Fahari ya Serengeti

Sunday, October 9, 2016

MATUKIO YA SEND OF YA ZAWADI GIRAFFE GARDEN MUGUMU

 Zawadi B.Malya akiingia uwanjani kwa bashasha baada ya kukata utepe akisindikizwa na mdogo wake kama inavyoonekana picha za juu

 Zawadi akiwa katika pozi la kisasa kabisa katikati ya ukumbi huku akishuhudiwa na kushangiliwa na wageni waalikwa na kuhanikizwa na maneno mazito toka kwa Mc Gasaya.
 Anapokewa na wageni waalikwa na kusindikizwa kwa vigelegele na shangwe.

 Wageni waalikwa wakifuatilia matukio yanayoendelea kwa kuongozwa na Mc Gasaya.
 Ndugu wa Mme mtarajiwa Alais Olengurumwa wakiingia ukumbi wa Giraffe Garden mjini Mugumu kwa mbwembwe za Kimasai,hakika ulikuwa ni usiku wa raha,burudani na shamrashamra na ni ishara kuwa ndoa yao itakayofungwa oktoba 15 Arusha mwaka huu itafana.
 Mc mwenye weledi mkubwa wa kusherehesha Mwalimu Gasaya akitoa maelezo na umuhimu wa shughuli .
 Zawadi akiwa Kirawira Hotel kabla ya kwenda ukumbini.
 Kila mmoja anafuatilia matukio yaliyopangiliwa vilivyo,huku Timu ya Serengeti Media Centre akichukua matukio yote ya video na picha mnato kwa umakini mkubwa.
 Mallya na Helen mkewe wakiwa pamoja na wageni waalikwa wakifuatia manjonjo yanayoonyeshwa ukumbuni Sendoff ya binti yao Zawadi.
 Mmabo yanaenda yakiongezeka kila aina ya burudani na manjonjo ilikuwepo
 Wazazi nao wanaonyesha enzi zao kuwa walikuwa wamo na kuwa burudani haijawapita kushoto.
 Wanaingia Kimasai
 Asili haikusahaulika
 Udhibiti mlangoni ulikuwa wa uhakika hakuna mzamiaji

 Wazee wa Kisingeli walikuwepo




 Mc akikoleza muziki na kumfanya Zawadi kujiachia kwa raha zake na kuufanya ukumbi mzima kuzizima kwa furaha,shangwe na vigelegele na wengine kuamua kujiachia kwa burudani.
 Mwenyekiti wa Kamati Vicky Magige akiwakaribisha wageni waalikwa ukumbini .
 Kwa raha zake
 Kila Upande ulichemka na kumshangilia kadri alivyokuwa akiingia ukumbini kwa burudani safiiii.
 Keki ilikatwa


 Analishwa keki na mdogo wake.

 Anawakabidhi wazazi wake keki
 Anakabidhi keki kwa upande wa wazazi wa mme wake mtarajiwa
Taratibu anaondoka huku kila mmoja akishangilia,Matukio yote ni kwa hisani ya Serengeti Media Centre.

MIKAKATI YA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YAANZA KUPANGWA

 Wadau wa maendeleo kutoka sekta mbalimbali ndani na nje ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa eneo la hospitali ya wilaya inayojengwa kwa ajili ya kuangalia hali ilivyo ili kuwawezesha kuweka mikakati ya namna ya kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi ,miongoni kwa mikakati hiyo ni kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wananchi wenyewe,wakazi wa wilaya hiyo waishio nje ya wilaya na Mkoa na serikali kuu.
 Mganga mkuu wa wilaya Salum Manyatta akitoa ufafanuzi wa majengo yaliyokamilika na ambayo bado kwa wadau wa maendeleo ambao kabla ya kikao chao waliamua kwenda eneo la mradi kuangalia hali ilivyo ambapo zaidi ya sh 3 bilioni zinahitajika ili kukamilisha kazi hiyo.
 Ufafanuzi unaendelea
 Viongozoi wa serikali kwa kuongozwa na dc Nurdin Babu na wadau wa maendeleo wakifuatilia maelezo ya mradi huo.

 Dc akitoa msimamo wa wilaya kwa wadau ambao hawachangii maendeleo ya wilaya hiyo hawatakiwi kwa kuwa wanaigharimu serikali kuwahudumia huku wakivuna pesa nyingi na faida haitumiki wilayani humo.
 Ded Juma Hamsini amesema jina la serengeti linatumiwa na wawekezaji kuuza biashara zao lakini hawachangii kuifanya wilaya hiyo ambayo inatoa huduma kwa wageni wa kitalii ili iweze kuendelea kwa kuboresha miundombinu ya barabara,maji ,elimu ,afya na uchumi wa jamii.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kwanza kupanga mikakati katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya

Thursday, October 6, 2016

WAPATA MADAWATI KUPUNGUZA UKUBWA WA TATIZO

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mugumu A iliyoko mjini Mugumu wilayani Serengeti wakiwa Chuo cha Chipuka kwa ajili ya kuchukua madawati ambayo yalinunuliwa na halmashauri ,shule hiyo imepata madawati 50 ,inakabiliwa na upungufu wa madawati 281.


Wanafunzi wanapelekea madawati shuleni


ZIARA ZA KUJENGA MAHUSIANO NA WAWEKEZAJI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Viongozi wakitoka Kambi ya Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,ziara hiyo iliyoshirikisha viongozi ngazi ya wilaya na kutoka kata ya Machochwe na idara ya ujilani mwema hifadhi ya Senapa.
Viongozi wakiwa katika majadiliano.
Zablon Mtweve wa Ujilani hifadhi ya Taifa ya Serengeti akitoa taarifa kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti wakati wa ziara ya kutembelea kambi za kitalii zilizomo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilizoko Kaskazini.




Issa Kassimu meneja wa Kambi ya Kitalii ya Nomard Lamai akitoa maelezo kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti

Monday, October 3, 2016

MWENYEKITI WA HALMASHAURI AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA KAMBI ZA KITALII NDANI YA HIFADHI YA SENAPA

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini akisisitiza jambo katika kambi ya Kilima hoteli inayojengwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa ziara yake aliyoambatana na wataalam,diwani na viongozi wa vijiji vinavyopakana na kambi hizo ,lengo likiwa ni kukutana na viongozi na wafanyakazi wa kambi hizo ili kujadiliana namna zinavyotakiwa kuchangia maendeleo ya wilaya,fursa za ajira kwa wazawa,mikataba ya wafanyakazi,na ununuaji wa bidhaa Mugumu badala ya Arusha.




 Majadiliano katika kambi ya Chaka yakiendelea
 Mkurugenzi wa kambi ya Alex Walkers Safaris Gerald Ambrose akimkaribisha Mwenyekiti na timu yake kwenye kambi hiyo iliyoko eneo la Kogatende

wakiwa kwenye mjadala