Fahari ya Serengeti

Friday, December 25, 2015

WAKAZI WA KITONGOJI CHA MCHURI KJJ CHA KENYANA W.SERENGETI MKOA WA MARA WAOMBA HATI YA MWEKEZA JI IFUTWE ILI ARDHI HIYO WAPEWE WANANCHI




 Mbunge wa jimbo la Serengeti Mwalimu Marwa Ryoba aliungana na wananchi hao kumtaka waziri wa Ardhi na Makazi afute hati ya mwekezaji wa shamba la Kenyana aliyechukua hati mwaka 1988 mpaka sasa hajawahi kulima ngano wala kuendeleza,na wananchi walioko eneo hilo wamejenga shule lakini haijafunguliwa kwa madai kuwa eneo hilo ni la mwekezaji na wao wameishi huko kwa zaidi ya miaka 18.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Mchuri Fransic Nyantori
 Diwani wa kata ya Ring'wani Maiso Mahemba naye aliungana na wananchi wake ili ardhi irudi kwa wananchi kwa kuwa haizalishi na wananchi wanakosa ardhi ya kulima ,kuchungia
 Mmoja wa wanafunzi ambaye hajaandikishwa kuanza shule ya msingi baada ya shule waliyojenga wananchi katika kitongoji hicho kukataliwa kufunguliwa na uongozi wa kijiji kuwa ilijengwa kwenye eneo la mwekezaji,shule iliyoko jilani ni kilometa 12 umbali ambao unawawia vigumu kwenda kusoma,na wakati wa mvua kuna mito mikubwa hawawezi kuvuka




 Kaimu afisa elimu wilaya Wanyancha Nyakoge anasema watoto hao wana haki ya kupata elimu hivyo kupitia mwongozo wa elimu namba 5 wa mwaka huu watahakikisha kunaanzishwa kituo maalum,maarufu kama elimu shikizi ili waweze kupata elimu kabla ya mgogoro huo wa eneo haujapatiwa ufumbuzi
 Ni baadhi ya mito huwazuia watoto kuvuka kwenda shule nyingine wakati wa mvua



0 comments:

Post a Comment