Fahari ya Serengeti

Wednesday, November 16, 2016

WANAWAKE WA KOO YA INCHUGU KEBANCHABANCHA WASEMA UKEKETAJI NI UKATILI

 Wazee wa mila wa Koo ya Inchugu Kebanchabanche wilayani Serengeti wakiwa kwenye mkutano wa Ritongo walioitisha kwa ajili ya kutoa tamko la kupinga ukeketaji wa watoto wa kike,licha ya wanaume kung'ang'ania mfumo huo wanawake walijitokeza na kusema hawakubaliani na ukatili huo kwa kuwa hakuna faida zaidi ya madhara na kuwa kama wanaume wanaona unafaa nao wakatwe sehemu zao za siri kama wanavyofanyiwa wao.
 Wakazi wa Kebanchabanche wakiwa kwenye mkutano wa Ritongo wakifuatilia igizo na maelezo yaliyotolewa na wataalam juu ya athari za ukeketaji.
 Wanafuatilia
 Wasanii wa Nyota njema wakiwa wanatoa elimu kwa njia ya sanaa juu ya madhara ya ukeketaji wa watoyo wa kike.

William Mtwazi Mwanasheria toka LHRC ambaye ni afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti akitoa ufafanuzi kuhusiana na sheria zinazoharamisha ukeketaji na adhabu zake kwa wanaokutwa na kuwaomba wananchi watii sheria bila shuruti kwa kuendeleza mila nyingine zisizokuwa na madhara.

0 comments:

Post a Comment