Thursday, July 7, 2016
Wednesday, July 6, 2016
SWALA YA IDD MUGUMU
Waumini wa Msikiti wa TAWHEED mjini Mugumu wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye swala ya Idd el fitri uwanja wa mbuzi leo.
Swala ikiendelea
Swala inaendelea ikijumuisha watu wa rika mbalimbali.
SWALA IKIENDELEA KAMA INAVYOONEKANA
Swala ikiendelea
Swala inaendelea ikijumuisha watu wa rika mbalimbali.
SWALA IKIENDELEA KAMA INAVYOONEKANA
Thursday, June 30, 2016
KATA YA KYAMBAHI WILAYANI SERENGETI YAVUKA LENGO KATIKA KUCHANGIA MADAWATI
Afisa Mtendaji wa kata ya Kyambahi wilayani Serengeti Mkome Manyanya akitoa ufafanuzi wa hitaji la madawati kwa sule tatu za msingi katani hapo ambapo madawati yaliyokuwa yakihitajika ni 174 yenye thamani ya zaidi sh 2 mil.lakini katika harambee hiyo iliyoendeshwa na Mwenyekiti wa Manispaa ya Musoma William Gumbo kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Musoma Mathayo Manyinyi na kupata zaidi ya sh 5 milioni.
Baadhi ya viongozi wa kata,tarafa,kijiji na wilaya wakiwa wamekaa wakisubiri utaratibu.
Mwenyekiti wa Manispaa ya Musoma William Gumbo akiwa anafungua baadhi ya michango ya wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya kata hiyo ambapo yeye na mbunge wa Musoma mjini walichangia madawati 60.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Naomi Nnko akisisitiza umuhimu wa jamii kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
MIFUGO ICHANGIE MAENDELEO YA WATOTO
KIELIMU,
Serengeti Media Centre
Jamii ya
wafugaji wilayani hapa Mkoa wa Mara inatakiwa kubadili mitizamo kwa kutumia
rasilimali walizonazo kusomesha watoto wao hasa wa kike badala ya kuwaoza.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini alisema hayo wakati wa
harambee ya kuchangia madawati katika kata ya Kyambahi kwa ajili ya shule za
msingi tatu zinazokabiliwa na upungufu wa madawati 174.
Alisema
sekta ya mifugo inahitaji wasomi na wataalam mbalimbali ambao watasaidia sekta
hiyo kutoa matunda mazuri,lakini baadhi ya
wafugaji wameshindwa kuwekeza
kwenye elimu ya watoto wao ambao watasaidia kusukuma maendeleo ya taifa.
“Wazazi
hakuna sababu ya kuwatupia lawama walimu juu ya kutofaulu kwa watoto kwenye masomo yao,chanzo ni ninyi wenyewe kutokuona
umuhimu wa kuchangia elimu na kuwaendeleza watoto,kuendelea na tabia hiyo
kutalikosesha taifa wasomi …wafugaji utajiri wenu wa mifugo utumike kuleta
mabadiliko kwenye familia zenu na jamii ,wekezeni kwenye elimu ndiyo faida
isiyokwisha thamani,”alisema.
Akiongoza
harambee hiyo iliyolenga kubata madawati 174 yenye thamani ya zaidi ya sh 2
milioni, na kufanikiwa kupata sh 5,124.200 ikiwa fedha taslimu sh3031200, ahadi
sh2,093,000, madawati 105 ahadi ngombe
3,mbuzi 4,Meya wa Manispaa ya Musoma William Gumbo alisisitiza wananchi kuwa
mstari wa mbele kuchangia maendeleo yao.
“Ni wajibu
wa wazazi kuandaa watoto wao kielimu ili waweze kupata mwanga wa kusaidia
jamii,hakuna mtu atakuja kuwasomeshea watoto wenu hilo ni jukumu la kila
mzazi,kwa kufanya hivyo mnawaandaa pia kuja kuwa wazazi bora,”alisema.
Gumbo pamoja
na kuchangia madawati 10 na kuwasilisha mchango wa madawati 50 ya mbunge wa
Musoma mjini Vedastus Mathayo ambaye amewekeza katika kijiji hicho,aliwataka
kuachana na dhana potofu kuwa serikali itafanya kila kitu kwa msingi wa elimu
bure,bali wazazi wanawajibu pia.
