Serengeti Media Centre
Ndege iliyokuwa imebeba watalii watano raia wa Marekani
imeanguka na kujeruhi Marubani wawili wa baada ya kupata hitilafu na kuanguka kisha kutketea kwa
moto wakati inapaa katika uwanja wa
Sasakwa wilayani SerengetI Mkoa wa Mara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Ramadhani Ng’hazi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo januari 2 mwaka huu katika Uwanja mdogo wa
ndege wa Sasakwa ulioko chini ya Kampuni ya Grumeti Reserves,baada ndege aina
ya CESNA F.406 Mali ya Air Excell iliyokuwa ikiongozwa na marubani Mohammed
Selemani akisaidiwa na Fahd Salehe kupata hitilafu na kuanguka na kuteketea kwa moto.
Alisema ndege hiyo
yenye uwezo wa kubeba abiria 12 siku ya tukio
ilikuwa na abiria watano ambao ni Greg Martin Perelman(60)Susan
Perelman(52) Sara Melissa Perelman (23) Danielle Jaffe Perelman(21)Emma
Stephanie Perelman(19)ambao ni familia moja
toka nchini Marekani ambao walinusurika .
Alisema baada ya ndege kupata hitilafu na kuanguka Perelman (baba wa familia hiyo) alifanikiwa
kuokoa familia yake yote na marubani wawili raia wa Tanzania ambao walishindwa
kutoka kutokana na majeraha waliyopata wasitekee kwa moto baada ya ndege kulipuka.
“Binafsi namwita shujaa kwa kuwa baada ya kutokea hitilafu
wakati wanaanza kupaa marubani walijaribu kutua na kushindikana,na kuanza
kuviringika,alichofanya akarusha watoto wake nje kupitia dirishani,kisha mke
wake,na baada ya kugundua marubani hawatoki na ndege inaanza kuwaka moto
aliingia na kuwatoa ingawa walikuwa wamejeruhiwa,”alisema Kamanda.
Alisema ndege imetekea yote na wachunguzi wa ajali toka
Mamlaka ya TCAA wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Kwa mjibu wa Taarifa ya maandishi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Singita Grumeti Graham
Ledger,kuwa wageni watano hawakupata majeraha ,lakini marubani wawili waliopata
majeraha walisafirishwa kwenda Nairobi nchini Kenya kwa ndege ya madaktari wa
amref (MEDIVAC servive)kwa ajili ya matibabu.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment