WAZAZI KIZIMBANI KWA KUKEKETA WATOTO
WAO WATATU,
Anthony Mayunga,Mwananchi
amayunga@mwananchipapers.co.tz
Serengeti.Wazazi wawili wamepandishwa
kizimbani kwa kosa la kuwakeketa watoto wao watatu kinyume cha kifungu cha
169(A)cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.
Mbele ya
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Amaria Mushi mwendesha Mashitaka
wa Polisi Paschal Nkenyenge aliwataja washitakiwa kuwa ni Chacha Kiheta(35)na
Mugusuhi Chacha(35)ambao ni mke na Mme wakazi wa kijiji cha Mesaga kata ya Kenyamota
wilayani Serengeti wanadaiwa kuwakeketa watoto wao watatu kinyume cha sheria.
Aliimbia
Mahakama kuwa washitakiwa kwa pamoja waliwakeketa watoto wao watatu wenye umri
wa miaka (17),(16) na (13) desemba 21 mwaka 2015 kijijini hapo na kukamatwa
novemba 10 mwaka huu,kwa kuwa kitendo hicho cha kikatili ni kinyume na kifungu
cha 169(A)cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo
washitakiwa baada ya kusomewa shitaka walikana kuwa si kweli ,kwa kuwa wao waliwakeketa
watoto wao mwaka jana si mwaka huu,wamepelekwa
mahabusu baada ya kukosa wadhamini licha ya dhamana yao kuwa wazi.
Kesi hiyo
ya jinai
namba 210/2016 imeahirishwa hadi novemba 24 mwaka huu itakapotajwa tena .
Hivi
karibuni katika mahakama hiyo ngariba Nyabitara Magori (45)na Nyakaho Msamba
(64) bibi wa mtoto wakazi wa kijiji cha Mesaga walifikishwa katika mahakama
hiyo kwa kosa la kumkeketa mtoto wa miaka (16)na kumsababishia dhara kuu,ambao
wanaendelea kusota rumande baada ya kukosa wadhamini.
Serikali
wilayani hapo imeishatoa agizo kwa watakaojihusisha na ukeketaji wakamatwe na
kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment