Na SERENGETI MEDIA CENTRE(SMC)
Agosti 28,2015
Mkazi wa kijiji cha Nyichoka wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara,Mahiri Nchagwa(30)akiwa amelazwa katika hospitali Teule ya Nyerere kufuatia kushambuliwa na watu wanaodhaniwa majambazi,picha na Serengeti Media Centre.
Watu wawili wamejeruhiwa mmoja akiwa na hali mbaya baada ya
kutekwa kupigwa,kuporwa fedha na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi walioteka gari na pikipiki
katika kijiji cha Burunga wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Philip Karangi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo,agosti 27 majira ya kati ya saa 2na 3 usiku mwaka
huu,watu wasiojulikana walitega magogo na kuteka pikipiki ,Hiace ,kupora na
kujeruhi.
Mmoja wa majeruhi Mahiri Nchagwa(30) ambaye amelazwa katika
hospitali Teule ya Nyerere wilayani hapa kutokana na kujeruhiwa vibaya,alisema
alitekwa na watu watano waliokuwa na mapanga,na marungu na kumkata kata
,kumpora sh 300,000 ,simu na ufunguo wa pikipiki.
“Nilikuwa natokea mjini kuuza maziwa ,nilipofika eneo hilo
niliona matawi ya miti,nikadhani kuna gari limeharibika,nikasogea taratibu
nikakuta magogo makubwa yamewekwa barabarani….kusimama ghafla nikavamiwa na
watu watano”alisema na kuongeza.
“Mbele yangu kulikuwa na watu wawili waliovalia kofia za
kufunika uso,makoti marefu wana mapanga na rungu,nyuma walikuwepo
watatu,wakaanza kunishambulia kwa kunikata kata kwa panga,na kunipiga kwa
rungu,wakachukua fedha za mauzo,funguo na simu “alisema kwa kugugumia.
Majeruhi huyo alisema wakati wanamshambulia lilitokea gari
aina ya Hiace lililokuwa linatokea Bunda ,wakamuacha na kwenda kuwashambulia
waliokuwa ndani ya gari,akafanikiwa kukimbia huku akipiga yowe na kusaidiwa na
mtu mmoja ,aliyemfikisha hospitali kwa matibabu.
Hata hivyo hakuweza kuwatambua watu hao kwa kuwa kulikuwa ni
giza na walikuwa wameficha nyuso zao,Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara hakuweza
kutaja namba za gari na pikipiki,na alikiri kuwa hakuna mtu anashikiliwa
kutokana na tukio hilo,na uchunguzi unaendelea.
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Emiliana Donald alisema
majeruhi huyo anaendelea na matibabu,ingawa amejeruhiwa vibaya sehemu
mbalimbali za mwili,na kuwa majeruhi mwingine Samsoni Jeremia(24)mkazi wa Bunda
ameruhusiwa kutoka baada ya kupata matibabu.
Matukio ya watu kutega magogo na kuteka magari ya abiria
yanayotoka Bunda jioni yameanza kujitokeza tena,ambapo mwaka 2011/12,uharifu
huo ulishamiri .
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment