Fahari ya Serengeti

Tuesday, January 31, 2017

KITUO CHA AFYA NATTA SERENGETI CHAPOKEA AMBULANCE

Dc Serengeti Nurdin Babu akitoa maelezo ya matumizi ya gari lililotolewa na serikali kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kwa Kituo cha Natta kabla ya kumkabidhi diwani wa kata hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Porini wa kwanza kulia,Ded Mhandisi Juma Hamsini,wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mwita Samweli.

Monday, January 30, 2017

SHEREHE YA JUMUIYA YA MT.MARIA MUGUMU YAFANA

Wageni waalikwa,wanakwaya na wanajumiya ya Mtakatifu Maria kigango cha Mugumu Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi Mugumu Jimbo Katoliki Mugumu wakipata chakula mara baada ya Misa Takatifu ambayo iliambatana na ubatizo wa watoto watano.

Tuesday, January 24, 2017

WATOTO 107 WAKATALIWA NA WAZAZI

 Baadhi ya watoto walioko katika Kituo cha Nyumba Salama Mugumu mjini Wilayani Serengeti ambao wamepewa hifadhi hapo baada ya mwaka jana kukimbia kukeketwa kutoka wilaya mbalimbali za  mkoa wa Mara,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya mazoezi,Jumla ya watoto 107 walikataliwa na wazazi wao na walipokelewa ni 134.

Monday, January 23, 2017

NGARIBA NA WENZAKE WAPATA WAKILI WA KUWATETEA


 Ngariba Wansato Buruna na mwenzake wakiwa mahakamani,wamepata wakili wa kuwatetea,Picha na Serengeti Media Centre

Friday, January 20, 2017

MAANDALIZI YA TUMBAKU YANAENDELEA

 Wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha Gwikongo kata ya Mbalibali wilayani Serengeti wakiendelea na maandalizi kwa ajili ya hatua ya kukausha.
Msimu unatarajiwa kufunguliwa februari 6 mwaka huu chini ya Kampuni ya Alliance One Tobacco Morogoro na bodi ya Tumbaku Tanzania.

WALIOPORA NG’OMBE WATATU WA AJUZA WAKUBALI YAISHE WAREJESHA,



Goshiyi Maduhu(72)kulia na Anna Masoya(51) wakazi wa Wagete kataya Rigicha wilayani Serengeti wakati wakiongea na Serengeti Media Centre jinsi walivyorudishiwa mifugo yao .Picha na Serengeti Media Centre.

DC SERENGETI AONGOZA TIMU KUTATUA MGOGORO PARKNYIGOTI

 Dc Serengeti Nurdin Babu wa pili kushoto akiongozana na timu ya watalaam na wananchi wa kijiji cha Parknyigoti kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu,hata hivyo viongozi wa kijiji hicho wanadaiwa kuongoza katika migogoro ya ardhi ikiwemo kujenga nyumba za kudumu katika eneo la malisho.
 Mjadala wa utatuzi wa ardhi unaendelea.



 Muafaka unatafutwa








 Dreva wa gari la Dc Serengeti Mhegete mhegete akisaidia kumzalisha ng'ombe baada ya kumkuta anahangaika katika kijiji cha Park nyigoti wilayani Serengeti.



 Ng'ombe akimsafisha ndama baada ya kuzaa.

 Wananchi wa kijiji cha Parknyigoti wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
 Dc Serengeti Nurdin Babu wa pili kulia akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji cha Parknyigoti,miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni mgogoro wa ardhi








Wednesday, January 18, 2017

APORWA MIFUGO BAADA YA KUACHANA NA UGANGA NA UNGARIBA

UKOO WAMPORA MIFUGO ALIYEAMUA KUOKOKA NA KUACHANA NA UNGARIBA,
“Wanadai ni adhabu ya kuachana na mila na desturi”
Serengeti Media Centre.
 Mkazi wa kijiji cha Wagete kata ya Rigicha wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Goshiyi Maduhu(72)aliyeporwa mifugo baada ya kuokoka.
Picha na Serengeti Media Centre.

TUMBAKU YAANZA KUUZWA KWA MAGENDO



ULANGUZI WA TUMBAKU WADAIWA KUHUSISHA MAKUNDI MBALIMBALI,
Serengeti Media Centre.



