Mgombea Ubunge kupitia Act Thomas Burito na uongozi wa chama hicho wilaya wakiwa wamekaa wakimsikiliza afisa uchaguzi wa jimbo hilo Prosper Ndiva aliyesimama akitoa maelekezo ,aliyekaa ni msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.
Afisa uchaguzi jimbo la Serengeti Naomi Nnko akimkaribisha rasmi mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Act Wazalendo Thomas Burito.
Msimamizi wa Uchaguzi akitoa mwongozo kwa Thomas Burito mambo muhimu ya kuzingatia ili asipoteze sifa ya kuteuliwa kuwania ubunge jimbo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi akimkabidhi fomu za kutafuta wadhamini Thomas Burito(ACT)wa kwanza kulia ni katibu wa Act wazalendo wilaya Yohana Dise,Mwenyekiti wa wilaya Stephen Masatu
Msimamizi wa uchaguzi akimpongeza mgombea na kumtakia heri katika mchakato huo akisisitiza kuzingatia masharti yaliyomo ndani ya fomu.
Burito anasaini kupokea fomu zote.
Wanaagana
Wanachama na mashabiki wa CCM jimbo la Serengeti wakiwasili halmashauri ya wilaya wakimsindikiza mgombea ubunge jimbo hilo Dk Stephen Kebwe.
Dk Kebwe akiwa na viongozi wa chama wilaya,nje ya lango la kuingia halmashauri wakijadiliana kabla ya kuingia ndani.
Dk Kebwe akisindikizwa na viongozi na wanachama mbalimbali wa chama hicho kuelekea ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi wilaya.
Msimamzi wa uchaguzi akitoa maelezo kwa mgombea aliyekaa na viongozi na wananchama wa chama hicho.
wanasikiliza kwa makini maelekezo ya msimamizi wa uchaguzi.
Msimamizi akitoa ufafanuzi.
Msimamzi wa uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko akimlabidhi dk Kebwe fomu za kutafutia wadhamini na kanuni za kuzingatia.
Hata hawa walikuwepo
Anapokea fomu
Dk Kebwe akisaini kupokea fomu za kugombea
Dk Kebwe akiwa kwenye boda boda
ACT WAZALENDO,CCM WACHUKUA FOMU ZA UBUNGE
Na Serengeti Media Centre.
Agosti 18,2015
Serengeti:Wagombea
Ubunge jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara wameaswa kuepuka kufanya kampeini kabla
ya wakati ,na wanatakiwa kuzingatia kanuni na maadili ya uchaguzi kama
ilivyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Akikabidhi fomu kwa wagombea Ubunge wa vyama vya
ACT-Wazelendo Thomas Burito na Dk Stephen Kebwe (CCM)kwa nyakati tofauti
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko katika ofisi ya Afisa
uchaguzi,alisema ili kuepukana na siasa zisizostahili wanatakiwa kusoma vema
vitabu vya maadili.
Alisema kila mgombea anatakiwa kutafuta wagombea wenye sifa
kama ilivyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,na si kufanya kampeini kwa
kuwa muda wake haujafika ,na watakao kiuka taratibu hizo watakuwa wamepoteza
sifa za kuteuliwa kugombea.
“Zingatieni maelekezo yote
kama yalivyoanishwa kwenye fomu za kugombea ,maana zina makatazo ambayo
yanatakiwa kuzingatiwa ,kinyume chake mtawekewa pingamizi na kukosa sifa za
kugombea,”alisema.
Akiongea na Serengeti Media Centre mgombea ubunge kupitia Act
Wazalendo Burito alisema iwapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa atatumia mfuko wa jimbo kuwalipia bima afya watu
wasiokuwa na uwezo ili waweze kuwa wanapata matibabu.
“Wilaya yetu ina utajiri mkubwa wa rasilimali,hazijatumika
kutatua matatizo ya wananchi kutokana na kukosekana kwa mwakilishi makini,mimi
natarajia kuifanya kazi hiyo ili kutoa tafsri halisi ya jina lenye sifa kubwa
duniani lakini wananchi hawana maji safi ya kunywa,watoto wanakaa chini “alisema.
Kwa upande wake Dk Kebwe(CCM)alisema akichaguliwa atatekeleza
mambo yaliyoanishwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020,na kutumia juhudi binafsi atahakikisha mtandao wa
maji unasambaa kwa asilimia 65 vijijini na asilimia 90 mjini.
“Kwa kushirikiana na wenzangu tunapambana kuhakikisha mji wa
Mugumu unakuwa kitovu cha utalii,ili kufikia malengo hayo tutahakikisha
barabara ya Lami Makutano ,Mugumu hadi Loliondo inakamilishwa na barabara za
mji zilizokwishaanza kutengenezwa kwa kiwango cha lami zinaungwanishwa”alisema.
Kwa upande wa afya alisema watahakikisha wanakamlisha ujenzi
wa hospitali ya halmashauri na kuipatia vifaa,”kwa juhudi binafsi tayari
marafiki zangu wa Marekani wamekubali kuleta vifaa vyenye thamani zaidi ya sh 3 bilioni,ambavyo vitatumika wilayani hapa
ili kuondoa adha huko vijijini,”alisema.
Wagombea wanne wameishachukua fomu,Emakulata Mniko(CUF)Mosena
Nyambabe(Nccr-Mageuzi)Thomas Burito(Act Wazalendo)na Dk Stephen Kebwe(CCM)
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment