Zawadi akiwa katika pozi la kisasa kabisa katikati ya ukumbi huku akishuhudiwa na kushangiliwa na wageni waalikwa na kuhanikizwa na maneno mazito toka kwa Mc Gasaya.
Anapokewa na wageni waalikwa na kusindikizwa kwa vigelegele na shangwe.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio yanayoendelea kwa kuongozwa na Mc Gasaya.
Ndugu wa Mme mtarajiwa Alais Olengurumwa wakiingia ukumbi wa Giraffe Garden mjini Mugumu kwa mbwembwe za Kimasai,hakika ulikuwa ni usiku wa raha,burudani na shamrashamra na ni ishara kuwa ndoa yao itakayofungwa oktoba 15 Arusha mwaka huu itafana.
Mc mwenye weledi mkubwa wa kusherehesha Mwalimu Gasaya akitoa maelezo na umuhimu wa shughuli .
Zawadi akiwa Kirawira Hotel kabla ya kwenda ukumbini.
Kila mmoja anafuatilia matukio yaliyopangiliwa vilivyo,huku Timu ya Serengeti Media Centre akichukua matukio yote ya video na picha mnato kwa umakini mkubwa.
Mallya na Helen mkewe wakiwa pamoja na wageni waalikwa wakifuatia manjonjo yanayoonyeshwa ukumbuni Sendoff ya binti yao Zawadi.
Mmabo yanaenda yakiongezeka kila aina ya burudani na manjonjo ilikuwepo
Wazazi nao wanaonyesha enzi zao kuwa walikuwa wamo na kuwa burudani haijawapita kushoto.
Wanaingia Kimasai
Asili haikusahaulika
Udhibiti mlangoni ulikuwa wa uhakika hakuna mzamiaji
Wazee wa Kisingeli walikuwepo
Mc akikoleza muziki na kumfanya Zawadi kujiachia kwa raha zake na kuufanya ukumbi mzima kuzizima kwa furaha,shangwe na vigelegele na wengine kuamua kujiachia kwa burudani.
Mwenyekiti wa Kamati Vicky Magige akiwakaribisha wageni waalikwa ukumbini .
Kwa raha zake
Kila Upande ulichemka na kumshangilia kadri alivyokuwa akiingia ukumbini kwa burudani safiiii.
Keki ilikatwa
Analishwa keki na mdogo wake.
Anawakabidhi wazazi wake keki
Anakabidhi keki kwa upande wa wazazi wa mme wake mtarajiwa
Taratibu anaondoka huku kila mmoja akishangilia,Matukio yote ni kwa hisani ya Serengeti Media Centre.
0 comments:
Post a Comment