Siku chache baada ya kubainika baadhi ya wakulima wa tumbaku wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kuanza kuuza tumbaku kwa walanguzi kutoka nchi jilani ya Kenya,imebainika baadhi ya wanasiasa,wafanyabiashara na watumishi wa Kampuni ya Alliance One wanahusika.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini alisema kuwa Licha ya kuweka matangazo na kusambaza barua kwa watendaji wa vijiji na kata  kudhibiti wanunuzi ,uchunguzi wa wahusika unafanyika kwa makini ili kubaini mtandao huo.
Alisema  wamelazimika kuongeza nguvu kwenye maeneo ya vivuko ili kubaini na kudhibiti wahusika ikiwemo eneo la  Mto Mara na maeneo mengine ,”biashara hii inaweza kuwa inahusisha  watu wa kada mbalimbali ,sisi tunapambana na  watendaji  wetu  ikibainika maeneo yao  biashara hiyo inafanyika na hawachukui hatua wala kutoa taarifa lazima washughulikiwe kwa mjibu wa taratibu za utumishi,”alisema.
Hata hivyo imebainika walanguzi wa ndani ya wilaya ambao ni wanasiasa,wafanya biashara na watumishi wa kampuni ya Alliance One Tobacco hasa maafisa ugani  ndiyo wanahusika kununua tumbaku kwa sh 2,500 kwa kilo bila kuangalia daraja la zao hilo, na wakati wa msimu unaotarajiwa kuanza februari 6 mwaka huu,baadhi watauzia kampuni na  walanguzi kutoka  nchi jilani ya Kenya.
“Suala hili kila mwaka linafanyika kwa kuwa linahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa kampuni ,ndiyo maana walanguzi wanakuja kwa jeuri,kama hakutafanyika mikakati ya madhubuti halmashauri itakosa mapato na kampuni itapata hasara kwa kuwa wanadai Kenya bei ni nzuri,”kilisema chanzo chetu cha uhakika jina tunalo.
Baadhi ya maeneo yanayotajwa kuanza ununuzi wa  tumbaku kwa njia za magendo ni pamoja na Machochwe,Kebanchabancha,Musati na Nyansurura ,maeneo ambayo yanalima tumbaku kwa wingi wilayani hapa.
Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu alisema yeyote atakayekamatwa atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Zao hilo ni miongoni mwa vyanzo vya mapato ya halmashauri kutokana na ushuru wa mazao,ambapo hukusanya kati y ash 500 mil hadi 600 mil kwa msimu.
Mwisho.

AKIRI KUUZIWA NYAMA YA NYUMBU NA MPANGAJI WAKE





 MWENYENYUMBA AKIRI  MAHAKAMANI KUUZIWA NYAMA YA MYUMBU NA MPANGAJI WAKE.
Serengeti Media Centre.


Mama mwenye nyumba amekiri mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kuuziwa vipande viwili vibichi vya nyama ya nyumbu kwa thamani ya sh 2000 na mpangaji wake.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Ismael Ngaile Neema Thomas(24)mkazi wa Mtaa wa Stendi kuu baada ya kusomewa shitaka, alikiri kuuziwa nyama hiyo na Samwel Kibundali(29)mkazi wa MCU,ambaye ni mpangaji wake.
Katika kesi ya uhujumu uchumi namba 111/2016  washitakiwa Samweli Kibundali na Neema Thomas wanakabiliwa na  kosa moja la kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh.1,430,000 kinyume na kifungu namba 86 kidogo(1)na cha(2)(c)(ii)cha sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 .
Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Emmanuel Zumba mbele ya Hakimu wa Ngaile aliiambia mahakama kuwa Novemba 8 majira ya saa 7:15 mchana mwaka 2016 katika eneo la Stendi Mpya washitakiwa walikamatwa baada ya kukutwa na nyara za taifa.
Alisema Polisi walipata taarifa  kutoka kwa msiri wao kuwa kuna mtu anauza nyama pori eneo hilo ,nakumkuta mshitakiwa Samwel Kibundali akiwa  na ndoo ya plastiki ambayo ilikuwa imehifadhi nyara za serikali kinyume cha sheria.
“Katika upekuzi wa polisi nyumbani kwa mshitakiwa namba moja walikuta  vipande 30 vikavu vya nyama ya nyumbu na vipande viwili vibichi ambavyo aliviuza kwa mshitakiwa namba namba mbili”alisema.
Baada ya kusomwa hati ya mashitaka ,mshitakiwa namba moja Samwel Kibundali alikana kosa ,mshitakiwa namba mbili  Neema Thomas alikiri na kusisitiza”ni kweli aliniuzia vipande viwili vya nyama mbichi  kwa bei ya sh.2,000,maana huyu ni mpangaji wangu,”aliiambia mahakama.
Kesi hiyo imehairishwa hadi januari 23 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa kwa jamhuri kuwasilisha ushahidi wake, mshitakiwa namba moja amerudishwa mahabusu na mshitakiwa namba mbili yupo nje kwa dhamana.
Mwisho.
  

Tuesday, January 17, 2017

CWT SERENGETI WACHAGUA VIONGOZI

Baadhi ya viongozi wa Chama cha Walimu Mkoa wa Mara(CWT)wakati wa kikao cha Uchaguzi wa baadhi ya Viongozi wilaya ya Serengeti.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Uchaguzi wa viongozi wa CWT,nafasi ya Mweka hazina na mjumbe mmoja mwakilishi kutoka shule za sekondari
Katibu wa Mkoa wa CWT Saulo ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo.

Katibu wa CWT wilaya ya Serengeti Nyaoke akitoa ufafanuzi wa upigaji kura
Wanafuatilia mjadala
Wajumbe wanafuatilia uchaguzi
Kura zinapigwa

Wanahesabu kura

Mwakilishi wa CWT kwa shule za sekondari