Fahari ya Serengeti

Saturday, December 5, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA SERENGETI MARWA RYOBA AMNUSURU MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA MERENGA

 Wakazi wa kijiji cha Merenga kata yaNyansurura wilayani Serengeti wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na agenda ya kujadili kero za viongozi wao kujichukulia sheria mkononi na kukamata mifugo kisha kuuza kinyamera,mkutano huo ulihudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Serengeti na diwani na afisa mtendaji wa kata hiyo.
 Afisa mtendaji wa kata hiyo Matororo akitoa maelezo ya utendaji wa viongozi wa serikali,alilazimika kuhudhuria mkutano huo baada ya afisa mtendaji kushindwa kushiriki mkutano ambao naye anathumiwa.
 Wanafuatilia maelezo
 Pamoja na mvua kunyesha lakini hawakutoka
 Mpaka kieleweke
 Hata wazee walikuwepo
 wengine walipanda juu ya miti kama inavyoonekana
 Mbunge alilazomika kumlipia Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho kwa kwanza kushoto baada ya kukiri kuuza mali za wananchi kinyamera na akawa ameishalamba laki moja ambayo wananchi waliitaka na mbunge kulazimika kumnusuru mikononi mwa nguvu ya umma,
 Mmenielewa,fuateni utaratibu,anasisitiza afisa mtendaji kata

 Diwani wa kata hiyo Francis Garatwa akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kijiji hicho,



 Baadhi ya walalamikaji waliokamatiwa ng'ombe zao wakiwa wemekaa wakisubiri utaratibu wa namna watakavyopata mali zao,wote walituhumiwa kuvamia mpaka wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti,na viongozi wakajigeuza Tanapa na kuanza kukusanya fedha ambazo hawakuzitolea stakabadhi.
 Ili kumusuru Mwenyekiti viongozi hao walilazimika kukaa kama kamati huku wananchi wakiwa wamewazunguka wasisubiri hatima ya mali zao,kwa kuwa wanadai kuchoshwa na dhuluma wanazofanyiwa na viongozi hao.
 Ndipo mbunge akamkabidhi mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Johanes waliyemchagua wao apokee fedha hizo badala ya mwenyekiti wao,hata hivyo mali zingine alisema atarejesha pindi afisa mtendaji wake atakapofika .
 Baada ya utatuzi wa mgogoro huo Mbunge alikutana na wakazi wa kijiji cha Nyansurura na kula nao matunda na hata uji wa jioni
 Wanapata matunda
 Kikafika kipindi cha uji kwa maandazi akaamua kununua na kunywa na wakazi hao,huku akisema hayo ndiyo maisha aliyokulia ,wakurya wanaita Kirunguri
 Mambo yanaenda yakiongezeka watu wengi wakajitokeza kupata uji na mambo yakawa kama inavyoonekana
 Ni kwa raha zao
 Na hata hao walikuwepo

0 comments:

Post a Comment