Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Dk Stephen Kebwe akiwasilisha fomu za kugombea ubunge jimbo hilo kwa Msimamizi wa Uchaguzi wilaya Naomi Nnko.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Jimbo la Serengeti Dk Stephen Kebwe akiwasilisha fomu zake kwa msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo akiweka sahihi kukiri kupokea fomu za mgombea huyo.
Dk Kebwe akiagana na Msimamizi wa Uchaguzi.
Mosena Nyambabe mgombea ubunge kwa tiketi ya Nccr Mageuzi jimbo la Serengeti akiwasilisha fomu kwa msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko.
Anaweka sahihi kukiri kurudisha fomu
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Serengeti Naomi Nnko akiongea na Mosena Nyambabe,aliyesimama ni afisa uchaguzi jimbo hilo Prosper Ndiva akipitia fomu za mgombea huyo baada ya kurudisha.
Mosena Nyambabe akiwa na viongozi wa chama hicho katika ofisi ya Afisa Uchaguzi wilaya.
Msimamizi wa Uchauguzi jimbo la Serengeti Naomi Nnko akiwa na afisa uchaguzi Prosper Ndiva wakijadiliana na mgombea Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya Nccr Mageuzi Mosena Nyambabe,hayupo pichani.
Mosena Nyambabe Mgombea Ubunge jimbo la Serengeti akisalimiana na Msimamizi wa Uchaguzi wilaya Naomi Nnko .
Mgombea Ubunge jimboa la Serengeti kwa tiketi ya Nccr Mageuzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Taifa wa Chama hicho,kushoto Mosena Nyambabe akiwa na viongozi na wanachama wa chama hicho mara baada ya kurudisha fomu ya kugombea Ubunge.
Mgombea Ubunge kupitia Act Wazalendo Thomas Burito kulia akiwa amekaa na viongozi wa chama hicho katika ofisi ya Afisa uchaguzi wilaya ya Serengeti ,muda mfupi baada ya kurusdisha fomu.
UKAWA
WASAMBARATIKA-SERENGETI
Na Serengeti
Media Centre
Agosti
21,2015
Umoja wa
Katiba ya Wananchi(Ukawa)wilayani Serengeti Mkoa wa Mara umesambaratika,na kila
chama kinachounda umoja huo kimesimamisha mgombea ubunge ,na udiwani kila kata.
Katika
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika wilaya hiyo vyama vya Nccr Mageuzi na
Chama cha Wananchi(CUF)viliunda Umoja wao baada ya kushindwa kuelewa na uongozi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)waliotaka kuachiwa vijiji na
vitongoji vingi,ikiwemo maeneo ambayo vyama hivyo vilikuwa vinaongoza.
Mwenyekiti
wa Chadema wilaya Manawa Sang’uda akiongea na Serengeti Media Centre kwa njia
ya simu amesema pamoja na kuwa hawana waraka kutoka Makao Makuu ya chama chao
kuhusiana na kumteua Mgombea Ubunge jimbo hilo,wameamua kuchukua fomu na
kurudisha.
“Makao makuu
wameniambia kuwa jimbo hili tumepewa sisi,ingawa hawajatuma waraka wowote kuhusiana
na uamzi huo….imetupa wakati mgumu sana maana katika orodha ya majina ya wagombea
mkoa wa Mara,yapo majina ya wagombea tisa na jimbo hili halipo”amesema.
Serengeti
Media Centre ilipomuuliza taarifa zilizozagaa jimboni humo kuwa Chama cha Nccr
Mageuzi kati ya majimbo waliyoongezewa na hilo limo,alikiri kusikia taarifa
hizo,”ni kweli nimesikia lakini sasa makao makuu nao wanasema mgombea wetu
ndiye anayegombea”amebainisha.
Kuhusu
madiwani ,Mwenyekiti amesema kuwa haitawezekana kwa kuwa muda umekwisha na
wanaanza kampeini,”ni vigumu kwa sasa,Toolate”amedai Mwenyekiti.
Akiongea na
SMC mgombea ubunge kupitia chama cha Nccr Mageuzi ambaye pia ni Katibu Mkuu
Taifa wa Chama hicho Mosena Nyambabe,amesema yeye ndiye amepewa jimbo hilo
kupitia Ukawa ,ikiwa ni kutekeleza azimio la kikao cha Umoja huo kilichofanyika
Zanzibar.
“Miongoni
mwa makubalino yalikuwa ni palipo na kiongozi Mkuu wa Kitaifa wa Chama anapewa
nafasi ya kugombea,na ndicho killichofanyika hapa….katika majimbo kumi ya mkoa
wa Mara ,sisi tumepewa moja hili la Serengeti,nadhani wenzetu wanapaswa
kuheshimu makubaliano hayo na wasitake kila kitu wenyewe”anasema.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi(CUF)wilaya hiyo Joseph Rhobi amesema kuwa amejitahidi
kuhakikisha vikao vinakaa ili waweze kugawana kata na namna ya kuendesha
kampeini kwa umoja wao ili waweze kushinda.
“Vikao
viwili tulivyokaa Chadema hawakufika kabisa,tulikutana ofisi ya Nccr
mageuzi,wenzetu wakadai hawana nafasi,wana vikao vya uteuzi,wakapanga tukutane
jioni ofisi ya Cuf wilaya…..hawakufika wala hawakutoa taarifa,sisi na Nccr Mageuzi
tumeunda umoja wetu kama ilivyokuwa uchaguzi wa serikali za mitaa,maana
hawataki”amesema kwa masikitiko.
Smc
ilipotaka ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chadema,amekiri kutohudhuria kwa
madai kuwa alikuwa na majukumu,hata hivyo amekiri kupokea waraka kutoka makao
makuu ya chama chake kuwataka wakae wagawane kata kwa kuzingatia vigezo
vilivyowekwa.
Wakati huo
huo wagombea wa vyama vya Wananchi (CUF)Emakulata Mniko,Thomas Burito(Act
wazalendo)Dk Stephen Kebwe(CCM)Marwa Ryoba(Chadema)na Mosena Nyambabe(Nccr
Mageuzi(Nccr Mageuzi,wamerudisha fomu za kuwania Ubunge jimbo hilo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment