Fahari ya Serengeti

Friday, September 11, 2015

MATUKIO YA MWENGE SERENGETI

 Maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa na mkuu wa wilaya hiyo wa nne kutoka kushoto Ally Mafutah wakisubiri Mwenge kutoka wilaya ya Tarime.
 Wanasubiri mwenge
 Maandalizi ya mapokezi ya mwenge eneo la Mto Mara
 Brass Band ya Tanapa ilikuwepo kunogesha mapokezi na kazi nzima ya mbio za mwenge
 Wako Kikazi zaidi
 Kazi inakwenda ikiongezeka
 Wako tayari kama inavyoonekana hapo

 Makamanda wakiwa wameimarisha ulinzi
 Mkuu wa wilaya ya Tarime akiongozana na wakimbiza mwenge kwa ajili ya kukabidhi mkuu wa wilaya ya Serengeti.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Ally Mafutah Mohammed akiwa tayari kupokea Mwenge wa uhuru tayari kuwa kuanza mbio wilayani kwake.
 Nimepokea na utazindua miradi yenye thamani ya zaidi ya sh bil.3 ni maneo ya Dc.
 Anasema wako tayari kwa kuanza mbio za Mwenge wilayani hapo.
 Hapo ni ulinzi tu kama inavyoonekana
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Khatib Chum akiwa pamoja na viongozi wa wilaya ya Serengeti ,mara baada ya kupokea mwenge .
 Dc anateta jambo na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa.

 Uzinduzi wa miradi ulifanyika
 Kamanda wa Polisi wilaya ya Serengeti Omar Nasri akisoma risala kwa ajili ya Polisi Jamii,
 Kiongozi wa mbio za Mwenge akizindua Klabu ya wanafunzi wa sekondari ya Nyansurura ya  kupambana na rushwa .
 Shughuli za vikundi nazo zilitembelewa na wakimbiza mwenge kitaifa.
 Uzinduzi, Uzinduzi wa miradi ilikuwa ni mojawapo ya kazi walizofanya.
 Kazi inaendelea

 Ukakamavu ni moja ya sifa ya kukimbiza mwenge kama inavyoonekana hapo.
 Maandalizi ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya kilometa 1.5 mjini Mugumu.
 Mambo yanaenda yakiongezeka

 Anasisitiza jambo pamoja na kutoa ujumbe wa mbio za mwenge wa mwaka huu,TUMIA HAKI YAKO YA KIDEMOKRASIA ,JIANDIKISHE NA KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015.
 Waliweka jiwe la msingi ujenzi wa chuji ya Maji katika bwawa la Manchira.
 Ukaguzi wa shughuli ilikuwa ni moja ya kazi zilizofanyika.






 Wasanii nao walikuwepo.
 Wajasiliamali hawakubaki nyuma.
 Mbio za mwenge hukutanisha watu wa rika mbalimbali kama inavyoonekana hapo.
 Hata hao watoto walikuwepo kushuhudia shughuli za mwenge uwanja wa Mbuzi.




 Salamu ya Utii kwa Rais ikisomwa.

 Burudani zilikuwepo.



 Mwenge ulipokelewa kwa shamra shamra na vikundi vya burudani toka Ngorongoro katika lango la Nabi

 Burudani,burudani,burudani


 Karibu Ngorongoro
 Viongozi kutoka wilaya ya Ngorongoro wakipokea Mwenge kwa ajili ya kuanza safari mkoa wa Arusha



Wednesday, September 9, 2015

AJINYONGA KWA KAMBA BAADA YA KUKOSA NG’OMBE WA KULIPA MAHARI



Na Serengeti Media Centre
Mkazi wa kitongoji cha  Mihuru kijiji cha Kitarungu kata ya Nyansurura wilayani Serengeti Mkoa wa Mara amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba ya katani ,chanzo kikitajwa  kukosa ng’ombe wa kulipa mahari.
Polisi wilayani hapa,uongozi wa kitongoji na serikali ya kijiji umethibitisha kutokea kwa tukio hilo kati ya septemba 7 na 8 majira ya usiku,ambapo Chacha Bruna(25)mwenyeji wa kijiji cha Nyabisaga wilayani Tarime ,alijinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho  Yohana Gimano akiongea na Serengeti Media Centre kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio ,alisema Bruna aliyekuwa amefikia kwa baba yake mdogo Diabe Marwa ,alifikia uamzi huo baada ya kunyang’anywa mwanamke kwa kushindwa kulipa mahari.
“ Yeye ni Mkazi wa Tarime lakini hapa kijijini  kuna ukoo wao,alipofika hapa alimtorosha binti mmoja(Rhobi Samweli)akakaa naye kwa muda wa siku nne,septemba 7 ndugu zake walifuata huyo binti ili atoe mahari,kufuatilia akaambiwa atoe ng’ombe 9,yeye akasema anaye mmoja….wakamfukuza mpaka atoe mahari ndipo apewe mke,usiku akaamua kujiua”alisema.
Alisema kuwa kabla ya kuchukua uamzi huo akiwa na kamba  ya katani alimwambia mwanamke mmoja kwenye mji aliokuwa anaishi,kuwa haoni faida ya kuishi na kuwa siku hiyo ndiyo mwisho wake,hata hivyo hawakufualia kwa kuwa hawakutegemea kama angechukua uamzi huo.
“Asubuhi wamekuta ananing’inia kwenye mti pembeni ya barabara akiwa ameishakufa…inaonekana alijinyonga usiku ule ule ,kwa kuwa wanadai hata chakula cha usiku hawakula naye,walijua yuko katika matembezi ya kawaida”alibainisha.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kitarungu ambaye ni jilani yake alisema ,tukio hilo limebainika alfajiri wakati watu wanapita ,wakiwemo wanafunzi ,”suala la yeye kunyang’anywa mwanamke linajulikana ,na alionekana mwenye mawazo sana baada ya kushindwa kuelewana na ndugu wa mchumba wake,huenda ilimuathiri kisaikolojia na kukosa msaada wa ushauri”alisema.
Mmoja wa wahudumu wa baa iliyoko jilani na eneo la tukio ambaye hakutaka jina lake litajwe,alisema kuwa uhusiano wa Bruno na huyo binti ulikuwa wa muda mrefu ,”toka mwezi februari nilikuwa najua ni wachumba,na walikuwa wanawasiliana sana kwa simu,na  ilijulikana baadae baada ya kumtorosha na ndugu kufuatilia,”alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Philip Karangi hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo,hata hivyo Polisi wilayani hapa  wamesema uchunguzi wa tukio hilo  unaoshirikisha mganga  ili kubaini chanzo cha kifo hicho ukikamilika ndugu wataruhusiwa kuendelea na mazishi,na hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Mwisho.

MAHAFALI YA 15 CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA -KISARE WILAYA YA SERENGETI

