Mafundi na vibarua wa kampuni ya Sama Investment ya mjini Mugumu Serengeti wakichimba na kujenga mtaro katika barabara ya mjini Mtaa wa Sedeco,kampuni hiyo inajenga kwa gharama zake ili kuwanusuru wananchi waliko pembezoni mwa barabara hiyo wanaoathirika na maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Hapa kazi tu mambo yanaendelea
Akina mama wauza nafaka eneo la Sedeco mjini Mugumu wakiwa wanaendelea na biashara yao,kopo moja huuzwa sh 3,000 na debe sh 15,000 la mahindi.wanatakiwa kukumbukwa pindi mamilioni ya Magufuli yakianza kutoka.
Katibu tawala Mkoa wa Mara Benedict ole Kuyan akiongea na wanufaika wa Mpango wa kusaidia kaya maskini kijiji cha Machochwe,wakati alipokuwa akikagua utekelezaji wa mpango huo kwa jamii.
Nunueni kuku ili muweze kuzalisha taratibu ,hii ni mbegu imepandwa inatakiwa kumea na kustawi
Mtaribu wa Tasaf Mkoa wa Mara akitoa maelekezo kwa wakazi wa kijiji cha Machochwe.
Mkuu wa wilaya Ally Mafutah akitoa maelezo ya hali ya wilaya,walivyojipanga na Hapa kazi tu.
Wanabadilishana uzoefu
0 comments:
Post a Comment