Na Serengeti Media Centre
Ili kukabiliwa na upungufu wa
wataalam katika sekta ya Afya hapa nchini,Chuo cha Sayansi za Afya Kisare wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kinatarajia
kuanzisha kozi mbalimbali za utabibu.
Mkuu wa chuo hicho Joachim Urassa
akitoa taarifa katika mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa
wiki ,alisema wanatarajia kuanzisha kada za afya ,ikiwemo Stashahada ya
Utabibu,Maabara,Afya ya Mazingira na Famasia.
“Leo wamehitimu wataalam 120
ngazi ya vyeti na Stashahada katika fani za Ukunga na Uuguzi,na wote wanakwenda
kuhudumia jamii katika maeneo mbalimbali….lengo ni kuhakikisha wanasaidia jamii
kutambua na kushughulikia matatizo yao,na tunayo matarajio ya kuongeza fani
nyingine ili kupunguza tatizo la upungufu wa wataalam,”alisema.
Hata hivyo alikiri kuwepo kwa
changamoto za jamii na taasisi mbalimbali
zilizopo wilayani hapo kutokujitokeza kuchangia uboreshaji wa chuo hicho,ili
kukamilisha bwalo la chakula na jiko na bweni kwa ajili ya wavulana ambao
wanaishi nyumba ya kupanga nje ya chuo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Bodi ya Chuo hicho,Mchungaji Abunel Mathube aliwataka wahitimu kutumia vema
taaluma yao kuhudumia wananchi,”zingatieni maadili ya kazi,mmefundishwa katika
chuo cha kidini,tunategemea mkawe mfano maana mnacheza na maisha ya
watu,epukeni rushwa”alisisitiza.
Mapema Mkurugenzi wa hospitali
Teule ya Nyerere na Chuo hicho Dk Musuto
Chirangi alisema mafanikio ya kazi ya uuguzi si visingizio bali kuwajibika kwa
kuzingatia maadili kama walivyofundishwa,itakuwa imesaidia kutimiza malengo ya
mafunzo hayo na kupambana na adui maradhi katika jamii.
Chuo hicho kilichoko chini ya
kanisa la Menonite kilianza mafunzo 1998 na kilipata usajili wa muda baraza la
Elimu ya Ufundi(NACTE) mwaka 2004,kilipata usajili wa kudumu 2009 na
kinaendesha mafunzo ya uuguzi na Ukunga ngazi ya cheti na stashahada.
Maandamano ya wanachuo kuelekea ukumbi ulioandaliwa
Wanachuo wanaelekea ukumbini
Maandamano yanaendelea
Viongozi wa hospitali,wilaya na chuo wakiwa meza kuu.
Wanachuo wakiwa wanafuatilia matukio mbalimbali.
Wanakumbuka kiapo
0 comments:
Post a Comment