Na Serengeti Media Centre
Ili kukabiliwa na upungufu wa wataalam katika sekta ya Afya hapa nchini,Chuo  cha Sayansi za Afya   Kisare wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kinatarajia kuanzisha kozi mbalimbali za utabibu.
Mkuu wa chuo hicho Joachim Urassa akitoa taarifa katika mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ,alisema wanatarajia kuanzisha kada za afya ,ikiwemo Stashahada ya Utabibu,Maabara,Afya ya Mazingira na Famasia.
“Leo wamehitimu wataalam 120 ngazi ya vyeti na Stashahada katika fani za Ukunga na Uuguzi,na wote wanakwenda kuhudumia jamii katika maeneo mbalimbali….lengo ni kuhakikisha wanasaidia jamii kutambua na kushughulikia matatizo yao,na tunayo matarajio ya kuongeza fani nyingine ili kupunguza tatizo la upungufu wa wataalam,”alisema.
Hata hivyo alikiri kuwepo kwa changamoto za jamii na  taasisi mbalimbali zilizopo wilayani hapo kutokujitokeza kuchangia uboreshaji wa chuo hicho,ili kukamilisha bwalo la chakula na jiko na bweni kwa ajili ya wavulana ambao wanaishi nyumba ya kupanga nje ya chuo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho,Mchungaji Abunel Mathube aliwataka wahitimu kutumia vema taaluma yao kuhudumia wananchi,”zingatieni maadili ya kazi,mmefundishwa katika chuo cha kidini,tunategemea mkawe mfano maana mnacheza na maisha ya watu,epukeni rushwa”alisisitiza.
Mapema Mkurugenzi wa hospitali Teule ya Nyerere na Chuo hicho  Dk Musuto Chirangi alisema mafanikio ya kazi ya uuguzi si visingizio bali kuwajibika kwa kuzingatia maadili kama walivyofundishwa,itakuwa imesaidia kutimiza malengo ya mafunzo hayo na kupambana na adui maradhi katika jamii.
Chuo hicho kilichoko chini ya kanisa la Menonite kilianza mafunzo 1998 na kilipata usajili wa muda baraza la Elimu ya Ufundi(NACTE) mwaka 2004,kilipata usajili wa kudumu 2009 na kinaendesha mafunzo ya uuguzi na Ukunga ngazi ya cheti na stashahada.



 Maandamano ya wanachuo kuelekea ukumbi ulioandaliwa
 Wanachuo wanaelekea ukumbini
 Maandamano yanaendelea


 Viongozi wa hospitali,wilaya na chuo wakiwa meza kuu.
 Wanachuo wakiwa wanafuatilia matukio mbalimbali.

 Wanakumbuka kiapo




Monday, September 7, 2015

KUHAMISHWA KWA MWALIMU KWAZUA TAHARUKI KWA WAZAZI

Na Serengeti Media Centre
Wakazi wa kijiji cha Mesaga kata ya Kenyamonta wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara,wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji kutohamisha walimu kwa shinikizo la watu,kwa kuwa inachangia kushuka kwa taaluma.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Chacha Getumbe amesema hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji ulioitishwa kupinga uhamisho wa Mwalimu  wa shule hiyo Jimmy Ambrose kwenda shule ya Msingi Kisaka,kuwa unatokana na kutoelewana kwa mwalimu huyo na  Padri wa Kanisa Katoliki Iramba Johnson Kitunzi.
Amesema  shule hiyo yenye wanafunzi 527 ina hitaji walimu 12 ,lakini ina walimu 6 ,na kuwa mwalimu huyo amehamishiwa kijijini hapo mwaka jana ili amuuguze mama yake ambaye ni kipofu ,kutolewa kwake watabaki  walimu watano na watoto wao wataathirika kitaaluma.
Afisa elimu wilaya William Mabanga amekiri kuwepo kwa mgogoro kati ya Padri na Mwalimu kwa masuala ya Kwaya,na kuwa ameishapokea  malalamiko ya wananchi na mwalimu mwenyewe,na kudai wamesitisha uhamisho huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Victor Rutonesha amesema suala hilo litaangaliwa upya,na kudai kuwa taratibu za uhamisho uzingatia sheria za utumishi wala si shinikizo.
Akiongea na Serengeti Media Centrea kwa njia ya Simu Padri Kitunzi amekiri kuwepo mgogoro kati yake na Mwalimu huyo,lakini amekana kuhusika na uhamisho wake kwa kuwa yeye hausiani na masuala ya serikali.

Viongozi wa kijiji cha Mesaga kata ya Kenyamonta wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kujadili hoja ya kupinga kuhamishwa kwa mwalimu wa shule ya Msingi Mesaga Jimmy Ambrose kwa shinikizo la Padri Johnson Kitunzi wa kanisa katoliki Mugumu baada ya kutoelewana.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kupinga uhamisho huo ambao wanadai una madhara kitaaluma kwa watoto wao.

Baadhi walishauri waandamane kwenda ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupinga uhamisho huo uliofanywa kwa maslahi ya mtu na kuathiri taaluma kwa watoto wao.
Wnatoa msimamo wao.