Thursday, August 4, 2016
UMOJA CUP MAMBO YAZIDI KUNOGA
Waamzi wa mchezo wa Mageta Fc na Burunga Fc wakiongoza timu kuingia uwanjani ,katika mchezo wa robo fainali ambapo Mageta Fc wamefuzu baada ya kuitoa Burunga Fc kwa bao 1-0 na katika mchezo wa awali Smartboys fc(Chamoto)walifanikiwa kuilaza timu ya Itununu Fc kwa bao 1-0 na leo Polisi Fc ,Tembo Fc ,Seronga na Kibeyo zinakamilisha michuano ya robo fainali.
Mwamzi akiwa kazini
Mwamzi akiwa kazini
Wednesday, August 3, 2016
TANESCO WATAKIWA KUHAMISHA NGUZO KUPISHA UJENZI WA BARABARA MUGUMU
Baadhi ya nguzo zinatakiwa kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami mjini Mugumu wilayani Serengeti,hata hivyo kumekuwa na kutupiana lawama kati ya Tanesco,halmashauri na mkandarasi.
Hatari nguzo hizo kutokutolewa barabarani
Hatari nguzo hizo kutokutolewa barabarani
Tuesday, August 2, 2016
MBUNGE SERENGETI AUNGANA NA WADAU WENGINE KUTOA ZAWADI KWA TIMU NNE BORA LIGI YA UMOJA CUP
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba ameahidi kutoa zawadi ya mipira minne kwa ajili ya washindi wa kwanza hadi wa nne Ligi ya Umoja Cup,ahadi hiyo ameitoa wakati anaongea na Serengeti Media Centre ambao ni Miongoni mwa waandaaji wa ligi hiyo iliyokuwa inashirikisha timu 12 ,na kati ya hizo timu sita zimeingia robo fainali ambayo inatarajiwa kuanza agosti 3 kwa kuzikutanisha timu za Smart boy's fc na Itununu Fc,itakayoanza saa nane uwanja wa Sokoine na mchezo wa pili ni kati ya Mageta Fc na Burunga Fc.
Mbunge amesema ameamua kutoa zawadi hizo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za waandaaji ambao ni pamoja na kampuni ya Sijui Kitu na Mageta ,na kuwa yeye anatarajia kuandaa ligi itakayoshirikisha timu zote za wilaya.
Kutokana na ahadi ya Mbunge ambayo amesema wakati wowote atatoa mshindi wa kwanza sasa atapata ng'ombe na mpira mmoja,wa pili mbuzi na mpira,watatu mipira miwili na wa nne mpira mmoja.
wakati huo Chuo cha Utalii Serengeti Setco wameahidi kutoa sh 40,000 kwa timu bora na wanaendelea kutafuta kikombe kwa ajili ya timu bora,na pia wanajitahidi kuhakikisha wanatoa zawadi kwa kipa bora,naye Paulo Magoiga(Pama Bazaar )ameahidi kutoa sh 50,000 kwa ajili ya mfungaji bora.
Waandaaji wanaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutoa zawadi kwa kuwa bado zawadi ya waamzi,na timu itakayokuwa imeonyesha nidhamu bora.
Mbunge amesema ameamua kutoa zawadi hizo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za waandaaji ambao ni pamoja na kampuni ya Sijui Kitu na Mageta ,na kuwa yeye anatarajia kuandaa ligi itakayoshirikisha timu zote za wilaya.
Kutokana na ahadi ya Mbunge ambayo amesema wakati wowote atatoa mshindi wa kwanza sasa atapata ng'ombe na mpira mmoja,wa pili mbuzi na mpira,watatu mipira miwili na wa nne mpira mmoja.
wakati huo Chuo cha Utalii Serengeti Setco wameahidi kutoa sh 40,000 kwa timu bora na wanaendelea kutafuta kikombe kwa ajili ya timu bora,na pia wanajitahidi kuhakikisha wanatoa zawadi kwa kipa bora,naye Paulo Magoiga(Pama Bazaar )ameahidi kutoa sh 50,000 kwa ajili ya mfungaji bora.
Waandaaji wanaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutoa zawadi kwa kuwa bado zawadi ya waamzi,na timu itakayokuwa imeonyesha nidhamu bora.
