Fahari ya Serengeti

Thursday, July 13, 2017

TPB BANK YAPIGA JEKI SHULE YA MSINGI KETEMBERE SERENGETI



Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akipokea na kuzindua Mradi wa byumba vya Madarasa viwili,ofisi mbili za walimu,madawati 30,meza mbili za walimu na choo cha matundu 8 kwa gharama ya zaidi ya sh 71 mil,iliyojengwa na TPB BANK kwa ajili ya shule ya Msingi Ketembere wilayani Serengeti,kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Robert Bashite.


Madarasa mawili na ofisi mbili za walimu shule ya Msingi Ketembere wilaya ya Serengeti yaliyojengwa na TPB BANK


 Burudani zilikonga nyoyo za watu.
 Mkuu wa Mkoa akisisitiza jambo kwa jamii kutokana na msaada huo ambao umesaidia kupunguza ukubwa wa tatizo la madarasa linaliokabili shule hiyo yenye watoto 712 ina vyumba nane vya madarasa hali ambayo inawafanya watoto kurundikana katika chumba kimoja na kuathiri mfumo mzima wa kujifunza na kujifunzia.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TPB  Bank Sabasaba Mashingi akielezea kilichowasukuma kujenga vyumba viwili vya madarasa,vyumba viwili vya Ofisi,madawati 30,meza mbili za walimu na choo cha matundu manane shule ya Msingi Ketembere wilayani Serengeti kwa gharama ya zaidi ya sh 71 mil,ni baada ya timu ya ufuatiliaji kujiridhisha na hali mbaya ya shule ilianza mwaka 1976 .
Amesema TPB BANK kupitia bajeti yao ya zaidi ya sh 150 mil wanayotenga kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo waliamua kusaidia,lengo ni kuwawezesha watoto kupata elimu katika mazingira mazuri.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPB BANK Sabasaba Mashingi ,katikati ni Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba.

 Picha ya viongozi mbalimbali mbele ya jengo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara dk Mlingwa.

 Burudani mbalimbali zilikuwepo,hiyo ni ngoma maarufu ya Gorona ya jamii ya Watatoga wilayani Serengeti.
 Baadhi ya maafisa wa TPB BANK wakifuatilia matukio mbalimbali.
 Kila aliyeguswa hakujizuia bali aliweza kutoa kitu kwa wacheza ngoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPB BANK Sabasaba Mashingi akicheza ngoma ya asili ya Watatoga ambayo ndiyo asili yake,

 Anapongezwa na mmoja wa wazee kwa jinsi alivyoweza kusakata ngoma yao ya asili,wahenga walisema msahau kwao ni mtumwa.
 Uzinduzi ukafanyika.



Tuesday, July 11, 2017

Grumeti agrees to repay over Sh1 billion it owes wildlife area

TUESDAY, JULY 11, 2017



  In Summary
·         On July 1 this year, officers and leaders of Ikona WMA had to close all roads leading to Farufaru Hotel and other areas used by Grumeti to pressurise the company so that it pays about Sh1.5 billion demanded for over three years unsuccessfully.

By Anthony Mayunga TheCitizenTz amayunga@tz.nationmedia.com
Serengeti. Grumeti Game Reserves (T) Ltd has agreed to repay Sh1.3 million it owes Ikona Wildlife Management Area (WMA) in Serengeti District, Mara Region.
On July 1 this year, officers and leaders of Ikona WMA had to close all roads leading to Farufaru Hotel and other areas used by Grumeti to pressurise the company so that it pays about Sh1.5 billion demanded for over three years unsuccessfully.
Grumeti public relations manager Ami Seki, speaking to reporters on the issue on July 6 this year, admitted they owed Ikoma WMA Sh1.3 billion and promised to repay it after signing an agreement, which was previously disputed by Ikona WMA.
Speaking to The Citizen during a telephone interview after a meeting with leaders of Grumeti, Ikona WMA and the district council, Serengeti District Commissioner Nurdin Babu said they had reached an agreement on debt settlement.
“What has been disputed by Ikona WMA requiring it to sign a new agreement we have left out and instead Ikona WMA has prepared a new agreement as the owner of the area and both parties are satisfied with it. So, Sh1.3 billion will be paid at any time from now,” said Mr Babu.
However, the district commissioner noted that his office in cooperation with experts from the district council would make a follow-up on Grumeti’s complaints about involving investors in the area without carrying out an environmental evaluation. Grumeti Game Reserves (T) Ltd public relations manager Ami Seki admitted having reached the agreement and that lawyers of both parties would go through what had been decided about the agreement, which Ikona WMA Council of Authorised Association (AA) would accent to before signing it and pay the money.
Grumeti Game Reserves (T) Ltd is among the investors hiring Ikona WMA and are supposed to pay rent charges every year, including charges on photos and hunting.
The 50 per cent payment paid by the investors, who hired the area is spent on conservation purposes, while 50 per cent is divided among member villages of Natta Mbiso, Robanda, Nyichoka, Makundusi and Nyigoti for development projects.



