Shughuli za kuweka mji wa Mugumu safi zinaendelea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk John Magufuli la kuitumia sikukuu ya Uhuru kwa kufanya usafi,hapo taka zinahamishwa kwenye jalala lililoko mtaa wa NHC kama inavyoonekana.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti wakikusanya Taka jalala la NHC tayari kwa kusombwa na magari.
HAPA KAZI TU.
Usafi ni kila kona.
Watumishi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mugumu wakifanya usafi maeneo yao ya ofisi.
Kazi kazi kazi ya usafi kila kona.
Anasisitiza jambo kuhusiana na usafi.
Watumishi wa halmashauri walitawanyika kila kona kama inavyoonekana lengo ni kuhakikisha mji uwe safi,kumbe inawezekana.
Wanazibua mtaro ili uweze kupiisha maji ya mvua kwa urahisi kwa kuwa maji yanapotuama hugeuka kuwa mazalia ya mbu na ni mwanzo wa kupata ugonjwa wa malaria .
Hawa hawapo hapo kwa ajili ya kupima afya zao,bali kufanya usafi .
HAPA KAZI TU anasikika akisema wakati anatoa tope na taka zingine ndani ya mtaro.
Eneo hili ni uwanja wa Mbuzi karibu na Meeting Point,kuna watu wamegeuza kuwa kituo cha kukusanyia taka,hatua za haraka zinahitajika kwa kuwa patageuzwa kuwa dampo kama ilivyoanza kuonekana.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Naomi Nnko naye hakuwa nyuma kuhakikisha maeneo yanakuwa safi na salama kama inavyoonekana hapo.
HAPA KAZI TU MPAKA PAWE SAFI.....
DSO naye hakubaki nyuma katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli.
Afisa elimu shule za msingi William Mabanga naye alishiriki kufanya usafi katika eneo la Wazi NHC.
Polisi kwao wanasema hilo ni sehemu ya zoezi kama wanavyoonekana.
Ni sehemu ya ukakamavu.
Si shamba la ushirika ,bali ni askari polisi wanafanya usafi kwa umoja kama inavyoonekana.hapa kazi tu.
Kila mtu na jembe lake
Zozezi hili limewakusanya watu mbalimbali wakiwemo watoto kama inavyoonekana.
Usafi usafi usafi.
Si migomba bali ni taka anapeleka jalalani.
Wednesday, December 9, 2015
Home »
» WATUMISHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUFANYA USAFI MAENEO MBALIMBALI SERENGETI.
0 comments:
Post a Comment