Mapema Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Kyambahi Mukome Manyanya na Mratibu elimu kata Nemes Sianga
wakitoa taarifa zao walisema mbali na upungufu wa madawati kata hiyo haina
shule ya sekondari hali inayochangia utoro kwa kuwa baadhi ya wanafunzi
wanatembea zaidi ya saa 4 kufika shuleni.
Walisema
moja ya mkakati walionao kwa kushirikisha jamii ni kujenga shule ya sekondari
ili kuwapunguzia safari ndefu wanafunzi,hali ambayo pia itachangia mazingira
rafiki ya kusoma.
Ili
kuhakikisha wilaya hiyo inakamilisha upungufu wa madawati zaidi ya 14,000 kwa
shule za msingi na sekondari ,kila kata imepewa jukumu la kutatua matatizo
yaliyopo,na wilaya inawaongezea kila kata madawati 20.
Mwisho.
Baadhi ya viongozi wa kata,tarafa,kijiji na wilaya wakiwa wamekaa wakisubiri utaratibu.
Mwenyekiti wa Manispaa ya Musoma William Gumbo akiwa anafungua baadhi ya michango ya wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya kata hiyo ambapo yeye na mbunge wa Musoma mjini walichangia madawati 60.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Naomi Nnko akisisitiza umuhimu wa jamii kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
WAJITOLEA KUJENGA BWENI ;KUWANUSURU WASICHANA RING'WANI SEKONDARI-SERENGETI
Ctherine Ruge Katibu wa shirika lisilo la Kiserikali la Girls Education Support Initiatives (gesi)kushoto akiwa ameshikana mkono na baba yake mzazi Ruge na wananchi wa kata ya Magange na Ring'wani wakimpongeza kwa uamzi wake wa kusaidia watoto wa kike katika shule ya sekondari ya Ring'wani wilayani Serengeti,shirika hilo limeanza ujenzi wa bweni la wasichana 56 ili kuwanusuru na adha wanazopata katika maisha ya upangaji kijijini,kazi hiyo itashirikisha mchango wa jamii.
Mapokezi ya vifaa yalishirikisha viongozi wa kada mbalimbali.
Catherine akiwa na wazazi na baadhi ya viongozi wa kijiji na kata ya Ring'wani na Magange baada ya mtoto wa kike kujitokeza kuwasaidia wadogo zake ili waweze kupata mazingira mazuri ya kuishi na wasome.
Mapokezi ya vifaa yalishirikisha viongozi wa kada mbalimbali.
WADAU WAAMUA KUJENGA BWENI KUNUSURU
WASICHANA NA MIMBA,
Serengeti Media Centre.
Ili
kuwanusuru wanafunzi wa shule za sekondari na mimba,utoro na ndoa za utotoni
zinazoendelea wilayani hapa Mkoa wa Mara shirika lisilo la kiserikali la Girls Education Support Initiatives(gesi)limeanza
kujenga bweni la wasichana katika
sekondari ya Ring’wani.
Inadaiwa
wasichana zaidi ya 36 wamekatishwa masomo wa sekondari na shule za msingi wilayani
hapa wamekatishwa masomo kutokana na ujauzito,pia ndoa za utotoni na utoro huku
ukosefu wa mabweni ukitajwa kama chanzo cha tatizo.
Katibu
Mtendaji wa shirika hilo lenye makao makuu yake wilayani hapa Catherine Ruge
alisema wameanza ujenzi wa bweni litakalosaidia watoto wa kike 56 ambao
wamepanga kijijini hapo katika mazingira yanayochangia kukata tamaa ya kusoma.
“Watoto
wamepanga kijijini hali inayowafanya waishi maisha kama ya unyumba,wengine
wanatoka mbali kiasi kwamba hawahudhurii masomo kwa wakati,waanza wengi
wanamaliza wachache na hawafanyi vizuri,ndiyo maana tukatafuta watu wa
kutusaidia ili kuwanusuru watoto wa kike,”alisema.
