Fahari ya Serengeti

Wednesday, November 9, 2016

WAZEE WA MILA KOO YA WARENCHOKA WASEMA HAKUNA UKEKETAJI KWA WATOTO WA KIKE

Mwenyekiti wa wazee wa mila koo ya Warenchoka toka kijiji cha Merenga kata ya Nyansurura wilaya ya Serengeti Julius Marwa akitoa tangazo kwa jamii hiyo kupiga marufuku ukeketaji wa watoto wa kike wakati wa mkutano wa jamii(Ritongo)kijijini hapo,hata hivyo mwenyekiti huyo amelazimika kutoa maelezo polisi na kuandika kwa maandishi kuwa ukeketaji ukifanyika katika jamii hiyo awe wa kwanza kukamatwa,hatua hiyo ilikuja  baada ya kuwepo taarifa kuwa kuna wananchi wamejiandaa kukeketa watoto wao.
Wasanii wa Nyota Njema wakitoa ujumbe kwa jamii katika mkutano wa hadhara kijiji cha Merenga madhara ya Ukeketaji.
Wananchi wakifuatilia picha ya athari za ukeketaji iliyoonyeshwa katika mkutano huo.

Katibu Tawala wa wilaya Cosmas Qamara katikati akifuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo,kulia ni Inspekta John Kweka na kushoto ni Mtendaji wa kata hiyo Neema Binagi.
Wazee wa mila wakifuatilia mijadala
Mganga mkuu wa wilaya ya Serengeti Salum Manyatta akieleza athari za ukeketaji kisayansi
.




0 comments:

Post a Comment