.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti
Mkoa wa Mara
wamegawanyika huku kundi kubwa likipinga mpango wa
kumtetea aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri aliyevuliwa madaraka kwa
kushindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.
Uteuzi wa Goody Pamba ulitenguliwa Desemba
17 mwaka huu na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri
Mkuu(Tamisemi)Hawa Ghasia baada ya Rais Jakaya Kikwete
kuridhia watendaji wote waliohusika kuvuruga uchaguzi
wachukuliwe hatua.
Baadhi ya madiwani wakiongea na Serengeti media
Centre wamesema hawakubalini na mpango
unaoendeshwa na Mwenyekiti wa halmashauri wa kumtetea Pamba kwa madai kuwa
kufanya hivyo ni kupingana na uamzi wa Rais Kikwete kwa kuwakutofanyika
kwa uchaguzi siku iliyopangwa kumechangia kuleta matokeo mabaya kwa CCM
katika maeneo mengi.
“Mpango huo hatutakubaliana nao kwa kuwa hauna
maslahi kwa wilaya bali kikundi cha watu wachache ambao wanahofu
kuondolewa kwake mambo yao mengi yatajulikana….maana alikuwa na kikundi
cha madiwani wachache na watumishi aliowaona bora ,kukaa vikao kwa ajili
ya jambo hili ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi”anasema diwani
mmoja jina tunalo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Ng’oina anasema
kuwa watakaa wajadili kisha nao
watoe kauli kuhusiana na uamzi huo ambao anadai haukumtendea haki Pamba
kwa kuwa hakuhojiwa na mamlaka zake zauteuzi ili ajitetee.
“Huyu mama ameonewa maana hajahojiwa sehemu
yoyote…hakuna
aliyemlalamikia,baada ya kutokea dosari
aliahirisha kwa mjibu wa
sheria na kupanga tarehe nyingine,sasa kutengua
uteuzi wake katika
mazingira haya lazima nasi kama halmashauri
tulijadili kisha nasi
tutoe sauti yetu”alisema.
Hata hivyo katika kikao cha kamati ya madiwani ya
Mipango ,uchumi na
fedha kilichokutana desemba 23 mwaka huu
hakikufikia uamzi baada ya
hoja hiyo kuleta mgongano,huku wengine wakitaka
waliokuwa wasimamizi
wasaidizi wa uchaguzi nao wachukuliwe hatua.
Katika kikao cha desemba 30
bado hawakupata muafaka na kukubaliana uchunguzi ufanyike utakaofanywa na kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya ili kubaini watumishi wengine waliohusika
kuvuruga uchaguzi huo,waweze kuchukuliwa hatua.
“Kuna watu waliokuwa wananufaika kwa tenda na kupitishiwa
fedha kwa
ajili ya mambo yao kwa kivuli cha safari za
halmashauri ndiyo wako
mstari wa mbele kutaka wote tuungane nao….hili
jambo limesababisha
madhara makubwa kidemokrasia,na kwasasa wananchi
wanafuatilia kwa
karibu mambo yanayoendelea na fedha zao zinavyotumiwa,”anasema
diwanina kuongeza.
“Kuna mkakati wa kuchota fedha baadhi ya watu
waende Dar es salaam ama Dodoma kumtetea ,hizo ni fedha za wananchi
ambazo zingesaidia kwenye ujenzi wa vyumba vya maabara ama kulipia karo
watoto
watakaokosa karo…. Matendo kama haya yataendelea
kututesa kwa
jamii,”anasema.
Habari kutoka kwa chanzo kingine kilisema kuwa
baada ya kusikia Rais
Kikwete alipokuwa kwenye mapumziko ya sikukuu katika hotel ya Four Session ndani ya hifadhi ya Taifa yaSerengeti
,wanasiasa walitumwa ili arudishiwe
madaraka,hata hivyo hawakufanikiwa.
Mmoja wa watu ambaye
anadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na mkurugenzi aliyevuliwa madaraka na pia
mnufaika wa zabuni kwa kofia ya nafasi yake ndani ya Chama hakuwa tayari
kulizungumzia suala hilo baada ya mkakati wake kukataliwa.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa
vinavyounda Ukawa
wilayani hapa walisema kuwa uamzi wa kumvua
madaraka ulikuwa sahihi
kutokana na uzembe wa kufanya maandalizi ya
uchaguzi,huku wakidai kuwa katika vikao vyao vyote aliwahakikishia kuwa
maandalizi yamekamilika,wakati hali ilikuwa kinyume.
Wanasema kuwa hapakuwa na
maandalizi ya kutosha kwa kuwa hata baada ya kuahirisha uchaguzi bado vifaa vilipungua na kulazimisha watendaji
kuwa wanatoa nakala karatasi za
kupigia kura kwenye maduka,huku matukio ya watu kukamatwa na karatasi za kupigia kura yakijitokeza.
Mwisho.