Fahari ya Serengeti

Monday, December 14, 2015

UTALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.


Utalii wa ndani uliohusisha familia yangu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,ikiwa ni moja ya njia ya kuwawezesha watoto kujifunza mambo mbalimbali ya uhifadhi ambayo wanayasoma kwenye vitabu.njia hiyo pia inawafanya wawe mabalozi wazuri kwa wengine juu ya umuhimu wa uhifadhi na utalii.
Hapo ni lango la kuingia la Ikoma
Niko kamanda wangu willy
Safari inaendelea huku wakifurahia uumbaji wa Mungu ndani ya hifadhi hiyo maarufu,ambayo iko wilayani kwetu Serengeti
Safari inaendelea vizuri kama wanavyoonekana hawa
Kila mmoja alikuwa akifuatilia matukio mbalimbali kadri macho yake yalivyoweza kuangaza kila kona .
Bata maji hawa ni maarufu sana inasemekana wana uwezo mkubwa wa kuruka na husafiri nchi moja hadi nyingine bila paspoti,ni miongoni mwa vivutio ndani ya hifadhi hiyo iliyo ndani ya maajabu makubwa ya dunia.
Huyu wanasema amejitengea ngome yake baada ya kufukuzwa na mwenzake mwenye nguvu zaidi,ubabe si kwa binadamu hata wanyama unatawala,hata hivyo anaendesha maisha kwa tahadhari kubwa ya kushambuliwa na wanyama walao nyama .
Watalii wa ndani na nje ya nchi nao walikuwa wakiendelea na kufurahia uumbaji wa Mungu kama inavyoonekana,
Wanyama ndani ya hifadhi hii ni marafiki wa watu kwa kuwa wanaishi kwa amani ,wanalindwa ,hawabughudhiwi na majangili,kama unavyoona Twiga hana wasiwasi wageni mbalimbali ikiwemo sisi tulifaidi na kupiga picha kwa karibu sana.
Simba akiendelea na msosi wake kama inavyoonekana,inasemekana uwindaji hufanywa na simba jike na watoto mzee wa kaya kama huyo husubiri kula baadae ,kama inavyoonekana inaonekana waliowinda baada ya kushiba naye akajisogeza kufaidi msosi.
Anajipumzisha karibu na msosi wake.
Utalii una raha yake kama inavyoonekana.
Simba akiwa amejipumzisha juu ya mti,kumbe ukifukuzwa na simba asiamini kupanda juu ya mti kuwa utakuwa salama ,aliyeko juu mfuate huko huko,anaweza kukufuata,lakini ndani ya hifadhi hiyo ni wapole sana.
Wageni mbalimbali wakipiga picha simba aliyepanda juu ya mti,nasi tulifanikiwa kuwanasa wakifuatilia tukio hilo lililowavuta watalii wengi kama inavyoonekana.
Kila mmoja anajitahidi kupata picha kadri ya mtambo wake.

Pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha kila siku miundo mbinu ndani ya hifadhi hiyo haijaathirika sana kutokana na matengenezo wanayofanya ,magari yaliweza kupita bila shida,
Eneo hilo kuna chui juu ya mti wageni wanafuatilia kwa kupiga picha ,hao ni miongoni mwa wanyama wanaojificha sana lakini ilikuwa rahisi kuwaona ndani ya hifadhi hiyo.
Picha picha kila mmoja kwa kadri alivyojiandaa.
Mbuni wanaendelea na maisha yao.
Twiga akila chakula kwa juu,hana wasiwasi
Hana shaka
Nyamera akiwa ameji[pumzisha kwenye kivuli baada ya kujipatia chakula.
Mpiga picha wetu naye baadae alipigwa picha katika eneo alilokuwa na mapenzi nalo

Mwongoza wageni katika kituo cha utalii cha Serengeti ambaye ni yuko kwenye mafunzo Godfrey akiwaelezea watalii wa ndani mzunguko wa wanyama hasa nyumbu na vitu vingine ndani ya hifadhi hiyo.
Hapo kuna elimu kubwa ya wanyama kila mmoja alikuwa makini kufuatilia.
Taarifa mbalimbali za utalii na uhifadhi zinapatikana katika kituo hicho.
Hapo si gwaride bali imetokea tukawakuta wamesimama kwa pamoja ,ndani ya hifadhi hiyo wanyama wana mitindo mbalimbali ya kuvutia,kusimama,kulala na hata kucheza kiduku.

Kila kilichomo humo kina historia yake ,hapa anaelezea mifupa ma mafuvu ya wanyama hao ni aina gani walipatikana lini na wapi,


Bwawa la viboko na Mamba























Godfrey akitoa elimu katika matukio tofauti juu ya utalii na uhifadhi


















Hapo kumejengwa historia ya uhifadhi kwa hao wahifadhi wetu waliokwisha tangulia mbele ya haki,tunatakiwa kuwaenzi milele kwa kutunza maliasili zetu.







Wanaangalia viboko na mamba
Wako ndani ya himaya yao
Wakiwa ndani ya makazi yao,yote unayapata ndani ya hifadhi hiyo.




0 comments:

Post a Comment