Fahari ya Serengeti

Wednesday, July 19, 2017

RC MARA AKUTANA NA MADUDU MRADI WA CHUJIO LA MAJI MUGUMU

 Rc Mara Dk Charles Mlingwa akipanda juu ya chuji la maji Mugumu wilayani Serengeti kwa ajili ya kukagua,hata hivyo alikutana na madudu kwa kazi iliyokuwa imefanyika ya kusuka nondo ili kumwaga zege kuanza kufumuliwa kutokana na Mkandarasi Kampuni ya Pet Cooperation Ltd kujenga bila kuzingatia hitaji la mchoro.
Aidha mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Musoma(Muwasa)ulianza kujengwa mwaka 2015 machi na ulitarajiwa kukamilika septemba 2015,hata hivyo haujakamilika na Mkandarasi aliomba muda hadi juni 30 mwaka huu angekuwa amemaliza na kukabidhi.

Katika hali ya kushangaza Muwasa na Mhandisi wa Kampuni hiyo walimkacha Mkuu wa Mkoa baada ya kujua angetembelea mradi huo,hali iliyomfanya fundi wa Kampuni hiyo kujigeuza mhandisi na baada ya kubanwa akakiri kuwa yeye ni fundi na si Mhandisi.

Mkuu wa Mkoa ameagiza kukutana na Muwasa na Mhandisi wa Kampuni hiyo ana kwa ana ili watoe maelezo kwa nini mradi huo haujakamilika na sababu za kumkacha na kuacha shughuli zinaendeshwa na watu wasiokuwa na sifa stahiki.
 Fundi wa Kampuni ya Pet Clodatus Felix akijibu maswali baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni Mhandisi ,hata hivyo alikiri kuwa yeye elimu yake ni kidato cha nne tu.

 Rc Dk Mlingwa akimcharukia fundi huyo aliyejifanya Mhandisi na kuwa kazi yao hairidhishi na wanawafanya wakazi wa Mji wa Mugumu kunywa maji machafu wakati serikali imeishalipa zaidi ya asilimia 65 ya fedha ya mradi ambayo ni zaidi ya sh 1.4 bil.
 Maswali yalimwelemea fundi
 Fundi akitoa maelezo ya changamoto wanazokutana nazo ikiwemo ni wasimamizi wa Mradi Muwasa kutochukua hatua kwa wakati hali ambayo inachangia kuwachelewesha baadhi ya maeneo.




 Hata hivyo baada ya kutorodhishwa na maelezo ya fundi akaamua kutoka huku akiacha maagizo wamtafute kabla ya kutoka serengeti
 Anashuka
 Dc Serengeti Nurdin Babu naye akishuka na kufuatiwa na Ded Serengeti Juma Hamsini
Wahenga walisema kupanda mchongoma si kazi ,kazi ni kushuka wanateremka kwa tahadhari

LUMUYE LEOPARD CO.LTD KUJENGA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAFUTA YA ALIZETI

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lumuye Leopard Co.Ltd Juma Mugiye Chacha kulia akiwa anateta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa muda mfupi baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa kiwanda hicho katika eneo la Tambisa mtaa wa MCU Mugumu wilayani Serengeti.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara DkCharles Mlingwa akiangalia shamba la alizeti la Kampuni ya Lumuye Leopard.Co.Ltd
 Kaimu meneja wa Tanesco wilaya ya Serengeti Peter Mtete akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ,lini Tanesco watafikisha umeme katika eneo hilo linalotarajiwa kujengwa kiwanda,hata hivyo amesema kuwa zinatakiwa zaidi ya sh 20 mil,na shirika halina bajeti hiyo hivyo mwekezaji agharamie gharama hizo.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akielezea mikakati ya wilaya kutekeleza sera ya uwekezaji.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Mugumu Bhoke Ruhinda akisoma taarifa ya kampuni ya Lumuye ambayo inatarajia kujenga kiwanda ambacho kitatoa ajira 400 za kudumu na 300 vibarua ,na uzalishaji wake utakuwa ni lita 30750 za mafuta kwa siku
 Rc akiongea na wananchi wa eneo la Tambisa kuchangamkia fursa hiyo ya uwekezaji
 Anasisitiza jambo
 Mkurugenzi wa Lumuye kushoto akifuatilia maelezo ya Mkuu wa Mkoa wakati anaongea na wananchi kuhusiana na uwekezaji anaotarajia kuuweka.
 Wanateta jambo


