Fahari ya Serengeti

Tuesday, August 18, 2015

MGOMBEA UBUNGE KUPITIA ACT WAZALENDO -SERENGETI ACHUKUA FOMU,

 Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Naomi Nnko akipitia nyaraka mbalimbali wakati mgombea ubunge jimbo hilo kupitia ACT-WAZALENDO Thomas Burito anachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
 Mgombea Ubunge kupitia Act Thomas Burito na uongozi wa chama hicho wilaya wakiwa wamekaa wakimsikiliza afisa uchaguzi wa jimbo hilo Prosper Ndiva aliyesimama akitoa maelekezo ,aliyekaa ni msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.
 Afisa uchaguzi jimbo la Serengeti Naomi Nnko akimkaribisha rasmi mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Act Wazalendo Thomas Burito.
 Msimamizi wa Uchaguzi akitoa mwongozo kwa Thomas Burito mambo muhimu ya kuzingatia ili asipoteze sifa ya kuteuliwa kuwania ubunge jimbo hilo.
 Msimamizi wa uchaguzi akimkabidhi fomu za kutafuta wadhamini Thomas Burito(ACT)wa kwanza kulia ni katibu wa Act wazalendo wilaya Yohana Dise,Mwenyekiti wa wilaya Stephen Masatu
 Msimamizi wa uchaguzi akimpongeza mgombea na kumtakia heri katika mchakato huo akisisitiza kuzingatia masharti yaliyomo ndani ya fomu.


 Burito anasaini kupokea fomu zote.

 Wanaagana
 Wanachama na mashabiki wa CCM jimbo la Serengeti  wakiwasili halmashauri ya wilaya wakimsindikiza mgombea ubunge jimbo hilo Dk Stephen Kebwe.
 Dk Kebwe akiwa na viongozi wa chama wilaya,nje ya lango la kuingia halmashauri wakijadiliana kabla ya kuingia ndani.

 Dk Kebwe akisindikizwa na viongozi na wanachama mbalimbali wa chama hicho kuelekea ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi wilaya.
 Msimamzi wa uchaguzi akitoa maelezo kwa mgombea aliyekaa na viongozi na wananchama wa chama hicho.
 wanasikiliza kwa makini maelekezo ya msimamizi wa uchaguzi.
 Msimamizi akitoa ufafanuzi.
 Msimamzi wa uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko akimlabidhi dk Kebwe fomu za kutafutia wadhamini na kanuni za kuzingatia.
 Hata hawa walikuwepo
 Anapokea fomu

 Dk Kebwe akisaini kupokea fomu za kugombea

 Msafara wa kuondoka ukiongozwa kwa pikipiki unaanza kuondoka kuelekea ofisini wakihanikizwa na tarumbeta
 Dk Kebwe akiwa kwenye boda boda


