Na Serengeti Media Centre
Agosti 24,2015.
Viongozi wanatakiwa kusimamia vema rasilimali tulizonazo kwa
ajili ya kukuza uchumi wanchi,badala ya kutegemea misaada toka nje ambayo huambatana na masharti magumu ikiwemo ndoa za jinsia moja.
Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa
Mara Alois Magabe amesema hayo wakati wa ibada takatifu iliyoambatana na
ubatizo wa watu 180,ndoa,komnio na kumuaga Katekista Ludovick Igonga ambaye
amestaafu,kuwa mataifa yaliyoendelea yanatumia njia hiyo kushinikiza nchi
zinazotegemea misaada kwao.
Padri Magabe amezitaka nchi za kiafrika kuepuka misaada hiyo
ambayo inakiuka maandiko na utamaduni wa kiafrika,na kuwataka viongozi kusimamia
vema raslimali zilizopo ziweze kutumika kwa maendeleo ya nchi ,ili kuondoa
umaskini badala ya kunufaisha watu
wachache.
Kuhusu uchaguzi Mkuu
mwaka huu amewataka wananchi kuwa makini na wagombea wanaotishia uvunjifu wa
amani kwa kauli zenye uchochezi,wanaojiingiza kwenye matendo ya ushirikina wawaogope kama Ebola kwa kuwa wanatanguliza
maslahi yao.
Mwisho.
Kwaya ya Mt.Fransisco wa Asizi Parokia ya Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara ambao ni mabingwa jimbo la Musoma wakitumbuiza katika hafla ya kumuaga katekista Ludovick Igonga ambaye amestaafu kazi hiyo aliyoitumikia kwa miaka mingi.
Burudani zinaendelea
Ni ujumbe ,ujumbe unatolewa
Kwaya ya Maria Mama wa Mungu Kanisa Katoliki Mugumu nao wanatoa burudani iliyoambatana na ujumbe mahsusi kwa mstaafu huyo.
Peter Mwita Mpiga kinanda na mwalimu wa kwaya ya Mt,Fransisco wa Asizi akiwa kazini.
Mambo yanaenda yakiongezeka.
Nasaha na shukrani kwa Mungu ni maneno yaliyotawala ukumbi kutoka kwa waimbaji.
Wajukuu wake hawakubaki nyuma wanaingia na keki ili wamlishe babu yao
Katekista na mkewe kama mwili mmoja wanakata keki wakishuhudiwa na wajukuu.
Tendo la kutakiana heri halikusahaulika
Padri Alois Magabe paroko wa Parokia hiyo akitoa nasaha,katika ibada alisisitiza kupiga vita ushoga.
Katekista Ludovick akiwa na mkewe .
0 comments:
Post a Comment