbe kwa jamii ili ibadilike waachane na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji na wasomesehe watoto wa kike.
 Wanawasilisha
 Wadau mbalimbali wakifuatilia
 viongozi wakifuatilia
 Ocd Serengeti Mathew Mgema  akielezea matukio ya ukatili wilayani serengeti



Friday, December 8, 2017

WAWILI JELA MIAKA 25 KWA KUKUTWA NA MAYAI YA MBUNI,GARI KUPIGWA MNADA


 Marwa Matiko(32)na Julius Marwa(42) wakazi wa Tarime wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti kila mmoja kifungo cha miaka 25 na gari lao kutaifishwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na mayai 16 ya mbuni yenye thamani ya zaidi ya sh 42 mil kinyume cha sheria.



Sunday, December 3, 2017

ZIARA YA WAZIRI LUKUVI SERENGETI





UCHANGIAJI DAMU