Fahari ya Serengeti

Wednesday, November 9, 2016

WAKAZI WA KENOKWE WILAYANI SEENGETI WACHUKUA UAMZI WA KUKATAA UKEKETAJI

 Wanapata elimu
 Wasanii nao wakielimisha kwa njia ya sanaa
 William Mtwazi ni Mwanasheria toka LHRC ambaye pia ni afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sheria kwa wanaojihusisha na ukeketaji kuwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu Namba 169(A)na sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009.
 Kiongozi wa Saiga Konokwe akitoa maelezo kwa wanasaiga wenzake kuachana na ukeketaji.
 Elimu ,walipo imewafikia.





 Wasanii hawakubaki nyuma

WAZEE WA MILA KOO YA WARENCHOKA WASEMA HAKUNA UKEKETAJI KWA WATOTO WA KIKE

Mwenyekiti wa wazee wa mila koo ya Warenchoka toka kijiji cha Merenga kata ya Nyansurura wilaya ya Serengeti Julius Marwa akitoa tangazo kwa jamii hiyo kupiga marufuku ukeketaji wa watoto wa kike wakati wa mkutano wa jamii(Ritongo)kijijini hapo,hata hivyo mwenyekiti huyo amelazimika kutoa maelezo polisi na kuandika kwa maandishi kuwa ukeketaji ukifanyika katika jamii hiyo awe wa kwanza kukamatwa,hatua hiyo ilikuja  baada ya kuwepo taarifa kuwa kuna wananchi wamejiandaa kukeketa watoto wao.
Wasanii wa Nyota Njema wakitoa ujumbe kwa jamii katika mkutano wa hadhara kijiji cha Merenga madhara ya Ukeketaji.
Wananchi wakifuatilia picha ya athari za ukeketaji iliyoonyeshwa katika mkutano huo.

Katibu Tawala wa wilaya Cosmas Qamara katikati akifuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo,kulia ni Inspekta John Kweka na kushoto ni Mtendaji wa kata hiyo Neema Binagi.
Wazee wa mila wakifuatilia mijadala
Mganga mkuu wa wilaya ya Serengeti Salum Manyatta akieleza athari za ukeketaji kisayansi
.




Saturday, November 5, 2016

NGARIBA NA WENZAKE WANASWA KWA TUHUMA ZA KUMKEKETA MTOTO

 Ngariba Nyabitara Magoiga(45)mkazi wa Kitongoji cha Kinyariri Mesaga kata ya Kenyamonta wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara anashikiliwa ma jeshi la polisi kwa tuhuma za kumkeketa mtoto wa miaka 16 akishirikiana na bibi yake na mtoto kwa madai ya kutimiza mila za Kingorema.

 Bibi yake na mtoto aliyekeketwa Nyakaho Msamba mkazi wa Mesaga kata ya Kenyamonta ni miongoni mwa wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kushirikiana na ngariba kumkeketa mjukuu wake ili atimize mila.
 William Mahemba baba yake na mtoto aliyekeketwa.

WANACHAMA WA TOUR OPERATOR WAMWAGA MISAADA KUNUSURU WANAFUNZI SERENGETI

 Ded Serengeti Mhandisi Juma Hamsini kulia akimkabidhi magodoro 311 makamu mkuu wa shule ya sekondari Serengeti Juvenary Chacha yaliyotolewa na baadhi ya wanachama wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania(Tato)baada ya bweni la shule hiyo kuungua moto na kuteketeza vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya wanafunzi.

Msaada huo ulioombwa na Serengeti media Centre ni pamoja na shula 208,blanketi 208,mito 311 na vyandarua 208 ukiwa na jumla ya thamani ya zaidi ya sh 25 milioni.

Kazi ya kushusha ikiendelea.
 Wanafunzi wakishiriki katika kushusha.


 Makabidhiano ya shuka

 Wanafunzi wakishuhudia kazi ya ushushaji wa msaada



Mwisho Ded alitoa onyo kwa watakaotumia vibaya msaada huo.

Tuesday, November 1, 2016

KOO YA INCHUGU YASEMA UKEKETAJI BASI

Wazee wa mila wa  koo ya Inchugu wilayani Serengeti wakiwa katika picha pamoja na viongozi wa serikali na taasisi za dini wakati wa mafunzo ya athari za ukeketaji kupiti Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na Amref na LHRC kwa ufadhili wa UN WOMEN ,kwa pamoja wazee wamesema ukeketaji wa watoto wa kike kwao basi kwa kuwa walikuwa hawajui athari zake.
Wakiweka mipango yao ili kutokomeza ukeketaji
Wanajadiliana
Wanafuatilia mada

Dc Nurdin Babu akiwa na baadhi ya viongozi akiwemo Ocd katika mjadala na wazee wa mila ili kuachana na ukeketaji  wa watoto wa kike

Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu Alois Magabe akiwaeleza wazee wa mila kuwan ukeketaji ni dhambi kwa kuwa unasababisha unaondoa kiungo cha mtoto wa kike na hakuna maandiko matakatifu yanayosema mtoto wa kike akeketwe bali wa kiume atahiriwe.




Mwezeshaji akitoa mada