Fahari ya Serengeti

Friday, December 18, 2015

MBUNGE NA MADIWANI WA CHADEMA WASHUKURU WAKAZI WA MJI WA MUGUMU SERENGETI KWA KUWACHANGUA NA KUTOA SERA NINI WATAWAFANYIA

 Mbunge wa jimbo la Serengeti Mwalimu Marwa Ryoba akielezea mikakati yao katika mkutano wa kuwashukuru wakazi wa mji wa Mugumu baada ya kumchagua yeye na madiwani ambao wameweza kuongoza halmashauri hiyo,miongoni mwa mambo aliyofafanua ni kupitia upya mikataba ya wawekezaji kwa lengo la kuhakikisha inakuwa na maslahi ya wanaserengeti na Taifa.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini diwani wa kata ya Natta Chadema akielezea mikakati ya halmashauri hiyo baada ya kuchaguliwa ,miongoni mwa mambo wanayokusudia kufanya ni kuhakikisha wawekezaji wote wenye kambi na hoteli za kitalii katika maeneo yanayowazunguka wafungue ofisi mjini Mugumu ili kurahisisha mawasiliano,kuliko hivi sasa wanafanya biashara Serengeti lakini ofisi ziko Arusha ,wakazi wa wilaya hiyo inawawia vigumu kuwafikia wanapokuwa na shida.
 Mwenyekiti wa chadema wilaya Sang'uda Manawa akisisitiza jambo kwa madiwani wa chadema kuwa wawatumikie wananchi si kwenda kufanya biashara na hiyo ndiyo itawatofautisha na waliokuwa wanaongoza halmashauri hiyo,na atakaye kwenda kinyume na maelekezo ya chama hawatasita kumvua wadhifa wake wa uwakilishi.
 Wananchi wakifuatilia mkutano huo licha ya mvua kunyesha lakini hawakujali
 Anasisitiza kuwa wale waliohusika na wizi kwa dhamana walizokuwa nazo wakibainika hawatasita kutumbua majipu ,kwa kuwa wizi wao umechangia wananchi wa wilaya kutopata huduma stahiki.


 Wanamsikiliza mwenyekiti wa halmashauri akimwaga sera,miongoni mwa mikakati yao ni kuhakikisha halmashauri inanunua mitambo yake ya kujengea barabara ambayo itawasaidia kuchimba malambo kwa wananchi hasa wafugaji,na fedha za mfuko wa barabara zitumike kujenga madaraja,mitaro na kalvati
 Mmenielewa........



0 comments:

Post a Comment