Fahari ya Serengeti

Monday, February 26, 2018

WACHIMBAJI WADOGO WAHITAJI MSAADA WA VIFAA VYA KISASA

 Dc Serengeti Nurdin Babu akiangalia kazi ya uuchenjuaji dhahabu katika mgodi wa Nemic ulioko Nyigoti ,hata hivyo kazi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa vya kisasa ikiwemo vifaa vya kujikinga kwa wanaohusika.
 Akina mama wakiponda mawe kwa  ili yapelekwe kwenye karasha, kazi hiyo wanalipwa kwa kutwa kati ya sh 4,000 hadi 10,000 kulingana na idadi ya karai.
 Kutokana na ugumu wa kazi akina mama hao huchoka kama anavyoonekana mmoja wao.



 Kazi ni kazi tu haiangalii mwanamke ama mwanamme .


 Wanachungulia kama kuna mabaki ya dhahabu
 Katika eneo hilo wanatumia kemikali aina ya zebaki ambayo ni hatari kwa viumbe hai,hata hivyo wanafanya kazi katika eneo hilo hawapewi vifaa vya kujikinga dhidi ya kemikali hiyo.

 Raphael Mwera akitoa ufafanuzi wa jinsi kazi hiyo inavyofanyika.


 Kazi inaendelea
Akina mama nao wamo,huyo ndiye anaongoza mtambo huo.

MIFUGO MARUFUKU MAENEO YA UHIFADHI

 Boniphace Chacha meneja wa Shamba la Mifugo la Vedastus Mathayo kushoto akimwomba radhi Marongoli anayemiliki eneo ambalo linatumika kwa utalii wa asili katika kijiji cha Bokore wilaya ya Serengeti baada ya kubainika kuingiza mifugo katika eneo hilona kuharibu mazingira na uoto wa asili.
Uamzi wa kuomba radhi umefikiwa baada ya Dc kubaini kuwepo ukiukwaji wa taratibu na kusababisha mgogoro kati yao,ambapo ameahidi kumkamata kama itabainika mifugo yao inaingia eneo lililohifadhiwa.
 Wanamsikiliza mkuu wa wilaya Nurdin Babu
 Tupatane majilani inaonekana Chacha akiomba baada ya kubainika mifugo yake kuingia eneo la uhifadhi mara kwa mara

DC SERENGETI ATATUA MGOGORO WA WAFUGAJI NA UHIFADHI

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Nurdin Babu akielezea msimamo wa serikali dhidi ya watu wanaokaidi taratibu zilizopo wakati akitatua mgogoro kati ya meneja wa Shamba la Mathayo na eneo la Uhifadhi la Ikoma Culture Centre katika kijiji cha Bokore.
Amesema mifugo ya Mathayo ikikutwa katika eneo la uhifadhi wa asili atamkamata meneja wake Boniphace Chacha kwa kukaidi maagizo yake na kuvunja sheria zinazolinda maeneo hayo.
 Kabla ya kutoa msimamo wa serikali wamepitia nyaraka mbalimbali na kubaini kuwa Ikoma Culture Centre ilipewa kihalali na serikali ya kijiji na hawatakiwi kuingiliwa .
 Umakini wakati wa kutatua mgogoro umetumika kwa kupitia nyaraka moja baada ya nyingine na matumizi ya eneo,hivyo mifugo ni marufuku katika maeneo ya uhifadhi wa asili.


Hatimaye muafaka ukapatikana kuwa kila mtu aheshimu eneo la mwingine

KATIKA KUHAKIKISHA WAFUNGWA WANAPATA TAARIFA MBUNGE AWAPA KING'AMUZI NA TV

 Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akikabidhi  king'amuzi na Tv Msaidizi wa gereza mahabusu Mugumu kwa ajili ya wafungwa na mahabusu ikiwa ni katika kutimiza haki ya kupata taarifa ,msaada huo una thamani ya sh 650.000=
 Askari magareza wakielezea jinsi msaada huo utakavyowasaidia mahabusu na wafungwa kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya nchi
 Anakabidhi dish la Azam
Wanapokea zawadi

Saturday, February 17, 2018

MATUMIZI YA VYOO BORA YATAPUNGUZA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA.

 Afisa afya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mugumu wilaya ya Serengeti Hellen Tupa akielezea athari za kutokutumia vyoo bora kwa wakazi wa kitongoji cha Kitahuru Kijiji cha Nyagasense ,baada ya kubainika kuwa wananchi wengi wanajisaidia vichakani.

Kupitia Mradi wa RAIN unaotekelezwa na amref health tanzania kwa kushirikiana na halmashauri kwa ufadhiliwa na Cocacola Africa Foundation ,amesema ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia kutapunguza magonjwa ya kuambukizwa ambayo yanawagharimu fedha nyingi kwa ajili ya tiba.
 Wanafuatilia maelezo yanayotolewa.
 Usafi baada ya kutoka chooni ni muhimu kwa afya.





KARIBU SERENGETI WAZIRI

 Dc Serengeti Nurdin Babu kulia akimkaribisha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prjofesa Makame Mbawala baada ya kuwasili daraja la Kimkakati la Mto Mara kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa shughuli,daraja hilo lilianza kujengwa februari 2017 na linatarajiwa kukamilika aprili mwaka huu ,limegharimu zaidi ya sh 6.8 bil
 Salaam zinaendelea
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini akimkaribisha Waziri Mbawala
 Waziri Mbawala akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba

 Rc Kigoma Malima akijadili jambo na dc Nurdin Babu
Ukaguzi

RIGHT TO PLAY YAANDAA TIMU YA KUFUNDISHA KWA NJIA YA MICHEZO

 Mwezeshaji toka Right To Play Leah Tarimo akiongoza kipindi cha Changamoto za elimu  kwa kikosi maalum kinachounda na waratibu elimu na Wadhibiti Ubora wa Elimu wilaya yaSerengeti Mkoa wa Mara ambao watahusika na kuelimisha walimu ufundishaji kwa kutumi njia ya Michezo shuleni.
 Mmoja wa  washiriki akiwasilisha kazi za kikundi
 Washiriki wakiendelea na kipindi.
 Wanafuatilia mada


 Mratibu wa Shirika la Right To Play Serengeti Idd Ramadhani akiendelea na kazi wakati wa Mafunzo ambayo yameshirikisha Waratibu Elimu na Wadhibiti Ubora wa Elimu na Afisa Michezo wilaya.
 Sophia Chamuriho Mratibu elimu kata ya Mugumu akiwasilisha kazi ya vikundi
 Burudani za hapa na pale zilikuwepo
Uwasilishaji.