Fahari ya Serengeti

Tuesday, January 31, 2017

KITUO CHA AFYA NATTA SERENGETI CHAPOKEA AMBULANCE

Dc Serengeti Nurdin Babu akitoa maelezo ya matumizi ya gari lililotolewa na serikali kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kwa Kituo cha Natta kabla ya kumkabidhi diwani wa kata hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Porini wa kwanza kulia,Ded Mhandisi Juma Hamsini,wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mwita Samweli.

 
 Ded Serengeti Mhandisi Juma Hamsini kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Porini muda mfupi kabla ya kukabidhiwa gari la Kituo cha Natta.
 Viongozi mbalimbali wakijadiliana kabla ya makabidhiano ya gari DFPA 2907 kwa ajili ya Kituo cha Afya Natta ambalo litasaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.

 Ded Serengeti Juma Hamsini akitoa maelezo ya matumizi ya gari hilo.

 Dc Nurdin Babu akimkabidhi gari Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Hamsini wa kwanza kushoto.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni diwani wa kata ya Natta Juma Porini kushoto akieleza watakavyotumia gari hilo kwa ajili ya kunusuru maisha ya akina mama wajawazito na watoto wachanga,baada ya kukabidhiwa.
 Dc akijaribu gari hilo.
 Mwenyekiti wa halmashauri baada ya kukabidhiwa gari akijaribu.



0 comments:

Post a Comment