Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mwalimu Marwa Ryoba amewakumbuka wafungwa na mahabusu wa gereza mahabusu Mugumu kwa kuwapa sabuni maboksi 30,ndizi za kula,fedha na kuahidi kuwanunua jozi mbili za Tv,hapo mzigo unashushwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Porini kama inavyooneka.
Matunda ni muhimu kwa afya zao,hilo nalo lilizingatiwa kama inavyoonekana
Anakabidhi sh 100,000 kwa ajili ya mahitaji mengine kwa wafungwa na mahabusu,pia amesema halmashauri ya wilaya hiyo itashirikiana na uongozi wa gereza hilo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa choo cha wafungwa katika gereza hilo.
Ameahidi kufikisha changamoto zinazowakabili wafungwa na mahabusu kwa waziri wa mambo ya ndani ,ili ziweze kupatiwa majawabu ikiwemo mazingira ya askari hao.
sisi sote ni kitu kimoja, hata kama tuko mazingira tofauti kwa leo ila kesho twaweza keti pamoja kama familia moja. Ni jambo jema kwa Mhe. Mbunge kuwakumbuka wafungwa na Mahabusu katika gereza la mahabusu Mugumu/Serengeti.
ReplyDelete