ACT WAZALENDO,CCM WACHUKUA FOMU ZA UBUNGE
Na Serengeti Media Centre.
Agosti 18,2015
 Serengeti:Wagombea Ubunge jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara wameaswa kuepuka kufanya kampeini kabla ya wakati ,na wanatakiwa kuzingatia kanuni na maadili ya uchaguzi kama ilivyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Akikabidhi fomu kwa wagombea Ubunge wa vyama vya ACT-Wazelendo Thomas Burito na Dk Stephen Kebwe (CCM)kwa nyakati tofauti Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko katika ofisi ya Afisa uchaguzi,alisema ili kuepukana na siasa zisizostahili wanatakiwa kusoma vema vitabu vya maadili.
Alisema kila mgombea anatakiwa kutafuta wagombea wenye sifa kama ilivyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,na si kufanya kampeini kwa kuwa muda wake haujafika ,na watakao kiuka taratibu hizo watakuwa wamepoteza sifa za kuteuliwa kugombea.
“Zingatieni maelekezo yote  kama yalivyoanishwa kwenye fomu za kugombea ,maana zina makatazo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa ,kinyume chake mtawekewa pingamizi na kukosa sifa za kugombea,”alisema.
Akiongea na Serengeti Media Centre mgombea ubunge kupitia Act Wazalendo Burito alisema iwapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa atatumia  mfuko wa jimbo kuwalipia bima afya watu wasiokuwa na uwezo ili waweze kuwa wanapata matibabu.
“Wilaya yetu ina utajiri mkubwa wa rasilimali,hazijatumika kutatua matatizo ya wananchi kutokana na kukosekana kwa mwakilishi makini,mimi natarajia kuifanya kazi hiyo ili kutoa tafsri halisi ya jina lenye sifa kubwa duniani lakini wananchi hawana maji safi ya kunywa,watoto wanakaa chini “alisema.
Kwa upande wake Dk Kebwe(CCM)alisema akichaguliwa atatekeleza mambo yaliyoanishwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020,na  kutumia juhudi binafsi atahakikisha mtandao wa maji unasambaa kwa asilimia 65 vijijini na asilimia 90 mjini.
“Kwa kushirikiana na wenzangu tunapambana kuhakikisha mji wa Mugumu unakuwa kitovu cha utalii,ili kufikia malengo hayo tutahakikisha barabara ya Lami Makutano ,Mugumu hadi Loliondo inakamilishwa na barabara za mji zilizokwishaanza kutengenezwa kwa kiwango cha lami zinaungwanishwa”alisema.
Kwa upande wa afya alisema watahakikisha wanakamlisha ujenzi wa hospitali ya halmashauri na kuipatia vifaa,”kwa juhudi binafsi tayari marafiki zangu wa Marekani wamekubali kuleta vifaa vyenye thamani zaidi ya  sh 3 bilioni,ambavyo vitatumika wilayani hapa ili kuondoa adha huko vijijini,”alisema.
Wagombea wanne wameishachukua fomu,Emakulata Mniko(CUF)Mosena Nyambabe(Nccr-Mageuzi)Thomas Burito(Act Wazalendo)na Dk Stephen Kebwe(CCM)
Mwisho.



Monday, August 17, 2015

KATIBU NCCR MAGEUZI TAIFA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE-SERENGETI

 Katibu wa chama cha Nccr Mageuzi Taifa Mosena Nyambabe kulia akimkabidhi afisa uchaguzi jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara Prosper Ndiva kushoto barua ya uteuzi ndani ya chama kuwania nafasi ya ubunge jimbo hilo,mwanzoni ni mwenyekiti wa chama hicho wilaya Tanu Mwita.
 Nyambabe akimkabidhi nyaraka mbalimbali kabla ya kukabidhiwa fomu ya kutafuta wadhamini kabla ya uteuzi wa kuwania ubunge jimbo hilo.
 Afisa uchaguzi jimbo la Serengeti Ndiva akitoa maelekezo mbalimbali ya tume kwa mgombea aliyeambata na viongozi wa wilaya hiyo.
 Anatoa maelekezo ya kuzingatia

 Nyambabe anapokea fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo
 Afisa uchaguzi anapitia fomu huku akitoa maelekezo kuwa wasianze kampeini kabla ya uteuzi
 Anapokea nyaraka



Sasa kazi ya kutafuta wadhamini waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura.



