Fahari ya Serengeti

Thursday, December 10, 2015

MATUKIO YA SIKU YA KUHITIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA SERENGETI.

Askari wa usalama barabarani Mugumu Serengeti akiongoza wasichana waliokimbia kukeketwa kutoka Ngoorongoro,Tarime na Serengeti Mkoani Mara ,ambao wamehifadhiwa katika Kituo cha Nyumba Salama Mugumu ,na wadau wengine kwenye maandamano ya siku ya kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili.


Maandamano yanaendelea kwa kupita mjini Mugumu huku wakipaza sauti kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji ambao umeanza katika maeneo ya Ngorongoro,Tarime ,Rorya na kufuatiwa na Serengeti.
Hata wenye mikokoteni ya ng'ombe walikuwepo.




Wadau mbalimbali walikuwepo




Usalama barabarani ulizingatiwa kama inavyoonekana kamanda akiwa kazini.

UKEKETAJI KWETU NI KAMA MAHABUSU,ANASIKIKA AKIPAZA SAUTI.








Mabango yenye ujumbe mbalimbali yalitawala
Diwani wa kata ya Mugumu Mjini Joseph Kihungwe maarufu kama Mchina kushoto akipokea maandamano,kulia ni Mwenyekiti wa shirika la Wasaidizi wa kisheria na Haki za Binadamu Smawel Mewama ,ambaye alikuwa mwenyekiti wa maandalizi kwa siku hiyo iliyojumuisha mashirika kama WASHEHABISE,CCT,IMARA,RIGHT TO PLAY,NYUMBA SALAMA,POLISI,SERENGETI MEDIA CENTRE,DC,DED na wanaharakati mbalimbali.

Wanasikilia ujumbe mahsusi

jumbe mbalimbali zinatolewa.


Anafuatilia nyimbo zenye ujumbe mkali wa kulaani vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao umewageuza wakimbizi,





Afisa tarafa ya Rogoro Maisha Mwaisengere kwa niaba ya Dc akitoa ujumbe mzito wa serikali.




Diwani mchina akitoa ujumbe
Alichangia chakula na fedha ili waweze kupata huduma,

Madiwani walioambatana na mgeni rasmi walitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto hao.
Diwani kwa kuguswa na matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa mahindi kwa ajili ya chakula,hongera kwa kuguswa.



0 comments:

Post a Comment