Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara Mwalimu Marwa Ryoba kulia akiangalia mzoga wa ng'ombe aliyeuawa na Simba mali ya Manyeresa Nguhecha mkazi wa kijiji cha Park nyigoti kata ya Ikoma,matukio ya ng'ombe kuuawa na Simba katika kijiji hicho yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ambapo toka mwaka 2012 inadaiwa zaidi ya ng'ombe 50 wameuawa,kutoka kushoto ni mtoto wa Manyeresa,Nguhecah na katikati ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Juma Porini.
Mbunge Marwa akiwa na maafisa wa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Serengeti ,Pori la akiba la Ikorongo na wafugaji ambao ng'ombe wao waliouliwa na Simba katika kijiji cha Parknyigoti ,katika tukio hilo ng'ombe wawili waliuawa mali ya Nguhecha na Nchagasi Wantora.
Nguhecha akiangalia ng'ombe wake aliyeuawa na Simba baada ya kuvamia zizini
Mkt wa serikali ya Kijiji cha Parknyigoti Mtiro Marinya akiongozana na Mbunge na mwenyekiti wa halmashauri kwenda kushuhdia tukio la ng'ombe waliouawa na Simba
Nyma ya ng'ombe aliyeuawa na Simba baada ya kuingia zizini katika mji wa Nchagasi kijiji cha Park nyigoti
Mkazi wa kijiji cha Park nyigoti aliambulia utumbo baada ya kuchuna ng'ombe aliyeuawa na Simba
0 comments:
Post a Comment