Fahari ya Serengeti

Sunday, October 9, 2016

MIKAKATI YA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YAANZA KUPANGWA

 Wadau wa maendeleo kutoka sekta mbalimbali ndani na nje ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa eneo la hospitali ya wilaya inayojengwa kwa ajili ya kuangalia hali ilivyo ili kuwawezesha kuweka mikakati ya namna ya kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi ,miongoni kwa mikakati hiyo ni kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wananchi wenyewe,wakazi wa wilaya hiyo waishio nje ya wilaya na Mkoa na serikali kuu.
 Mganga mkuu wa wilaya Salum Manyatta akitoa ufafanuzi wa majengo yaliyokamilika na ambayo bado kwa wadau wa maendeleo ambao kabla ya kikao chao waliamua kwenda eneo la mradi kuangalia hali ilivyo ambapo zaidi ya sh 3 bilioni zinahitajika ili kukamilisha kazi hiyo.
 Ufafanuzi unaendelea
 Viongozoi wa serikali kwa kuongozwa na dc Nurdin Babu na wadau wa maendeleo wakifuatilia maelezo ya mradi huo.

 Dc akitoa msimamo wa wilaya kwa wadau ambao hawachangii maendeleo ya wilaya hiyo hawatakiwi kwa kuwa wanaigharimu serikali kuwahudumia huku wakivuna pesa nyingi na faida haitumiki wilayani humo.
 Ded Juma Hamsini amesema jina la serengeti linatumiwa na wawekezaji kuuza biashara zao lakini hawachangii kuifanya wilaya hiyo ambayo inatoa huduma kwa wageni wa kitalii ili iweze kuendelea kwa kuboresha miundombinu ya barabara,maji ,elimu ,afya na uchumi wa jamii.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kwanza kupanga mikakati katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya

0 comments:

Post a Comment