Fahari ya Serengeti

Tuesday, March 24, 2015

Polisi msitumie nguvu kubwa - JK.



 Na Salome Kitomary
24th March 2015


 


Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu kubwa katika kukamatwa wahalifu,  badala yake kuweka mbele suala la haki za binadamu.

Rais alitoa angalizo hilo jana jijini Dar es Salaam katika Chuo Kikuu cha Polisi, wakati wa hafla ya kuwapandisha vyeo askari 290 wa Zanzibar na Bara waliomaliza mafunzo ya miezi sita.

“Ipo haja ya kutumia mbinu mbalimbali katika kuwakamatwa watuhumiwa kuliko matumizi ya nguvu kubwa, jitahidini sana kutumia nguvu kiasi ili kuhakikisha hamvunji haki za binadamu,” alisema.

Rais Kikwete aliwataka polisi kujenga mazingira rafiki na wananchi ili kurahisisha utendaji kazi ikiwamo kukabiliana na uhalifu nchini kwa kupata taarifa mbalimbali kwa urahisi.

Rais Kikwete pia alisema wizi wa mtandaoni ni tatizo kubwa na zinahitajika nguvu za ziada kupambana nalo na polisi wanapaswa kujipanga kikamilifu na kwamba kwa sasa kuna matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo inatumika kutukana, kukashfu watu jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Naliagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua dhidi ya wahusika wote wa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii,” alisema.

Aidha, alisema mauaji yanayotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi yameongezeka kutoka 2,075 mwaka 2005 hadi 3,775 mwaka 2015, hasa  mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambayo yameliabisha Taifa na kwamba zinahitajika jitihada kuyamaliza.

Awali, Mkuu wa Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, alimuomba Rais kuangalia uwezekano wa kuongeza vifaa vya kisasa kwa jeshi hilo ili liweze kutekeleza majukumu yake vizuri hasa kwa kipindi hiki ambako Taifa litashiriki kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE


Thursday, March 19, 2015

Wednesday, March 18, 2015

KIKAO KAZI CHA WARATIBU,WAHASIBU ,MAAFISA UFUATILIAJI WA MPANGO WA TASAF NA WAANDISHI WA HABARI MIKOA YA MWANZA,A NA SIMIYU JIJINI MWANZAMAR


 Waandishi wa habari na waratibu wa mpango wakifuatilia mada ukumbi wa Nyakahoja jijini Mwanza
 Wanasikiliza
 Mratibu wa Tasaf na mhasibu wake toka wilaya ya Serengeti wakifuatilia mada
 Kila mmoja alikuwa makini kusikiliza kama inavyoonekana hapo
 mada zinaendelea
 Kama ilivyoa ada kwa waandishi wa habari kusikiliza na kuandika pointi kama inavyoonekana hapo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Ladislaus Mwamanga akifungua kikao kazi
 Waandishi wa vyombo mbalimbali wakitimiza wajibu wao
 Nguli Ngesi Mwenyekiti wa mafunzo akitoa shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari
 picha ya pamoja tibu ikihusisha Tasaf Makao Makuu na waratibu wa Mpango kutoka wilaya mbalimbali
 Picha ya Pamoja
 Picha inajumuisha waandishi wa habari na uongozi wa Tasaf Makao makuu
 Picha ya pamoja
 Waandishi hasa wapiga picha husahaulika kwenye picha ya Pamoja lakini Blog hii imewakumbuka na kuwapiga picha wakiwa kazini kama inavyoonekana hapo
 Wako kikazi zaidi
 Mkurugenzi wa Tasaf na baadhi ya maafisa wake wakibadilishana mawazo
 Maswali na majibu yanaendelea
Wanaimarisha uhusiano Tasaf na waandishi wa habari