Saturday, July 8, 2017

MRADI WA CHUJIO LA MAJI MUGUMU PASUA KICHWA

 Mradi wa Chujio la Maji Mugumu wilaya ya Serengeti ambao Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa alimwahidi Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa atakabidhiwa juni 30 mwaka huu,sasa ni pasua kichwa kutokana na msimamizi wa Mradi Muwasa kutokuonekana eneo la shughuli,huku mkandarasi akidai kuwa amekwamishwa na Muwasa kwa kutokumpa baadhi ya vipimo.
 Chujio hilo lililoanza kujengwa machi 2015 kwa muda wa miezi sita ,sasa ni zaidi ya miaka miwili na kazi haijakamilika,
 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiongea na msimamizi wa Ujenzi upande wa Mkandarasi Kampuni ya Pet Cooperatives  Ltd  Clodatus Felix ,ambaye anadai kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mchoro na kutokupewa kipimo cha maji  kwa wakati na Msimamizi wa Maradi,Muwasa.
 Mbunge Marwa Ryoba akipata taarifa kwa msimamizi wa ujenzi Upande wa Mkandarasi kuhusu tenki la maji ambalo halijaanza kujengwa licha ya muda walioomba kwisha juni 30 mwaka huu.

 Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akipata maelezo ya mradi huo machi 13 mwaka huu alipozuru eneo la mradi na kuahidiwa kukabidhiwa mradi juni 30 mwaka huu,hata hivyo mradi huo haujakabidhiwa na hakuna anayeeleza lini watakamilisha na kukabidhi.
Mhandisi Mshauri toka Muwasa Kajigili akimwelezea  Mkuu wa Mkoa jinsi shughuli zinavyokwenda wakati na kuwa juni 30 mwaka huu watamkabidhi,hata hivyo kabla ya siku za kukabidhi mhandisi huyo alikwenda likizo na kazi haijakamilika.

MRADI WA RAIN PROJECT UNAOTEKELEZWA NA AMREF AFRICA NA COCACOLA AFRIKA KUTATUA TATIZO LA MAJI MOSONGO SERENGETI

 Wakazi wa kijiji cha Kenokwe kata ya Mosongo wilayani Serengeti wakielekea katika kisima  cha maji kilichoko Mosongo umbali wa Kilometa nane,wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo,Hata hivyo kupitia Mradi wa Rain unaotekelezwa na AAmref Africa na Cocacola Afrika wanatarakiwa kuchimbiwa kisima kirefu,maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo ni Busawa,Machochwe na Kenyamonta.
 Meneja wa Rain Project Mhandisi Onesmo Stephano kulia akisaidia wakazi wa kijiji cha Kenokwe kumnyanyua Punda baada ya kutwisha mzigo wa Maji.

 Mradi huo utashughulika na suala la vyoo kwa shule za msingi.




 Kisima hicho hutegemewa na wakazi wa kata hiyo pamoja na mifugo.


Thursday, July 6, 2017

WAKAZI WA MACHOCHWE SERENGETI WATAKA SHERIA YA WANYAMAPORI IFANYIWE MAREKEBISHO

 Diwani wa Kata ya Machochwe wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Chacha Michael akipitia hoja zilizowasilishwa na wananchi wa kata yake wakati wa Mkutano wa hadhara,moja ya mambo yaliyojadiliwa kwa nguvu na watu wengi ni kukithiri kwa tatizo la tembo kutoka ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wameomba .Kanuni za ulipaji wa fidia na kifuta machozi kwa wananchi wanaopata madhara yanayotokana na wanyama kama tembo ziangaliwe upya kwa kuwa zinachangia ongezeko la umaskini kwa jamii.

Kupitia sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya Mwaka 2009 na kanuni za ulipaji fidia za mwaka 2011 ,ekari moja ya mazao yaliyoharibiwa na tembo hulipwa kati ya sh 25,000 hadi 100,000 kutegemea na umbali.

Daniel Makuri Mkazi wa Kijiji cha Machochwe wilayani Serengeti katika mkutano huo ameshauri serikali na wabunge ,badala ya kurekebisha sheria za Madini ,waangalie pia udhaifu wa sheria hiyo ya  wanyamapori kwa kuwa inachangia ongezeko la maskini hasa waishio pembezoni mwa maeneo yaliyohifadhiwa.

“Ng’ombe akikanyaga hifadhini mfugaji hulazimika kulipa sh 50,000 kwa ng’ombe mmoja,lakini tembo akila ekari moja moja ya mazao mtu analipwa sh 25,000,tena inachukua zaidi ya miaka mitatu,wakati  mifugo unalipa papo hapo,sheria hii inatakiwa kufanyiwa mabadiliko kama tunataka kupunguza umaskini,”alisema.

