Nyambabe akimkabidhi nyaraka mbalimbali kabla ya kukabidhiwa fomu ya kutafuta wadhamini kabla ya uteuzi wa kuwania ubunge jimbo hilo.
Afisa uchaguzi jimbo la Serengeti Ndiva akitoa maelekezo mbalimbali ya tume kwa mgombea aliyeambata na viongozi wa wilaya hiyo.
Anatoa maelekezo ya kuzingatia
Nyambabe anapokea fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo
Afisa uchaguzi anapitia fomu huku akitoa maelekezo kuwa wasianze kampeini kabla ya uteuzi
Anapokea nyaraka
Sasa kazi ya kutafuta wadhamini waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura.
KATIBU MKUU NCCR MAGEUZI ACHUKUA FOMU,
Na Serengeti Media
Centre
Agosti 17,2015
Katibu Mkuu Taifa chama cha Nccr Mageuzi Mosena Nyambabe
amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara na kuanika vipaumbele vyake.
Akiongea na Serengeti Media Centre (SMC) baada ya kukabidhiwa
fomu na afisa uchaguz jimbo hilo Prosper Ndiva,Nyambabe amesema mambo ya kuanza
nayo ni madai ya walimu,kwa kuwa hayahitaji fedha zaidi ya
kufuatilia,uboreshaji wa elimu ,matumizi sawa ya mapato ya wilaya na migogoro
ya wakulima na wahifadhi.
Amesema matatizo ya walimu yanajulikana na kinachotakiwa ni
ufuatiliaji kwa ngazi husika ili waweze kulipwa stahiki zao na waweze kufanya
kazi kwa ufanisi,”nikipata ridhaa nitahakikisha tatizo hilo linakwisha,maana
halihitaji fedha…nitashughulikia suala la miundo mbinu ya elimu kama maabara na
vifaa ,maana mazingira yalivyo hayatoi nafasi nzuri kwa walimu kufundishia na watoto
kujifunzia”amesema.
Nyambabe amesema ili kutoa elimu nzuri na kuzalisha watu
wenye weledi ataelekeza nguvu kuboresha maabara na vifaa vyake kwa shule za
sekondari,na shule za msingi atahakikisha wanaboresha miundo mbinu.
Kuhusu mgawanyo sawa wa raslimali za umma zinazopatikana
amesema ataondoa kasumba iliyokuwa imejengeka kubagua baadhi ya maeneo
kimaendeleo,tabia ambayo amesema haijengi umoja wa wilaya.
“Wilaya yetu inazungukwa na maeneo yaliyohifadhiwa yenye
wanyama kama tembo na mengine yana wawekezaji..wananchi walitakiwa kunufaika na
raslimali hizo,badala yake wanazidi kuwa maskini maana wanacholima hawavuni,tembo
wanakula mazao ,watu wanauawa na wengine kujeruhiwa ,lakini hawalipwi
nitayatafutia ufumbuzi,”anasema.
Katibu Mkuu huyo amesema serikali na wadau wa uhifadhi
kushindwa kushughulikia matatizo hayo ni chanzo cha wananchi kuona uhifadhi
kama balaa badala ya baraka,hivyo atahakikisha kunawekwa utaratibu mzuri wa
kupunguza madhara kwa wananchi ili waweze kushiriki uhifadhi wa wanyamapori.
Akizungumzia Ukawa amesema kati ya majimbo kumi mkoani Mara
Nccr Mageuzi wamepewa jimbo moja tu la Serengeti kwa kuzingatia tafiti
zilizofanywa na wataalam wa Ukawa ,pia makubaliano wa viongozi wa Umoja kuwa
walipo viongozi wakuu wa kitaifa wanaachiwa jimbo.
“Vigezo vyote
vimefuatwa na nimeteuliwa kugombea jimbo hili,chama chetu kimekubali kuachia
majimbo tisa ya mkoa wa Mara na kusimamisha hili tu….mimi kama katibu mkuu
mwenza taifa wa Ukawa nilikubaliana na kuachia majimbo mengine na hivyo,ndani
ya chama nimeteuliwa kuwania nafasi hiyo”amesema.
Hata hivyo Emakulata Mniko kutoka Chama cha Wananchi
(CUF)kinachounda Ukawa amekuwa mgombea wa
kwanza kuchukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo.
Afisa Uchaguzi jimbo hilo Ndiva amesema kuwa wanatakiwa
kutafuta wadhamini na kurudisha fomu zao agosti 21 kwa ajili ya uteuzi na
hawaruhusiwi kuanza kampeini.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment