Fahari ya Serengeti

Monday, October 17, 2016

MADIWANI SERENGETI WAPIGWA BUMBUWAZI KUHUSIANA NA ATHARI ZA UKEKETAJI KWA WATOTO WA KIKE

 Meneja Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti Godfrey Matumu(amref)akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo jinsi mradi huo unavyotekelezwa katika semina ya Athari ya Ukeketaji Ukumbi wa Anita.
 Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti William Mtwazi(LHRC)akifafanua sababu za madiwani kushiriki kwenye mradi huo ili kumwokoa mtoto wa kike wa Serengeti.
 Baadhi ya Madiwani wakiwa wanafuatilia mwezeshaji akitoa mada

 Madiwani wakiwa wanafanya jaribio la kupima uelewa juu ya masuala ya athari za ukeketaji na ukatili wa kijinsia wilayani humo.



 Madiwani wakiwa kwenye kazi za makundi
 Mijadala kimakundi inaendelea
 Wanajadiliana

 Mjadala mjadala
 Kila kundi likiendelea na mjadala



Thursday, October 13, 2016

FAINALI YA NYERERE CUP KUWAKUTANISHA MAGETA FC NA SMARTBOYS FC UWANJA WA SOKOINE MUGUMU SERENGETI.


F
Fainali ya Nyerere Cup inayoshirikisha vijana wa chini ya Umri wa Miaka 17 kuzikutanisha timu hasimu mjini Mugumu Mageta Fc na Smartboys maarufu kama Chamoto Uwanja wa Sokoine Oktoba 14 majira ya saa kumi,Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya Nurdin Babu,
mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ni kati ya Polisi Fc na Bomani ,pia kutakuwa na Mchezo wa mpira wa Miguu kwa wanawake ,na burudani nyingine.
Mashindano hayo yameandaliwa na Serengeti Media Centre ,Mageta na Rhobi Magoiga lengo likiwa ni kuibua vipaji na kuwawezesha timu ya wataalam kuchagua timu ya wilaya.

UV CCM SERENGETI WACHANGIA CHUPA 33 ZA DAMU

 Katibu wa CCM wilaya ya Serengeti akipima Presha kabla ya zoezi la uchangiaji damu katika wiki ya vijana ambapo jumla ya chupa 33 zilipatikana,anayefuata ni mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu.
 Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Serengeti Charles Makena akitoa maelezo ya zoezi la uchangiaji wa damu.
 Watu wanaendelea kuchangia damu.















Tuesday, October 11, 2016

SIKU YA HAKI YA MTOTO DUNAINI SERENGETI WANAFUNZI WA IKORONGO SECONDARY WATOA YA MOYONI

Wanafunzi wa sekondari ya Ikorongo wakiwa kwenye kongamano la kujadili matatizo ya ukeketaji yanavyochangia kuwadumaza kielimu ,na pia ndoa za utotoni


Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti wawajengea uwezo watoto wa kike ili kupinga vitendo vya ukeketaji


Afisa Mradi wa Tokomeza ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na Amref na LHRC kwa ufadhili wa UN Women William Mtwazi akifafanua madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike



Sunday, October 9, 2016

MATUKIO YA SEND OF YA ZAWADI GIRAFFE GARDEN MUGUMU

 Zawadi B.Malya akiingia uwanjani kwa bashasha baada ya kukata utepe akisindikizwa na mdogo wake kama inavyoonekana picha za juu

 Zawadi akiwa katika pozi la kisasa kabisa katikati ya ukumbi huku akishuhudiwa na kushangiliwa na wageni waalikwa na kuhanikizwa na maneno mazito toka kwa Mc Gasaya.
 Anapokewa na wageni waalikwa na kusindikizwa kwa vigelegele na shangwe.

 Wageni waalikwa wakifuatilia matukio yanayoendelea kwa kuongozwa na Mc Gasaya.
 Ndugu wa Mme mtarajiwa Alais Olengurumwa wakiingia ukumbi wa Giraffe Garden mjini Mugumu kwa mbwembwe za Kimasai,hakika ulikuwa ni usiku wa raha,burudani na shamrashamra na ni ishara kuwa ndoa yao itakayofungwa oktoba 15 Arusha mwaka huu itafana.
 Mc mwenye weledi mkubwa wa kusherehesha Mwalimu Gasaya akitoa maelezo na umuhimu wa shughuli .
 Zawadi akiwa Kirawira Hotel kabla ya kwenda ukumbini.
 Kila mmoja anafuatilia matukio yaliyopangiliwa vilivyo,huku Timu ya Serengeti Media Centre akichukua matukio yote ya video na picha mnato kwa umakini mkubwa.
 Mallya na Helen mkewe wakiwa pamoja na wageni waalikwa wakifuatia manjonjo yanayoonyeshwa ukumbuni Sendoff ya binti yao Zawadi.
 Mmabo yanaenda yakiongezeka kila aina ya burudani na manjonjo ilikuwepo
 Wazazi nao wanaonyesha enzi zao kuwa walikuwa wamo na kuwa burudani haijawapita kushoto.
 Wanaingia Kimasai
 Asili haikusahaulika
 Udhibiti mlangoni ulikuwa wa uhakika hakuna mzamiaji

 Wazee wa Kisingeli walikuwepo




 Mc akikoleza muziki na kumfanya Zawadi kujiachia kwa raha zake na kuufanya ukumbi mzima kuzizima kwa furaha,shangwe na vigelegele na wengine kuamua kujiachia kwa burudani.
 Mwenyekiti wa Kamati Vicky Magige akiwakaribisha wageni waalikwa ukumbini .
 Kwa raha zake
 Kila Upande ulichemka na kumshangilia kadri alivyokuwa akiingia ukumbini kwa burudani safiiii.
 Keki ilikatwa


 Analishwa keki na mdogo wake.

 Anawakabidhi wazazi wake keki
 Anakabidhi keki kwa upande wa wazazi wa mme wake mtarajiwa
Taratibu anaondoka huku kila mmoja akishangilia,Matukio yote ni kwa hisani ya Serengeti Media Centre.