CHUO CHA SETCO WAJITOKEZA KUTOA ZAWADI KWA TIMU BORA LIGI YA UMOJA CUP
UMOJA CUP YAINGIA ROBO FAINALI KUANZIA AGOSTI 3 MWAKA HUU
Dc Serengeti Nurdin Babu akiwaasa wachezaji kutumia furasa hiyo kucheza kwa amani kwa kuwa kupitia Umoja Cup wengine wanaweza kupata fursa ya kwenda kucheza maeneo mengine,na kuahidi kuwa wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha uwanja wa Sokoine unakarabatiwa ikiwa ni pamoja na kujenga.mashindano ya Umoja Cup yaliyodhaminiwa na Serengeti Media Centre,Kampuni ya Sijui Kitu na Mageta yanatarajiwa kukamilika agosti 8 mwaka huu ambapo mshindi wa kwanza anapata Ng'ombe na Mpira ,wa pili Mbuzi na Mpira wa tatu Mipira miwili na wanne mpira mmoja ,zawadi hizo zimeongezeka baada ya Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuguswa ametoa mipira minne na kuahidi kuwa anatarajia kuanzia ligi yake itakayoshirikisha wilaya nzima.Aidha Pama Bazaar ameahidi kutoa sh 50,000 kwa mfungaji bora na Chuo cha Utalii cha Serengeti(SETCO)wameahidi kutoa sh 40,000 kwa timu bora na wanategemea kununua kikombe kwa ajili ya timu bora ,wadau walio tayari kutoa zawadi wanakaribishwa
WAUMINI WA KANISA LA KANISA LA MENONITELA KIINJILI (KMKT MUGUMU WAHITIMISHA MKUTANO WA VIBANDA
Askofu
mkuu wa kanisa la Menonite la kiinjili Tanzania(KMKT)Dayosisi ya Mwanza Lameck Manji
kushoto akiwa na askofu wa jimbo la Mara Naamon Kajeri wakati wa kuhitimisha mkutano
wa vibanda uliofanyika katika kanisa hilo mjini Mugumu
Wanakwaya kutoka Musoma kaskazin wakitumbuiza waumini katika mkutano wa vibanda(KMKT)Mugumu mjiniAskofu Mkuu wa Dayosisi Mara(KMKT) Naamon Kajeri akiwahubiri waumini katika moja ya ibaada za mkutano wa makambi jimboni Mugumu.
Mama Askofu Ester Kajeri akiwasalimu washiriki katika ibaada maalum ya mkutano.
Askofu Mkuu Dayosisi ya Mwanza Lameck Manji(kushoto)na Mchungaji Paulo Budaga wakisikiliza mafundisho ya ibaada katika mkutano wa vibanda jimboni Mugumu.
Mchungaji Mtatiro akiwafundisha washiriki wa KMKT kuhusiana na umuhimu wa Maombi.
Baadhi wa viongozi wa kanisa la KMKT wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mkutano wa vibanda katika jimbo la Mugumu mjini.
Wakati wa harambee watu wengi walijitokeza kuhakikisha kazi ya Mungu inaenda vizuri.
Kikundi cha kwaya kutoka Musoma Kusini nao walikuwepo kuhakikisha kazi ya Mungu inatendeka sawasawa.
Askofu Mkuu Naamon Kajeri akiwasalimia wageni na wenyeji katika ufumbuzi wa mkutano wa vibanda uliofanyika katika kanisa la Menonite la kiinjili Tanzania(KMKT)Mugumu mjini.
Wapigaji wa vyombo vya Muziki wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano.
| Washiriki na wakristo wa madhehebu mbalimbali wakifuatilia mahubiri katika mkutano uliofanyika jimboni Mugumu(KMKT). |
Waumini wakitoa sadaka zao kama shukurani ya ibaada katika mkutano wa vibanda(KMKT)
Askofu kiongozi Dayosisi ya Mara Naamon Kajeri(kulia)akimkaribisha Askofu Lameck Manji mbele ya madhabahu kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu katika mkutano.
Askofu mkuu wa kanisa la (KMKT) Dayosisi ya Mwanza Lameck Manji akihubiri neno la Mungu mbele ya washiriki.
| Baadhi ya waumini wakiendelea kupata mahubiri kutoka kwa Askofu Lameck Manji. |
Washiriki wakipeana mkono wa baraka mara baada ya kuhitimisha ibaada ya mkutano wa vibanda.










