Na Serengeti Media Centre
Wakazi wa kijiji cha Mesaga kata ya Kenyamonta wilaya ya
Serengeti Mkoa wa Mara,wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji kutohamisha walimu kwa
shinikizo la watu,kwa kuwa inachangia kushuka kwa taaluma.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Chacha Getumbe
amesema hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji ulioitishwa kupinga uhamisho
wa Mwalimu wa shule hiyo Jimmy Ambrose
kwenda shule ya Msingi Kisaka,kuwa unatokana na kutoelewana kwa mwalimu huyo
na Padri wa Kanisa Katoliki Iramba
Johnson Kitunzi.
Amesema shule hiyo
yenye wanafunzi 527 ina hitaji walimu 12 ,lakini ina walimu 6 ,na kuwa mwalimu
huyo amehamishiwa kijijini hapo mwaka jana ili amuuguze mama yake ambaye ni
kipofu ,kutolewa kwake watabaki walimu watano
na watoto wao wataathirika kitaaluma.
Afisa elimu wilaya William Mabanga amekiri kuwepo kwa
mgogoro kati ya Padri na Mwalimu kwa masuala ya Kwaya,na kuwa ameishapokea malalamiko ya wananchi na mwalimu mwenyewe,na
kudai wamesitisha uhamisho huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Victor
Rutonesha amesema suala hilo litaangaliwa upya,na kudai kuwa taratibu za
uhamisho uzingatia sheria za utumishi wala si shinikizo.
Akiongea na Serengeti Media Centrea kwa njia ya Simu Padri
Kitunzi amekiri kuwepo mgogoro kati yake na Mwalimu huyo,lakini amekana
kuhusika na uhamisho wake kwa kuwa yeye hausiani na masuala ya serikali.
Viongozi wa kijiji cha Mesaga kata ya Kenyamonta wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kujadili hoja ya kupinga kuhamishwa kwa mwalimu wa shule ya Msingi Mesaga Jimmy Ambrose kwa shinikizo la Padri Johnson Kitunzi wa kanisa katoliki Mugumu baada ya kutoelewana.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kupinga uhamisho huo ambao wanadai una madhara kitaaluma kwa watoto wao.
Baadhi walishauri waandamane kwenda ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupinga uhamisho huo uliofanywa kwa maslahi ya mtu na kuathiri taaluma kwa watoto wao.
Wnatoa msimamo wao.
0 comments:
Post a Comment