Fahari ya Serengeti

Tuesday, December 8, 2015

PICHA ZA MATUKIO YA KUAPISHWA MADIWANI NA UCHAGUZI WA MWENYEKITI SERENGETI



Mbunge wa jimbo la Serengeti katikati Mwalimu Ryoba Marwa akisoma karatasi ya maelekezo ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri na Makamu wake,kushoto ni Katibu Tawala wilaya Cosmas Qamara na kulia ni Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti na wageni waalikwa wakisikiliza utaratibu utakaotumika kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo Naomi Nnko.
Wanapata maelekzo ya namna ya kuapa
Kiapo
Baadhi wanasaini Kiapo
Hawa wanasoma kiapo chao kabla ya kuapa
Ayubu Makuruma diwani wa Busawe CCM aligombea nafasi ya Mwenyekiti na kupata kura 15

Kiapo
Kiapo
Anaapa



Wanafuatilia kiapo

















Mwenyekiti wa baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini akiwashukuru madiwani na kutoa mwelekeo wa halmashauri hiyo katika kipindi chake cha uongozi.


Kura zinapigwa


Katibu Tawala akitoa maelekezo
Wanahakiki kura zilizopigwa
Zoezi la kuhesabu lilijumuisha mawakala kutoka vyama vya Chadema na CCM.

Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Serengeti ambayeni Mkurugenzi Mtendaji Naomi Nnko akifuatilia zoezi la upigaji kura.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Mwita Samweli katikati akipongezwa na mwenyekiti wa Chadema wilaya Sang'uda Manawa kulia.
HONGERA SANA.
PONGEZI ziliendelea baada ya kupata kura 28 dhidi ya 13 za mgombea wa CCM
ANATOA SHUKRANI.

John Heche mbunge wa jimbo la Tarime vijijini kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Serengeti Manawe katikati na Katibu wa Chadema Mkoa Chacha Heche kulia.
Mbunge wa jimbo la Serengeti Ryoba akiteta jambo na Mwenyekiti wa halmashauri Juma Porini,kulia ni makamu mwenyekiti.
Hongera kwa kuchaguliwa sasa tushirikiane kusukuma maendeleo ya wilaya yetu ili kukidhi matarajio ya wananchi,kauli ya Mbunge.


Picha mbalimbali zilipigwa baada ya uchaguzi.
Wao wanajiita makamanda




Kutokana na wingi wa watu wengine walikaa nje wakawa wanafuatilia mkkutano huo kwa kupitia vipaza sauti,ni tukio la kwanza toka halmashauri hiyo imeanza mfumo wa vyama vingi kukaa mpaka nje kama walivyokutwa.

Dua zilitolewa
Hata sala  pia
Wapiga picha walitekeleza majukumu yao






Saturday, December 5, 2015

WAFANYABIASHARA NA WAKAZI WA NHC MUGUMU SERENGETI WAOMBA JALALA LILILOKO NHC LIONDOLEWE ILI KUWANUSURU NA MAGONJWA YA MLIPUKO

 Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Gesase akitoa kilio chake
 mwendeshaji wa biashara ya baa na jiko katika nyumba ya Gesase
 Mfanya usafi wa katika jalala hilo akilalama ugumu wa kazi na ukosefu wa vifaa
 mwendesha biashara ya salon jilani na jalala hilo
 Mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa mji wa Mugumu





MBUNGE WA JIMBO LA SERENGETI MARWA RYOBA AMNUSURU MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA MERENGA

 Wakazi wa kijiji cha Merenga kata yaNyansurura wilayani Serengeti wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na agenda ya kujadili kero za viongozi wao kujichukulia sheria mkononi na kukamata mifugo kisha kuuza kinyamera,mkutano huo ulihudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Serengeti na diwani na afisa mtendaji wa kata hiyo.
 Afisa mtendaji wa kata hiyo Matororo akitoa maelezo ya utendaji wa viongozi wa serikali,alilazimika kuhudhuria mkutano huo baada ya afisa mtendaji kushindwa kushiriki mkutano ambao naye anathumiwa.
 Wanafuatilia maelezo
 Pamoja na mvua kunyesha lakini hawakutoka
 Mpaka kieleweke
 Hata wazee walikuwepo
 wengine walipanda juu ya miti kama inavyoonekana
 Mbunge alilazomika kumlipia Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho kwa kwanza kushoto baada ya kukiri kuuza mali za wananchi kinyamera na akawa ameishalamba laki moja ambayo wananchi waliitaka na mbunge kulazimika kumnusuru mikononi mwa nguvu ya umma,
 Mmenielewa,fuateni utaratibu,anasisitiza afisa mtendaji kata

 Diwani wa kata hiyo Francis Garatwa akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kijiji hicho,



 Baadhi ya walalamikaji waliokamatiwa ng'ombe zao wakiwa wemekaa wakisubiri utaratibu wa namna watakavyopata mali zao,wote walituhumiwa kuvamia mpaka wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti,na viongozi wakajigeuza Tanapa na kuanza kukusanya fedha ambazo hawakuzitolea stakabadhi.
 Ili kumusuru Mwenyekiti viongozi hao walilazimika kukaa kama kamati huku wananchi wakiwa wamewazunguka wasisubiri hatima ya mali zao,kwa kuwa wanadai kuchoshwa na dhuluma wanazofanyiwa na viongozi hao.
 Ndipo mbunge akamkabidhi mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Johanes waliyemchagua wao apokee fedha hizo badala ya mwenyekiti wao,hata hivyo mali zingine alisema atarejesha pindi afisa mtendaji wake atakapofika .
 Baada ya utatuzi wa mgogoro huo Mbunge alikutana na wakazi wa kijiji cha Nyansurura na kula nao matunda na hata uji wa jioni
 Wanapata matunda
 Kikafika kipindi cha uji kwa maandazi akaamua kununua na kunywa na wakazi hao,huku akisema hayo ndiyo maisha aliyokulia ,wakurya wanaita Kirunguri
 Mambo yanaenda yakiongezeka watu wengi wakajitokeza kupata uji na mambo yakawa kama inavyoonekana
 Ni kwa raha zao
 Na hata hao walikuwepo

Tuesday, December 1, 2015

MATUKIO MBALIMBALI YA WIKI SERENGETI

 Mafundi na vibarua wa kampuni ya Sama Investment ya mjini Mugumu Serengeti wakichimba na kujenga mtaro katika barabara ya mjini Mtaa wa Sedeco,kampuni hiyo inajenga kwa gharama zake ili kuwanusuru wananchi waliko pembezoni mwa barabara hiyo wanaoathirika na maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


 Hapa kazi tu mambo yanaendelea

 Akina mama wauza nafaka eneo la Sedeco mjini Mugumu wakiwa wanaendelea na biashara yao,kopo moja huuzwa sh 3,000 na debe sh 15,000 la mahindi.wanatakiwa kukumbukwa pindi mamilioni ya Magufuli yakianza kutoka.


 Katibu tawala Mkoa wa Mara Benedict ole Kuyan akiongea na wanufaika wa Mpango wa kusaidia kaya maskini kijiji cha Machochwe,wakati alipokuwa akikagua utekelezaji wa mpango huo kwa jamii.
 Nunueni kuku ili muweze kuzalisha taratibu ,hii ni mbegu imepandwa inatakiwa kumea na kustawi


 Mtaribu wa Tasaf Mkoa wa Mara akitoa maelekezo kwa wakazi wa kijiji cha Machochwe.
 Mkuu wa wilaya Ally Mafutah akitoa maelezo ya hali ya wilaya,walivyojipanga na Hapa kazi tu.
Wanabadilishana uzoefu