Suzana Chacha mkazi wa kijiji cha Manyata kwa hasira alisema,”tembo akiuawa mtu anatakiwa kutoa kulipa sh 25 mil,lakini akiua mtu serikali inamlipa mtu sh 1 milioni,harafu viongozi wanasisitiza tupende uhifadhi,katika mazingira ya kutathimini wanyama kuliko watu,kuna uhifadhi hapo,?”alisema
 Baadhi ya wazee wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kata ya Machochwe ulioongozwa na Diwani wa kata hiyo.
 Wanafuatilia mjadala



Kila kona katika kata hiyo na kata za jilani zilizoko kando ya maeneo yaliyohifadhiwa wanalia na tatizo la tembo.

GRUMETI GAME RESERVES WADAI WAKO TAYARI KULIPA IKONA WMA BAADA YA MARIDHIANO

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Grumeti Game Reserves Ami Seki amekiri kampuni yao inadaiwa na Ikona Wma zaidi ya sh 1.2 bilioni na kuwa wapo tayari kulipa baada ya kukamilisha maridhiano na kusainiana makubaliano hayo.

Ufafanuzi huo ameutoa baada ya siku tano toka askari na viongozi wa Ikona Wma kuziba njia za kwenda kwenye hoteli ya Farufaru na maeneo mengine yaliyoko ndani ya eneo la Ikona Wma ambayo yanatumiwa na Kampuni hiyo kwa mkataba wa Malipo,hata hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu kampuni hiyo haijalipa deni hilo hali ambayo inadaiwa kuathiri utendaji wa jumuiya hiyo.

Seki amesema kuwa katika mpango Mkakati wa Ikona imeanishwa taratibu za uwekezaji ,hata hivyo wanadai zimekiukwa ikiwa ni pamoja na kuweka kambi nyingi nje ya mpango na kuathiri wawekezaji wengine ikiwemo kampuni hiyo.

"Tumeishalalamika sana kwao,halmashauri na ofisi ya Dc bila mafanikio,tukaamua kusitisha malipo yao ili tukae maana wanataka haki bila kutimiza wajibu ,tuko tayari kuwalipa mara baada ya kusainiana makubaliano ya utendaji kazi,"anasema.

Akizungumzia masharti hayo Katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda anasema kuwa Grumeti wanatakiwa kutimiza matakwa ya mkataba uliowafanya wakapewa eneo,si kuleta masharti ambayo hayana msingi ,kwa kuwa deni hilo ni haki ya Ikona kulipwa kwa kuwa anafanya biashara kwenye eneo la jamii.

"Haiwezekani mpangaji ndiye anaweka masharti dhidi ya mwenye nyumba na kumtaka ayasaini,maana Grumeti hawezi kuandaa masharti ya kufanya kazi katika eneo ambalo ameomba na kupewa kwa taratibu za jumuiya na taifa,kama kuna mambo ambayo anaona yamekiukwa afuate mamlaka zinazohusika,si kutalia fedha wakati akiendelea kufanya biashara,"anasema.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amesema ameishaita pande zote ofisini mwake ili waweze kumaliza mgogoro huo ambao kimsingi unahitaji maridhiano,"hatua ya kufunga njia wageni wasiiingie inaathiri sekta ya utalii,ni kweli Grumeti anadaiwa anatakiwa kulipa ,kuna mambo tukikutana tutayamaliza,"amesema.

Monday, July 3, 2017

UHIFADHI SERENGETI

 Twiga wakiwa wamepumzika katika maeneo ya Ikona Wma ,wanyama hawa ni miongoni mwa vivutio vikubwa kwa watalii.

 Nyumbu wanaanza safari ya kuelekea Masai Mara


IKONA WMA WAWAFUNGIA WAGENI WA GRUMETI NJIA WAKISHINIKIZA KULIPWA DENI LA ZAIDI YA SH 1.5 BIL

 Askari wa I kona Wma na viongozi wao wakiwa wameziba njia za kupita watalii wa kampuni ya Grumeti Reserves baada ya kutolipwa zaidi ya sh 1.5 bil kwa kipindi cha miaka 4 ,wakati akifanya biashara ya utalii wa picha,pango na uwindaji kwenye eneo la hifadhi hiyo.
hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu aliingilia kati kunusuru hali hiyo na kuwataka wafike ofisini mwake,na kuitaka kampuni hiyo kulipa deni wanalodaiwa ili jumuiya iweze kuendesha shughuli zake za uhifadhi .
 Baadhi ya askari wa hifadhi hiyo wakiwa kwenye maeneo maalum ya njia ili kuzuia magari ya wageni yasiweze kupita.
 Hakuna gari kupita mmoja wa askari anadai.

 Udhibiti unaendelea.

Mhifadhi mkuu wa Ikona akifafanua  sababu za kuziba njia hiyo.