Na Serengeti Media
Centre(SMC)
Agosti 22,2015.
Katika uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2010 vyama vya CCM,CHADEMA na CUF vilitoa ahadi mbalimbali ambazo walipanga kuzitekeleza katika kipindi cha
miaka mitano.
Ahadi ambazo zililenga
kutoa majawabu ya matatizo ya
Ujinga,Umaskini,maradhi na kuimarisha utawala bora kwa jamii.
Kabla ya kuja na ahadi
mpya katika kampeini ambazo zimeanza ,hawajarudi kwa wananchi kama sehemu ya
tathimini nini tuliahidi,tumetekeleza nini,bado nini,je kuna changamoto
mpya,badala yake ndimi zao uhubiri mafanikio tu, kana kwamba waliyoyafanya yako
mbinguni ambako hatujafika.
Kazi nyingi
zilizofanyika ,utekelezaji wake umewahusisha wanancha kwa nguvu na michango
yao,sioni mantiki ya kuja na maneno
mengi kwa kuwa walishiriki katika utekelezaji wake, tunategemea waje waseme kwa
yake ambayo hayakufanyika ni kero kwa jamii,kwanini hayakufanyika,na kuna
mkakati gani.
Serengeti Media
Centre(SMC)inawarudisha kwenye ahadi za vyama vya CCM,CUF na CHADEMA walizotoa
mwaka 2010 ili wananchi waone
kilichoahidiwa ,kilichotekelezwa na nini wanaleta kipya,je kimezingatia matatizo
yao ama yameachwa.
CCM.
Chama cha Mapinduzi
(CCM)kupitia aliyekuwa mgombea wake Jakaya Kikwete alitoa ahadi 75 kubwa
,ambazo kama zingetekelezwa taifa lingesonga mbele na kuinua uchumi wa jamii.
Ujenzi reli mpya kutoka Dar es salaam mpaka mikoa ya kanda ya
Ziwa(Nzega),Mikoa ya Tanga kuwa jiji la viwanda(Tangamjini)Tabora kutumia maji ya
ziwa Victoria(Igunga)kulipa madeni ya chama cha Ushirika Mkoa wa
Shinyanga(SHIRECU)Shinyanga.
Kumaliza migogoro ya ardhi nchini(Dodoma)Wakulima kuacha
kutumia jembe la mkono(Dodoma mjini)Kuwapatia trekta wakulima –kata ya
Mrijo(Dodoma)Wananchi kutoondolewa Ranchi ya Misenyi(Kagera)Kujenga uwanja wa
ndege Misenyi(Kagera).
Kupanua uwanja wa Ndege Bukoba(Bukoba mjini)Kujenga uwanja wa
Ndege mkubwa Kigoma(Kigoma mjini)Mtukula kupatiwa umeme kutoka
Uganda(Kagera)Mikoa ya Kagera,Kigoma,Lindi,Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika
gridi ya Taifa ya Umeme(Kagera)Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu(Kagera).
Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino(Mbeya)Kununua Meli kubwa kuliko Mv
Bukoba(Kagera)Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiliamali,Serikali
kusaidia vyama vya Ushirika (Mwanza)Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa
Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na
waharifu(Mwanza),Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya Mkoa (Geita)Kulinda Muungano kwa
gharama zote(Pemba).
Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko ya
Kilosa(Morogoro)Kununua Meli mpya kubwa Ziwa Nyasa(Mbeya mjini)Kujenga bandari
Kasanga(Rukwa)Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano (Songea)Kufufua Mgodi wa
Makaa ya Mawe Kiwira(Mbeya)Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Pangani
kuzama(Tanga)Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa
vijijini(Iringa)Kujenga barabara yenye kiwango cha Lami kutoka Same mpaka
Kisiwani,Kihunio na kuunganisha na barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam(Same).
Kuboresha barabara za Igunga (Tabora)Kusambaza walimu 16,000
katika shule za sekondari zenye upungufu mkubwa wa walimu(Kisesa
Magu),Kusambaza vyandarua viwili kwa kila Kaya(Mbeya Mjini),Kuzipandisha hadhi
hospitali maalum saba nchini kuwa za rufaa ili kupunguzia mzigo hospitali ya
taifa ya Muhimbili(MNH)(Hydom Wanyama).
Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini,kikabila
na kisiasa(Musoma)Kulinda haki za walemavu (Makete),Kujenga barabara ya Makete
Njombe kwa kiwango cha Lami urefu wa kilometa 109(Iringa mjini),Kuenga barabara
ya Lami Musoma –Mto wa Mbu(Arusha mjini),Kuanzisha jimbo la
Ulyankulu(Shinyangamjini).
Kujenga barabara ya lami Manyoni Kigoma(Kaliua Tabora)Kukarabati
barabara ya Arusha Moshi(Moshi mjini)Kuboresha barabara ya Handeni ,Kondoa
mpaka Singida (Dodoma)Kuwafidia
wanakijiji ng’ombe waliokufa wakati wa kiangazi mwaka 2009(Longido),Vijiji
vyote vilivyoko kilometa 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa
Ziwa Victoria Shinyanga-Kahama
kuunganishiwa Maji,(Shinyanga).
Tatizo la umeme kufika kikomo novemba 2010 mkoa wa
Arusha(Arusha mjini)Kukopesha wavuvi zana za kilimo (Busekela wilaya ya
Musoma)Kuwapatia maji wakazi wa Longido(Longido)Kujenga barabara ya lami
kupitia pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Ngorongoro),Utekelezaji wa
mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza
mifugo yao vizuri,(Mbulu Arusha).
Kusambaza umeme,utoaji wa huduma za afya,na uboreshaji wa
kilimo cha umwagiliaji na utoaji wa ruzuku kwa wakulima 2010-2015(Babati
mjini)Kuongeza mara tatu wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo na kilimo
kwa mfumo wa Vocha -(Iringa),Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika(Iringa
mjini),Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya
nchi-(Ifunda).
Kutokomeza Malaria 2015(Bunda Mara)Kuwapa wanawake nafasi zaidi(Iringa)Kuisaidia
Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii(Kibandamaiti mjini Zanzibar),Kusaidia
Zanzibar kila panapohitajika msaada(Kibandamaiti Zanzibar)Serikali kujenga upya
bandari ya Mbambabay(Ruvuma)Ununuzi wa Meli Mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400(Mbambabay Ruvuma).
Kufufua chama kikuu cha Ushirika cha wakulima wa Mbinga(Ruvuma),Hakutakuwa
na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi wa 2010(Dar es Salaam),Mtwara kuwa mji wa
viwanda(Mtwara)Ujenzi wa kiwanda cha dawa ya viluwiluwi vya mbu,hospitali ya
Tumbi kuwa ya Mkoa(Kibaha),Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo
maalum la viwanda(Kibaha)Ujenzi wa reli kutoka Ubungo hadi Tegeta(Dar es
Salaam).
Kujenga kiwanda cha kusindika matunda mkoani
Pwani(Kibaha)Kuhifadhi zao la mpunga katika ghala la Taifa (Malinyi),kujenga
daraja la Kilombero lenye ukubwa wa mita 400(Morogoro)na kuboresha barabara za
vijijini kwa kiwango cha
changarawe(Kilombero)
CHADEMA.
Dk Wilbroad Slaa
akinadi sera za chama cha Demokrasia na Maendeleo mwaka 2010 alitoa ahadi 18
kubwa ,iwapo wangeshinda ambazo zingesaidia kukuza uchumi wa taifa na wananchi.
Kurudisha fedha za mradi wa Rada(Moshi),Kushughulikia suala
la taasisi ya kuweka na kuvuna pesa
(DECI-Uwanja wa Mashujaa Moshi),Kujenga nchi isiyo na ufisadi(Mwanza)Kufufua
Tanganyika ili irejee mezani kujadili Muungano na Zanzibar(Ifakara)Kufufua
uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo(Arusha) Kukata asilimia 20 ya
mshahara wa Rais(Mwanza),Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia
15(Arusha).
Kuweka Mwenge wa uhuru jumba la Makumbusho(Kilimanjaro),Kutoa
huduma bora za afya bure(Mwanza )Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi(Tarime)Kufuta
walimu wote wa cheti cha stashahada shule za sekondari na kuleta walimu walio
na shahada (Arusha)Kutoa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha
sita(Morogoro).
Kutoa huduma za afya bure kuanzia kituo cha afya hadi hospitali
ya rufaa(Mwanza)Kutoa ruzuku taasisi za kidini(Ifakara)Kusambaza magari aina ya
shangingi kwa jeshi la polisi ili wakamatie wahalifu badala ya mawaziri
kuyatumia(Ifakara)Mfuko wa saruji na bati kuuzwa sh 5,000(Bukoba)Kufuta pocho
ya chai serikalini.
CHAMA CHA WANANCHI(CUF)
Tofauti na wagombea
wengine Profesa Ibrahimu Lipumba alitoa
10 kubwa ambazo angepata ridhaa zingesaidia kutatua matatizo
yanayoikabili nchi na jamii.
Kubadili Katiba na kumteua Dk Mohamed Shein kuwa Makamu wa
Rais(Unguja)Elimu ya bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu(Tanga)Kubana
matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la Mawaziri(Tanga)Kuunda serikali
shirikishi(Mtwara)Kusimamia raslimali(Tanga),Kuimarisha miundo mbinu(Kidongo
chekundu).
Kusimamia na kuboresha afya(Kidongo Chekundu)Kuboresha
kilimo,viwanda na uwekezaji(Mtwara)Kudhibiti uuzaji wa zao la Korosho(Mtwara)na
Mfuko maalum wa kusomesha walemavu.
Tusubiri ahadi za Mwaka huu zitakazodumu kwa kipindi cha
miaka mitano,Tutaendelea kuwaletea taarifa mbalimbali kadri kampeini
zinavyoendelea ili wananchi waweze kuchukua uamzi sahihi wakati wa kupiga kura.
0 comments:
Post a Comment