Mbunge wa jimbo la Serengeti Mwalimu Ryoba ameahidi wananchi kuwa hawatasita kuwatumbua majipu wale watakaobainika kuiba ama kufuja fedha za halmashauri hiyo kwa kutumia nyadhifa zao,kwa kuwa vitendo hivyo vimechangia wananchi kutopata huduma nzuri za kijamii.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini amesema kuwa wenye kambi za kitalii waliowekeza katika maeneo yaliyomo wilayani hapo,kama hawatafungua ofisi zao mjini Mugumu bora waachane nao,kwa kuwa kuweka ofisi Arusha wakati wamewekeza wilayani hapo kunawanyima fursa wananchi kupata kazi,hata kuuza bidhaa kwa kuwa mambo yote hufanyikia Arusha,kuendelea na watu wa namna hiyo ni kuzidi kudumaza mji na wilaya hiyo.
Saturday, December 19, 2015
Home »
» MBUNGE JIMBO LA SERENGETI ASEMA WALIOHUSIKA NA WIZI WA MALI YA UMMA WAKIBAINIKA WATAWATUMBUA MAJIPU
0 comments:
Post a Comment