RC MARA AAGIZA UONGOZI WA WILAYA YA SERENGETI KUHAKIKISHA UJENZI WA HOSPITALI UNAKAMILIKA

 Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akitoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya ya Serengeti juu ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya alipofanya ukaguzi wa kuangalia maendeleo ya kazi,ameagiza kuwa wanatakiwa kuweka mpango maalum wa kazi ,kazi gani inafanyika na kwa wakati gani ili kuwawezesha kupima na kufanya tathimini ya kazi.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akitoa maelezo ya namna kazi zilivyofanyika na wanavyoendelea kuhakikisha kazi ya upigaji lipu inakamilika.

 Mafundi wakiwa kazini

Saturday, July 15, 2017

KAMPUNI YA GRUMETI RESERVES LTD YAILIPA IKONA WMA ZAIDI YA SH 1.3 BIL

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd Ami Seki kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa IIkona Wma Elias Nchama kushoto Hundi ya zaidi ya sh 1.3 bil ikiwa ni malipo ya deni za miaka mitatu walilokuwa wanadaiwa na Jumuiya hiyo ya Uhifadhi,ikiwa ni gharama za pango,ushuru wa Vitanda,Upigaji Picha na uwindaji wa kitalii.
Katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda kulia akisaini makubaliano ya hiyari kati ya Jumuiya hiyo na Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd ambayo yanawapa wajibu pande zote za kuheshimu taratibu za uwekezaji na uhifadhi,kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elias Nchama.
Mwenyekiti wa Ikona Wma Elias Nchama akisaini Makubaliano ya hiari ,kushoto ni Katibu wa Jumuiya hiyo Yusuph Manyanda.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Grumeti Reserves Ltd Ami Seki akisaini makubaliano ya hiari kati yao na Ikona ,kulia kwake ni Msaidizi wake David Mwakipesele.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Simioni Warioba kushoto na Afisa wanyamapori wilaya hiyo John Lendoyan wakisaini makubaliano ya hiari kati ya Grumeti Reserves na Ikona Wma.
Wakili Maganiko Msabi ambaye ni Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti akitoa maelekezo kabla ya kusaini makubaliano ya hiayo ya kampuni ya Grumeti Reserves na Ikona Wma.
Katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda akitoa ufafanuzi wa pesa zinazotakiwa kulipwa na Grumeti Reserves kabla ya kusainiana makubaliano ya hiari.
Wanajadiliana
Malipo Malipo Malipo.
Wanafuatilia
Wajumbe wa Bodi ya Ikona na wajumbe wa baraza la Jumuiya hiyo wakifuatilia



Wanasheria hawakucheza mbali kuhakikisha saini zinawekwa mahali husika


Thursday, July 13, 2017

UFUGAJI WA KONDOO WASHAMIRI ISSENYE SERENGETI

 Licha ya maeneo mengi kukabiliwa na ukame ,kondoo katika maeneo ya Issenye wilayani Serengeti wanazidi kushamiri,huku wafugaji wakikiri kuwa soko lake linaongezeka.
 Watoto wakipeleka kondoo kwa ajili ya kuchunga,hata hivyo ufugaji huo unadaiwa kuathiri masomo ya watoto.

Watalii wakipita barabara ya Issenye kuelekea hifadhi ya Taifa ya Serengeti kutokea Musoma.