KATIBU MKUU NCCR MAGEUZI ACHUKUA FOMU,
Na  Serengeti Media Centre
Agosti 17,2015
Katibu Mkuu Taifa  chama cha Nccr Mageuzi Mosena Nyambabe amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara na kuanika  vipaumbele vyake.
Akiongea na Serengeti Media Centre (SMC) baada ya kukabidhiwa fomu na afisa uchaguz jimbo hilo Prosper Ndiva,Nyambabe amesema mambo ya kuanza nayo ni madai ya walimu,kwa kuwa hayahitaji fedha zaidi ya kufuatilia,uboreshaji wa elimu ,matumizi sawa ya mapato ya wilaya na migogoro ya wakulima na wahifadhi.
Amesema matatizo ya walimu yanajulikana na kinachotakiwa ni ufuatiliaji kwa ngazi husika ili waweze kulipwa stahiki zao na waweze kufanya kazi kwa ufanisi,”nikipata ridhaa nitahakikisha tatizo hilo linakwisha,maana halihitaji fedha…nitashughulikia suala la miundo mbinu ya elimu kama maabara na vifaa ,maana mazingira yalivyo hayatoi nafasi  nzuri kwa walimu kufundishia na watoto kujifunzia”amesema.
Nyambabe amesema ili kutoa elimu nzuri na kuzalisha watu wenye weledi ataelekeza nguvu kuboresha maabara na vifaa vyake kwa shule za sekondari,na shule za msingi atahakikisha wanaboresha miundo mbinu.
Kuhusu mgawanyo sawa wa raslimali za umma zinazopatikana amesema ataondoa kasumba iliyokuwa imejengeka kubagua baadhi ya maeneo kimaendeleo,tabia ambayo amesema haijengi umoja wa wilaya.
“Wilaya yetu inazungukwa na maeneo yaliyohifadhiwa yenye wanyama kama tembo na mengine yana wawekezaji..wananchi walitakiwa kunufaika na raslimali hizo,badala yake wanazidi kuwa maskini maana wanacholima hawavuni,tembo wanakula mazao ,watu wanauawa na wengine kujeruhiwa ,lakini hawalipwi nitayatafutia ufumbuzi,”anasema.
Katibu Mkuu huyo amesema serikali na wadau wa uhifadhi kushindwa kushughulikia matatizo hayo ni chanzo cha wananchi kuona uhifadhi kama balaa badala ya baraka,hivyo atahakikisha kunawekwa utaratibu mzuri wa kupunguza madhara kwa wananchi ili waweze kushiriki uhifadhi wa wanyamapori.
Akizungumzia Ukawa amesema kati ya majimbo kumi mkoani Mara Nccr Mageuzi wamepewa jimbo moja tu la Serengeti kwa kuzingatia tafiti zilizofanywa na wataalam wa Ukawa ,pia makubaliano wa viongozi wa Umoja kuwa walipo viongozi wakuu wa kitaifa wanaachiwa jimbo.
 “Vigezo vyote vimefuatwa na nimeteuliwa kugombea jimbo hili,chama chetu kimekubali kuachia majimbo tisa ya mkoa wa Mara na kusimamisha hili tu….mimi kama katibu mkuu mwenza taifa wa Ukawa nilikubaliana na kuachia majimbo mengine na hivyo,ndani ya chama nimeteuliwa kuwania nafasi hiyo”amesema.
Hata hivyo Emakulata Mniko kutoka Chama cha Wananchi (CUF)kinachounda Ukawa amekuwa mgombea wa  kwanza kuchukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo.
Afisa Uchaguzi jimbo hilo Ndiva amesema kuwa wanatakiwa kutafuta wadhamini na kurudisha fomu zao agosti 21 kwa ajili ya uteuzi na hawaruhusiwi kuanza kampeini.
Mwisho.

Thursday, August 13, 2015

KITARUNGU





















CUF SERENGETI WAANZA KUCHUKUA FOMU ZA UDIWANI

 Joseph Magoiga mgombea udiwani kata ya Stendi kuu mjini Mugumu akiwa katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Stendi Kuu Remmy Ngoso kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea udiwani kata hiyo.
Joseph Magoiga akionyesha fomu ya kugombea udiwani mara baada ya kukabidhiwa,kushoto mwenye fomu ni Grace Nyangeta Kagina anawania udiwani kata ya Morotonga

Friday, August 7, 2015

MAFUNZO YA UHAKIKI

 Charles Mrema mtafiti akifafanua malengo ya Mpango wa Tanzania Civic and Political Rights Tracking(UHAKIKI)unaolenga kuboresha taarifa ya Haki za Binadamu kuanzia ngazi za chini.
 Anafafanua huku wataalam wengine wa mpango huo wakifuatilia
 Mkuta Masoli mwanasheria na mratibu wa dawati la Uangalizi wa Hakiza Binadamu kutoka Kituocha Sheria na Haki za Binadamu wakati akifafanua namna ya utekelezaji wa mpango wa Uhakiki.
Mjadala inaendelea

MBUNGE ANAYEMALIZA MUDA WAKE ATOA MAGARI YA WAGONJWA.

Moja ya magari ya wagonjwa yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Serengeti na Naibu Waziri wa afya na ustawi wa jamii,dk Stephen Kebwe kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa katika vituo vya afya ya Natta na Iramba