Fahari ya Serengeti

Wednesday, September 21, 2016

ELIMU YA ATHARI YA UKEKETAJI YAZIDI KUTOLEWA MAKUNDI MBALIMBALI,WANASHERIA,WAZEE WA MABARAZA YA SHERIA,WAENDESHA MASHITAKA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAPATA DOZI

 Wawezeshaji wa mada za athari za ukeketaji na ukatili wa kijinsia wakifuatilia mjadala wakati wa semina kwa mahakimu,waendesha mashitaka,wazee wa mabaraza ya kisheria na watumishi wa mahakama wilaya ya Serengeti chini ya Mradi wa Tokomeza Ukeketaji unatekeleza na Amref health africa na LHRC,wa kwanza kushoto ni mganga mkuu wa wilaya Salum Manyatta,Anna Henga mwanasheria toka LHRC na Reginald Martini wakili toka LHRC.Ukumbi wa Anita Motel.
 Anna Henga akitoa mada
 Kila mmoja akiandika kila anachoona ni muhimu
 Anna Henga akielezea athari za ukatili wa kijinsia

 Dk Manyatta akielezea athari za ukeketaji kwa watoto wa kike
 mijadala inaendelea

 Picha ya Pamoja ilipigwa
 Wakili akitoa mada za kuhusu sheria na mikataba ya kimataifa inayopinga vitendo vya ukeketaji


MRADI WA TOKOMEZA UKEKETAJI SERENGETI WAWAJENGEA UWEZO MAHAKIMU NA WENYEVITI WA MABARAZA

 Mahakimu ,wenyeviti wa mabaraza ya Sheria na watumishi wa Mahakama wilaya ya Serengeti wajengewa Uwezo na Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti juu ya Athari za Ukeketaji kwa watoto wa kike,Mradi huo unaotekelezwa na Amref health africa na Kituo cha Haki za Binadamu(LHRC)kwa Ufadhili wa UN Women unalenga kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji.

 Baadhi ya wawezeshaji wakiwa wanafuatilia mjadala kutoka kwa wanasheria.
 Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti William Mtwazi(LHRC)akitoa maelezo ya mradi huo kwa mahakimu,wenyeviti wa mabaraza ya sheria na watendaji wa mahakama kwenye ukumbi wa Anita Motel.
 Meneja Mradi waTokomeza Ukeketaji Serengeti Godfrey Matumu(Amref health africa)akielezea malengo ya mradi na utekelezaji wake.

 Anna Henga mwanasheria kutoka LHRC akitoa ufafanuzi wa kazi za Kituo na umuhimu wake kwa jamii.

 Washiriki wa semina wakiwa wamesimama kwa ajili ya kutambuana
 Wanafuatilia mjadala
 Wawezeshaji wakiwa wanaendelea na maandalizi yao.









Tuesday, September 20, 2016

MASHINDANO YA NYERERE CUP YANAZIDI KUSHIKA KASI SERENGETI

 Timu 11 zinashiriki katika mashindano hayo uwanja wa sokoine serengeti kwa kushirikisha vijana wa kidato cha kwanza hadi cha tatu











UTALII AFRIKA KUSINI

 Huu ni uwekezaji uliofanywa na mtanzania mjini Johannesburg Afrika kusini ,ni fursa nzuri kwa wageni kutoka nchi mbalimbali kupumzika.
 Nje ya nyumba ya Marehemu Mandela,mawe hayo ni moja ya alama za watu wanaofika kutoa rambirambi,watu kutoka maeneo mbalimbali huandika kwenye mawe kama ukumbusho.
 Makabila manne yanabeba historia ya Afrika Kusini Zulu,Sotho,Xhosa na Pedi na wageni wengi humiminika kwenda kujifunza historia mbalimbali za nchi hiyo hapa ni ni kwenye kituo cha Lesedi Siyanamukera.

 Sun City kunapatikana mambo mbalimbali



 Mwongoza wageni katika kituo cha asili cha Makumbusho cha Lesedi Siyanamukera  Themba Meaya akielezea jinsi wanavyotengeneza chakula cha asili

HATUA ZA MWISHO ZA UWEKAJI LAMI MUGUMU MJINI

 Hatua za mwisho za uwekaji wa lami barabara ya kilometa tatu mjini Mugumu wilayani Serengeti ukiendelea .
 Baadhi ya mafundi na vibarua wakiwa wanaendelea na kusawazisha kokote
 Mtambo wa kuweka kokoto barabarani





Friday, September 16, 2016

UTALII UTALII


Utalii ulinifikisha katika hifadhi hii nchini Afrika kusini
 Ikulu ya Afrika Kusini iliyoko mjini Pretoria ni ni mali ya wananchi hivyo  fursa tosha ya Utalii na biashara,wamachinga wanaendesha biashara maeneo hayo na wapiga picha ,utaratibu huo ni tofauti na nchi nyingi ambazo hata kusogea wananchi hawaruhusiwi.
 Sanamu ya Mandela iliyoko mbele ya Ikulu ya Afrika Kusini ni fursa tosha ya utalii na kwa wauza bidhaa ikiwemo wapiga picha.





 Eneo hili lililoko Ikulu ya Pretoria ni maarufu pia kwa wapiga picha,kwao ni fursa ya utalii ,inachangia wageni wengi kufika na kupiga picha hata maharusi,kwa kuwa Ikulu ni mali ya wananchi,ni tofauti na nchi nyingine.