Fahari ya Serengeti

Wednesday, August 26, 2015

ACT WAZALENDO SERENGETI WAZINDUA KAMPEINI

 Kada wa Act Wazalendo jimbo la Serengeti akinadi sera za chama hicho siku ya uzinduzi.
 Viongozi wa Act wazalendo  baadhi wakisikiliza ,na wengine kutafakari kama inavyoonekana.



 Mashabiki wa Act wazalendo

 Mgombea wa Act wazalendo jimbo la Serengeti Thomas Burito akiwasiliana na mmoja wa makada wa chama hicho.
Mgombea wa Act wazalendo Thomas Burito mwenye Kipaza sauti akipongezwa na mashabiki wake kabla hajaanza kumwaga sera

Tuesday, August 25, 2015

IBADA YA KUSTAAFU KWA KATEKISTA LUDOVICK

 Waumini wa kanisa katoliki Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara waliofika katika ibada ya ya misa takatifu ya kumuaga katekista Ludovick Igonga aliyestaafu kwa umri.
 Wanaingia kanisani


 Wanakwaya wa kwaya ya Mt,Fransisco wa Asizi Parokia ya Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiingia kanisani kwa mbwembwe.
 Katekista Ludovick Igonga akiwa na Mkewe wakati wa Ibada ya misa takatifu ya kumuaga
 Mwalimu Peter Mwita akipiga kinanda wakati wa ibada hiyo.
Paroko Alois Magabe akiendesha ibada ya misa takatifu

CHADEMA WAANZA MIKUTANO YA AWALI KABLA YA UZINDUZI.

 Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya mti wakufuatilia mkutano wa Chadema jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara kwenye Uwanja wa Right To Play,mkutano huo waliodai ni awali utafuatiwa na uzinduzi rasmi wa Kampeini katika uwanja wa Mbuzi mjini hapo.
 Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mara Juma Porini ambaye ni Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Makunduzi,na mgombea udiwani kata ya Natta akimwaga sera .
 Mwenyekiti wa Chadema Wilaya wa pili kutoka kushoto Sang'uda Manawa ,katikati Marwa Ryoba Mgombea Ubunge jimbo la Serengeti,wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Bavicha wilaya Mchina mwenye kofia ambaye ni mgombea udiwani kata ya Mugumu wakifuatilia mkutano.
 Mashabiki na wanachama wa chama hicho wakifuatilia hotuba.




 Mwenyekiti wa Chadema wilaya akiwa na Mweka hazina wa chama wilaya ambaye pia alikuwa diwani wa kata ya Nyamatare,David Maganya.
 Mgombea Ubunge Marwa Ryoba akimwaga sera
 Watu wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Chadema.
 Mgombea akinadi sera
 Mgombea ubunge akimnadi mgombea udiwani kata ya Mugumu








Biashara ya Mkaa iliendelea kama kawaida wakati wa Mkutano wa Chadema kama inavyoonekana,

Monday, August 24, 2015

MATUKIO YA HAFLA YA KUSTAAFU KWA KATEKISTA LUDOVICK IGONGA PAROKIA YA MUGUMU SERENGETI

Na Serengeti Media Centre
Agosti 24,2015.
Viongozi wanatakiwa kusimamia vema rasilimali tulizonazo kwa ajili ya kukuza uchumi wanchi,badala ya kutegemea misaada toka nje ambayo  huambatana na  masharti magumu ikiwemo ndoa za jinsia moja.
Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Alois Magabe amesema hayo wakati wa ibada takatifu iliyoambatana na ubatizo wa watu 180,ndoa,komnio na kumuaga Katekista Ludovick Igonga ambaye amestaafu,kuwa mataifa yaliyoendelea yanatumia njia hiyo kushinikiza nchi zinazotegemea misaada kwao.
Padri Magabe amezitaka nchi za kiafrika kuepuka misaada hiyo ambayo inakiuka maandiko na utamaduni wa kiafrika,na kuwataka viongozi kusimamia vema raslimali zilizopo ziweze kutumika kwa maendeleo ya nchi ,ili kuondoa umaskini badala ya kunufaisha  watu wachache.
Kuhusu uchaguzi  Mkuu mwaka huu amewataka wananchi kuwa makini na wagombea wanaotishia uvunjifu wa amani kwa kauli zenye uchochezi,wanaojiingiza kwenye matendo ya ushirikina  wawaogope kama Ebola kwa kuwa wanatanguliza maslahi yao.
Mwisho.

Kwaya ya Mt.Fransisco wa Asizi Parokia ya Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara ambao ni mabingwa jimbo la Musoma wakitumbuiza katika hafla ya kumuaga katekista Ludovick Igonga ambaye amestaafu kazi hiyo aliyoitumikia kwa miaka mingi.
Burudani zinaendelea
Ni ujumbe ,ujumbe unatolewa
Kwaya ya Maria Mama wa Mungu Kanisa Katoliki Mugumu nao wanatoa burudani iliyoambatana na ujumbe mahsusi kwa mstaafu huyo.
Peter Mwita Mpiga kinanda na mwalimu wa kwaya ya Mt,Fransisco wa Asizi akiwa kazini.
Mambo yanaenda yakiongezeka.
Nasaha na shukrani kwa Mungu ni maneno yaliyotawala ukumbi kutoka kwa waimbaji.
Wajukuu wake hawakubaki nyuma wanaingia na keki ili wamlishe babu yao
Katekista na mkewe kama mwili mmoja wanakata keki wakishuhudiwa na wajukuu.

Wanawalisha babu na Bibi
Tendo la kutakiana heri halikusahaulika
Padri Alois Magabe paroko wa Parokia hiyo akitoa nasaha,katika ibada alisisitiza kupiga vita ushoga.







Katekista Ludovick akiwa na mkewe .