Mwalimu Mkuu
wa shule hiyo Elibariki Mwita alisema shule hiyo inahudumia kata mbili za
Ring’wani na Magange na wengi wanatoka mbali ,wanalazimika kupanga mtaani na
wengine wanatembea umbali mrefu hali ambayo inawafanya waache masomo.
“Kwa kipindi
cha miaka 13 wasichana 3 pekee ndiyo waliofaulu kwenda kidato cha tano,mwaka
2013 tulipokea wasichana 37 kuanza kidato cha kwanza,lakini waliopo sasa ni 20
pekee ,wasichana 9 wameacha shule ,wawili
wamerudia kidato cha pili na uhamisho wasichana watano,ukosefu wa bweni ni
tatizo kubwa hapa kwa kuwa maisha ya mtaani huwageuza kuwa wake za
watu,”alisema.
Na kuwa
katika mitihani ya majaribio ikiwemo ya BRN wasichana wote hakuna aliyefaulu
chanzo kikiwa ni ukosefu wa mabweni.
Ruge
akizungumzia mkakati wao alisema ujenzi huo wanategemea kukamilika mwishoni mwa
mwaka huu,”inagharimu zaidi y ash 85 milioni kama hakuna nguvu za
wananchi,lakini kwa kushirikisha wananchi ambao wamekubali kuchangia nguvu kazi
tunategemea kazi hiyo itagharimu zaidi y ash 50 milioni,”alisema.
Alisema
shirika lao linalolenga kumsaidia mtoto wa kike wilayani humo lina malengo ya
kusaidia shule mbalimbali kadri wanavyopata msaada,aliomba wadau wengine
kuwekeza kwenye elimu kama njia pekee ya kumkomboa mtoto wa kike anayekabiliwa
na vikwazo vingi ikiwemo mila na desturi.
Diwani wa
kata ya Magange George Mahemba alisema kupitia msaada huo wananchi wamekubali
kuchangia ili kuwanusuru watoto wa kike .
Mwisho.
Catherine akiwa na wazazi na baadhi ya viongozi wa kijiji na kata ya Ring'wani na Magange baada ya mtoto wa kike kujitokeza kuwasaidia wadogo zake ili waweze kupata mazingira mazuri ya kuishi na wasome.
WAKAZI WA KATA YA BUSAWE WILAYANI SERENGETI WAJENGA KITUO CHA AFYA NA KUKABIDHI HALMASHAURI.
Kituo cha Afya kilichojengwa na wakazi wa kata ya Busawe wilayani Serengeti waishio nje ya wilaya,kwa kushirikiana na walio katani hapo na halmashauri wamejenga kituo cha afya chenye thamani ya zaidi ya sh 150 mil.na kukabidhi halmashauri kwa ajili ya uendeshaji
Baadhi ya waliohuska na ujenzi huo wakiwa na uongozi wa wilaya kwa ajili ya kukabidhi jengo na vifaa na lengo lao ni kuhakikisha huduma za upasuaji zinafanyikia hapo.
Wananchi wakiwa katika majengo ya kituo hicho ambacho kitakuwa kimewapunguzia adha ya kwenda umbali mrefu kupata huduma za afya.
Viongozi wakijadiliana mambo ya kufanya.
Dk Geogre mmoja wa watu walioweza ujenzi wa kituo hicho akitoa maelezo kabla ya kukabidhi vifaa vya afya
Wakikabidhi vifaa
makabidhiano ya vifaa
Baadhi ya waliohuska na ujenzi huo wakiwa na uongozi wa wilaya kwa ajili ya kukabidhi jengo na vifaa na lengo lao ni kuhakikisha huduma za upasuaji zinafanyikia hapo.
Wananchi wakiwa katika majengo ya kituo hicho ambacho kitakuwa kimewapunguzia adha ya kwenda umbali mrefu kupata huduma za afya.
Viongozi wakijadiliana mambo ya kufanya.
Dk Geogre mmoja wa watu walioweza ujenzi wa kituo hicho akitoa maelezo kabla ya kukabidhi vifaa vya afya
Wakikabidhi vifaa
makabidhiano ya vifaa



















