Fahari ya Serengeti

Monday, October 31, 2016

GRUMETI YAMWAGA MISAADA SERENGETI NA BUNDA

 Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe(kulia)akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 na Nyumbaya Mwalimu shule ya Msingi  Makundusi vyote vikiwa na  Thamani ya sh.198,160,970 kwa ajili ya wilaya za Serengeti na Bunda afla  iliyofanyika  katika shule ya Msingi Makundusi wilayani Serengeti.
Mkuu wa mkoa wa Mara Charles Mlingwa(wa tano kutoka kushoto)akiwa na Baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya kukabidhiwa Nyumba ya Mwalimu katika shule ya msingi Makundusi.
Haya ni madawati yalitolewa na Singita Grumeti yakiwa tayari yametengwa kwa ajili ya kupelekwa katika eneo husika kwa matumizi Rasmi ya wanafunzi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara akiwa pamoja na waburudishaji wa Ngoma za asili almaarufu kama (Ritungu) mara baada ya kukabidhiwa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Makundusi.       
 Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe(kushoto)akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Mara Charles Mlingwa moja ya thamani zilizopo ndani ya nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Makundusi.
 Hii ni moja ya nyumba ya mwalimu iliyopo katika Shule ya Msingi Makundusi wilayani Serengeti ikiwa katika hatua za mwisho za matengenezokabla ya kukabidhiwa Rasmi kwa Walimu.
Wakuu wa wilaya na badhi ya viongozi wa Serikali wakiwa pamoja na Mkuu wa mkoa mara baada ya kutembelea eneo maalum lililokuwa limetengwa madawati 500 kwa ajili ya kukabidhiwa Rasmi kwa mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe.Nurdin Babu wa kwanza(Kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe.Lydia Bupilipili wa pili kutoka(Kushoto).
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Makundusi wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa madawati shuleni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Charles Mlingwa akisalimiana na Wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Makundusi wilayani Serengeti mkoani Mara.
 Baadhi ya Walimu wa Shule ya msingi Makundusi wakisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Charles Mlingwa alipowasili katika viwanja vya shule hiyo.
Kikundi cha burudani cha nyimbo za asili maarufu kama(Ritungu)wakiendelea kuburudisha wageni katika hafla fupi ya kukabidhi madawati pamoja na nyumba ya mwalimu shule ya Msingi Makundusi.
Meneja wa mradi mfuko wa  Maendeleo ya Jamii Singita Grumeti(Richard Ndaskoi)akitoa salam kwa mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara pamoja na viongozi wote walioudhulia hafla hoyo ya kukabidhi madawati pamoja na nyumba ya mwalimu.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe,Lydia Bupilipili wa kwanza(Kushoto)na Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mhe.Nurdin Babu wa Pili(Kushoto)wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kabla ya kuwakabidhi Rasmi madawati yaliyotolewa na Singita Grumeti.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr.Charles Mlingwa akiwashukuru viongozi wa Singita Grumeti kwa msaada wa madawati walioutoa katika wilaya ya Bunda na wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.
 Mkuu wa Mara Dr.Charles Mlingwa akitoa Hotuba yake kwa wananchi na viongozi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati na nyumba ya mwalimu viwanja vya shule ya msinginMakundusi.
 Baadhi ya Wanafunzi wanaofadhiliwa na Singita Grumeti wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi Wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe(Kushoto)akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara mara baada ya kumkabidhi madawati 500 viwanja vya shule ya Msingi Makundusi.

 Mkuu wa Mkoa wa Mara Charles Mlingwa akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali tayari kwenda kukagua Nyumba ya Mwalimu iliyotolewa na Singita Grumeti katika shule ya Msingi Makundusi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Charles Mlingwa akikata Utepe kufungua nyumba ya Mwalimu yenye thamni ya zaidi ya sh 86 mil.iliyojengwa na Kampuni ya Singita Grumeti Fund.
Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara wakiwa ndani ya nyumba ya mwalimu iliyotolewa na Singita Grumeti.

0 comments:

Post a Comment