Paroko wa kanisa Katoliki Mugumu wilaya ya Serengeti Alois Magabe akiendesha ibada ya misa takatifu,picha na Serengeti Media Centre.
Na Serengeti Media
Centre
Ili kuachana na siasa zisizokuwa na tija ,watu wenye ushahidi wa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Edward
Lowassa kuwa ni fisadi,waweke wazi ili vyombo vinavyohusika vichukue hatua kwa
maslahi ya taifa.
Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu wilaya ya Serengeti Alois
Magabe katika mahubiri ya ibada takatifu ya kwanza nay a pili ,amesema kwa
serikali yenye kuheshimu utawala wa sheria,haiwezekani tuhuma za mtu zikatolewa
kwenye majukwaa badala ya kukabidhi vyombo vinavyohusika aweze kushughulikiwa.
“Karibu miaka kumi tunasikia fisadi fisadi,mla rushwa,hakuna
anayetoka na kuweka wazi tuhuma zake wananchi tuzijue ,tunashuhudia wezi,wenye
makosa na tuhuma mbalimbali wanakamatwa na kufikishwa mahakamani,wengine
wananchi wanawaua ….kwanini huyu anatajwa majukwaani hafikishwi kwenye vyombo
vya sheria,au ni chuki binafsi?,”amehoji.
Padri Magabe amesema siasa kama hizo haziwasaidii wananchi
kufikia maamzi sahihi kwa kuwa hazina tija,”mimi si mshabiki wa Chadema wala
CCM,lakini nakerwa na siasa za namna hii,nchi hii ina maadili ya
viongozi,utawala bora,inakuwaje Takukuru,Usalama wa Taifa,Polisi,wapelelezi na
Mahakama wapo,kwanini hafikishwi kwenye vyombo hivyo,maana majukwaa
hayashughulikii waharifu,”amebainisha na kuongeza.
“Kwa wakristo katika Zaburi ya 15 inasema,Bwana ni nani
atakayekaa katika hema yako,atakayefanya maskani yake katika kilima chako
kitakatifu…ni mtu aendaye kwa ukamilifu na kutenda haki,asemaye kweli kwa moyo
wake,asiyesingizia kwa ulimi wake,wala hakumtendea mwenziwe mabaya”amesema.
Amesema imefikia hatua hata kama kuna ukweli ama la ,wananchi
hawaamini kwa kuwa suala moja linazungumzwa kwa miaka mingi,lakini
anayetuhumiwa hafikishwi kwenye vyombo vya dola,maana kama amesababisha athari kubwa kwa jamii inawezekanaje apate
sifa za kugombea,na asikamatwe.
Amevitaka na vyombo vya habari visiishie kuandika na
kutangaza kama wanavyosema wanasiasa,bali wafanye uchambuzi na kuanisha tuhuma
zake zake kama zipo ili wananchi wazijue,kwa kuwa kinachosema ni
fisadi,mla rushwa na hakuna anayetoka kukabidhi ushahidi vyombo husika,badala
yake ni kuichafua familia hiyo bila
kosa.
Amehoji Lowassa ana
uwezo gani wa kuvishinda vyombo vya dola ,badala yake anasemwa majukwaani na
ameshiriki shughuli nyingi za kijamii ,kwa kipindi chote na kushika nafasi
mbalimbali ndani ya kamati zao za bunge ,na hao hao ndiyo walimchagua,sasa
wananchi watawaminije kwa wanayosema leo.
Kuhusu tuhuma za utajiri anaotajwa nao,amesema Azimio la
Arusha lilikuwa na misingi mizuri juu ya viongozi,kwa matajiri walibanwa na
kodi,”kazi ya serikali ni kutoza kodi kwenye shughuli zake zinazompa
utajiri,kama halipi waseme ili wananchi wamjue mapema ,”alisisitiza.
Akizungumzia sera ya mgombea urais wa Chama cha
Mapinduzi(CCM)John Magufuli ya kuanzisha
chombo cha kushughulikia wala rushwa na
mafisadi, kuwa ni ya Chadema ,hata hivyo amesema kutokana na rekodi yake iwapo
atashinda anaweza kusimamia sera hiyo na kuwabana watuhumiwa wote.
Amekemea siasa za matusi na chuki zinazotolewa na viongozi na
kuwataka waeleze mikakati yao ili wananchi wapime nani amejipanga kuliondoa
taifa katika matatizo yaliyopo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment