Wauguzi ,waganga na madaktari wa hospitali Teule ya Nyerere wilaya ya Serengeti walijitahidi sana kuokoa maisha ya Nyantito Robert mkazi wa kijiji cha Bwitengi,ambaye alichomwa mshale kifuani,juhudi zao hazikuzaa matunda,aliaga dunia.
Serengeti Media
Centre(SMC)
Agosti 28,2015
Serengeti:Wakazi wa Kijiji cha Bwitengi wilaya ya Serengeti
Mkoa wa Mara wanaodaiwa kuvamia mji wa Robert Ntantato na kusababisha kifo,kujeruhi,kubomoa
mji na kupora vitu,wamesusa shughuli za
mazishi ya mwanakijiji mwenzao.
Uamzi huo unadaiwa ni mwendelezo wa msimamo wa vijiji vitano vya
Bwitengi,Morotonga,Rwamchanga,Miseke na Parknyigoti waliouweka agosti 26 mwaka
huu kupitia mkutano wa Jamii(Ritongo),kuhamisha familia ya Robert
Nyantato,aliyewashitaki baada ya kumnyang’anya ng’ombe tano kufuatia kijana
wake kukamatwa kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe mmoja.
Paulo Boche mkazi wa kijiji cha Burunga alisema ,mazingira
hayo yaliwalazimu majilani kusaidia shughuli
za mazishi baada ya wakazi wa kijiji hicho kususia kwa madai kuwa ametengwa na
jamii hiyo.
“Sisi kijiji jilani cha Burunga na ndugu zake ndiyo
tumeshiriki shughuli za mazishi ya Nyantato Robert ambaye anadaiwa kuchomwa
mshale agosti 26 nyumbani kwao mwaka huu
na kufia hospitali,kitendo hiki kwa kweli kimetusikitisha sana”alisema.
Alisema hakuna matanga yatakayofanyika,”kwa mila na desturi
mtu akiuawa katika mazingira kama haya hakuna matanga….na huzikwa nje ya mji
kwa kuwa huchukuliwa ni mkosi katika familia”alisema.
Rpc,
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Philip Karangi akiongea na Serengeti Media Centre(SMC) kwa njia ya simu ,alisema
watu tisa wameishakamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni wakazi wa kijiji
hicho.
“Tunaendelea na msako na wote wanaotuhumiwa watakamatwa ,wananchi
watambue kuwa kujichukulia sheria mkononi ni kosa kubwa….tunahimiza utawala wa
sheria,hatutamuacha hata mmoja anayevunja sheria,”alisema.
habari kutoka vijiji hivyo zinadaiwa kuwa watu wengi wamekimbilia porini wakikimbia kukamatwa kutokana na tuhuma za kuua,kujeruhi,kubomoa nyumba na kupora mali za Robert Nyantato.
Wanaharakati,
Mwenyekiti Mtendaji wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria na
Haki za Binadamu Samwel Mewama alisema,serikali kuruhusu vikao visivyokuwa vya
kisheria kutoa uamzi unaokinzana na sheria za nchi ndiyo matokeo yake.
“Jadi iko juu ya serikali hapa,wanaweza kukaa na kuamua
kumhamisha mtu,kupora mali zake,kuua,kuchoma mji ,lakini serikali imekuwa kimya
sana na matokeo yake yanasababisha taswira mbaya ya wilaya na jamii ya
Waikoma,”alisema.
Ilivyotokea.
Agosti 11 mwaka huu eneo la mnada wa Mugumu Sanja Robet(27)ambaye ni kijana wa Robert
Nyantato alikamatwa na ng’ombe mmoja anayedaiwa kuwa wa wizi,na kufikishwa
polisi.
Pamoja na kufikishwa polisi kwa hatua za kisheria ,wananchi
walivamia makazi ya Nyantato ambaye ni baba yake na kuchukua ng’ombe tano kwa
kosa alilotenda kijana wake ambaye ana mji wake.
Hata hivyo alifikisha malalamiko polisi na ofisi ya Mkuu wa
wilaya ,wananchi wakaamriwa warudishe ng’ombe hizo ,na agosti 26 mwaka huu
waliahidi kurudisha.
Katika kikao cha wananchi hao kwa mwanvuli wa
jadi(ritongo)agenda ya kurudisha ng’ombe ilikataliwa na kuamua
kumtenga,kumhamisha hapo kijijini,katika utekelezaji huo walimchoma mshale
kifuani Nyantato Robert na kusababisha kifo.
Pia walimjeruhi Robert Nyantato ,kubomoa nyumba na kupora
vitu mbalimbali ikiwemo mifugo.
Matukio Mengine kwa
jamii hiyo,
Mwanzoni mwa mwaka huu kupitia vikao vya ritongo watu watano
katika kata ya Ikoma waliuawa ,wengine makazi yao kuteketezwa,kuhamishwa kwa
kutuhumiwa kujihusisha na matendo ya uchawi.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment