Fahari ya Serengeti

Friday, January 15, 2016

Saturday, January 9, 2016

CHADEMA YATUMBUA MAJIPU YATIMUA UANACHAMA VIONGOZI WAWILI KWA USALITI NA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

 Mwenyekiti wa Chadema wilaya Sang'uda Manawa akitoa msimamo wa kamati tendaji ya wilaya dhidi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho kutimuliwa uanachama na kupoteza nafasi zao
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Majimoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho nimiongoni mwa waliotimuliwa uanachama
 Katibuwa chama wilaya Chacha Anthony akitoa maelezo kwa nini wamefukuzwa
 Francis Msabi aliyekuwa IT wa chama naye ametumbuliwa jipu kwa kufukuzwa kwenye nafasi yake na kuvuliwa uanachama kwa kuwachafua viongozi kwenye mitandao




SIMBA WAUA NG'OMBE PARKNYIGOTI SERENGETI

Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara Mwalimu Marwa Ryoba kulia akiangalia mzoga wa ng'ombe aliyeuawa na Simba mali ya Manyeresa Nguhecha mkazi wa kijiji cha Park nyigoti kata ya Ikoma,matukio ya ng'ombe kuuawa na Simba katika kijiji hicho yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ambapo toka mwaka 2012 inadaiwa zaidi ya ng'ombe 50 wameuawa,kutoka kushoto ni mtoto wa Manyeresa,Nguhecah na katikati ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Juma Porini.
Mbunge Marwa akiwa na maafisa wa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Serengeti ,Pori la akiba la Ikorongo na wafugaji ambao ng'ombe wao waliouliwa na Simba katika kijiji cha Parknyigoti ,katika tukio hilo ng'ombe wawili waliuawa mali ya Nguhecha na Nchagasi Wantora.




Nguhecha akiangalia ng'ombe wake aliyeuawa na Simba baada ya kuvamia zizini




Mkt wa serikali ya Kijiji cha Parknyigoti Mtiro Marinya akiongozana na Mbunge na mwenyekiti wa halmashauri kwenda kushuhdia tukio la ng'ombe waliouawa na Simba

Nyma ya ng'ombe aliyeuawa na Simba baada ya kuingia zizini katika mji wa Nchagasi kijiji cha Park nyigoti


Mkazi wa kijiji  cha Park nyigoti aliambulia utumbo baada ya kuchuna ng'ombe aliyeuawa na Simba