Fahari ya Serengeti

Tuesday, January 3, 2017

KWAYA YA MT.MARIA YAADHIMISHA SIKU YA SOMO WAO KWA KISHINDO

 Baadhi ya Wanakwaya ya Mtakatifu Maria Parokia ya Mugumu wilayani Serengeti wakiendelea na mchezo wa kuumbuana ambao unawasaidia kuwajenga katika Upendo na Umoja ,ambapo kila mmoja humzawadia aliyemuumbua,ikiwa ni sehemu ya matukio ya siku ya kumbukumbu ya somo wao,siku ya familia takatifu,hawakusahau kuwatakia HERI YA MWAKA MPYA.
 Ulifika muda wa chakula na kila mmoja akashiriki,kazi na dawa.

 Mwenyekiti wa Kwaya Caltas Simion akitoa ufafanuzi wa kukutana kwao,wengine ni viongozi mbalimbali akiwemo Paroko Alois Magabe.
 Zawadi mbalimbali zilitolewa kama sehemu ya Upendo na Umoja.
 Wanakwaya wamemzawadia baiskeli mwanakwaya mwenzao ambaye anasimamia vyombo vya matangazo ili kumwezesha kufika maeneo mbalimbali wakati wa kutimiza majukumu yake,Hongera sana.

 Wapo waliopata kanga na zawadi mbalimbali,kwa ujumla sherehe ilifana sana.
 Mwalimu wa kwaya naye hakusita kueleza furaha yake kulingana na matendo makuu yaliyoonyeshwa na wenzake,mzidi kubarikiwa.
 Mambo yanazidi kuongezeka.
 Ni mapozi ya mwaka mpya.
 Zawadi zinazidi kuongezeka
 Hongereni
 Zawadi zinazidi kuongezeka kama inavyoonekana
 Kila mmoja alitoa nasaha kwa wenzake.
 Hongera sana.
Paroko Alois Magabe akitoa pongezi kwa matendo makuu yaliyofanywa na wanakwaya wa MT.MARIA,HERI YA MWAKA MPYA.

0 comments:

Post a Comment